Taratibu za kufunga ndoa ya Serikali (Bomani)

Sigara Kali

JF-Expert Member
May 28, 2017
3,623
8,428
Salaam kwenu wakulungwa

Baada ya kuishi kwenye mahusiano na mama watoto wangu kwa miaka 8 bila ndoa nimefikiria kufunga ndoa ya kiserikali. Nimeamua hivi ili kila mtu anendelee na imani yake kwa Amani na upendo, yeye mkristo na Mimi muislam

Sasa wajuvi wa mambo naomba mnijuze taratibu zote za kufunga hii ndoa zinavyokuwa ,Lengo niwe na ufahamu mapema kabla sijaanza kufuatilia mchakato mzima

Jumapili njema.
 
kwa nini umefikilia kufunga ndoa ya kiserikali na si ya dini?
Dini zenu tofauti sawa,kwanini mmoja wenu asibadili, miaka 8 ni mingi umezini imetosha sasa au unataka kuendelea kuwa mzinifu?
Sheria ya ndoa ya JMT kuna ndoa za aina 3 zinazotambulika,nazo ni za Kidini,Serikali na kimila,masuala ya kuonekana nadhini sijui nini kwangu hayana nafasi,nataka kila mmoja aendelee na ustaarabu wa imani yake
 
Unadhani au ni uhakika ipo hivyo?
Tafuta ukweli,lakini wewe izo mambo hazina nafasi kwako kwa hiyo ni bure ata ukihoji,
Nenda kwenye kujakwaa la sheria utakutana na watalaamu wa sheria utapewa taratibu za kufata kwa ajili kukamilisha mipango ya ndoa yako.
Ahsante kila la kheri. 🙏🙏🙏
 
kwa nini umefikilia kufunga ndoa ya kiserikali na si ya dini?
Dini zenu tofauti sawa,kwanini mmoja wenu asibadili, miaka 8 ni mingi umezini imetosha sasa au unataka kuendelea kuwa mzinifu?
mkuu unajua maana ya kuzini?
 
Sheria ya ndoa ya JMT kuna ndoa za aina 3 zinazotambulika,nazo ni za Kidini,Serikali na kimila,masuala ya kuonekana nadhini sijui nini kwangu hayana nafasi,nataka kila mmoja aendelee na ustaarabu wa imani yake
Kumbuka umesema wewe ni muislamu na unataka uendelee kubakia na uislamu ndomana jamaa akakushauri kihivyo (kiislamu)
 
Nenda halmashauri ya jiji uliopo uliza hii inshu kwa masijara wanaweza kukupa itro na niniccha kufanya
 
Ukisema ufunge ndoa ya kiserikali na mtu siyo mwislamu halafu wewe ubaki kuwa mwislamu unajidangaya kaka... kuhusu swala(swali) lako wataalamu watakusaidia tuendelee kusubiri.
 
Back
Top Bottom