Leo ndiyo najua kumbe kitendo cha kukamilisha mahari ndiyo umeshafunga ndoa ya kimila, mwaka huu navuta jiko

NetMaster

JF-Expert Member
Sep 12, 2022
1,454
4,842
Nisiwe mnafki hata kidogo, mimi ni mkristo lakini linapokuja suala la ndoa za kikristo huwa sina imani nazo, ninapoona ndoa zinafungishwa na padri au mchungaji wakati hili jambo halipo katika biblia napata mtazamo tofauti, Pia kumezuka matatizo mengi sana kwenye ndoa za kikristo.

Na ndio maana nimeamua kuoa ndoa ya kimila, hata kwenye biblia ndoa zilifungwa kwa mtindo huu huu.

Hapo zamani nilipokuwa nafikiria ndoa ya kimila basi nilikuwa nadhani inabidi uanze kufatilia mambo ya machifu wa kabila na hata kufanyiwa tambiko, kila nikifikiria haya nilikuwa naziogopa.

Basi katika kufatilia fatilia nikaona ni heri niwafate wahusika waliomo ndani ya ndoa hizi kuliko kujijengea fikra ambazo sina uhakika nazo,

Nilimtafuta muhusika mojawapo ndio akanipa ramani nzima, ni kwamba kitendo kile cha utaratibu wa kupeleka posa hadi kulipia mahari kwa tamaduni za nyumbani kwa binti ndio mchakato mzima wa ndoa ya kimila.

Kuanzia kupeleka posa kwa kumtuma utaratibu wanaoutaka wao hadi kumalizia kumtolea binti mahari kwa mtindo wa tamaduni zao kuanzia idadi ha ng'ombe, idadi ya mbuzi, n.k. hizo ni taratibu za kimila zinazokamilisha ndoa ya kimila.

kinachofuata huwa ni kumchukua binti na mnaenda kuanza maisha yenu.. FULLSTOP.

Baada ya hapo mtafuata cheti cha ndoa kwa mkuu wa wilaya ama mahakamani na kitaonyesha ni ndoa ya kimila, DEAL DONE....

Faida:

Mkigombana wasuluhishi ni pande mlizokutana, ndugu na jamaa, hao ndio washirika wenu wa karibu wanaowajua vizuri zaidi, mambo ya kuipa taasisi ambayo haijawahi hata kuja kuwasalimia jukumu la kusuluhisha ndoa ni ya ajabu.

Kuongeza mke, unaweza usiongeze mke lakini mwanamke kujua kwamba una uwezo huo kunampunguzia kiburi cha kujiona kafika na mpo sawa.

Kuenzi mila zetu, ni ndoa zinazofuata utaratibu uliotumika enzi tangu enzi, hata kwenye biblia ndoa zilifungwa kwa mtindo huu huu.

Gharama ndogo, wewe andaa mahari tu hata na kalaki 3 hivi watu wale ubwabwa.

....................

Nilichelewa mno kujua ila nashukuru sikukanyaga mtego wa ndoa ya kikristo ama ya bomani, Kama ndoa ndio zipo rahisi kihivi sioni haja yoyote ya kuendelea kufuga ukabera, Ndani ya mwaka huu itanibidi nilipie mahari jiko na kulichukulia risiti (cheti), nimepata ari mpya, nguvu mpya na kasi mpya ya kuweka jiko ndani.
 
Sawa mkuu kumbe bado unahaha haujuva jiko la gesi?
Sheria za ndoa za kikristo zinatuogopesha wengi kukwepa ndoa hasa katika ulimwengu huu wa utandawazi...

Ndoa orijino hata kwenye biblia ni za kimila,

peleka posa, wakikubali lipia mahali umchukue binti muanze maisha yenu.. mambo ya taasisi wapi na wapi aisee
 
Hivi kwa nini iwe kidini au kiserikali au kimila, kwa nini wanawake na wao wasiweke sahihi katika uchaguzi kua na yeye anaweza kuongeza wanaume huko mbele ya safari?

Najua wanaume wengi tutapinga. Sasa kwa nini sisi inaonekana kawaida tukichagua au kuongeza mke wa pili, ila si kwa wanawake?
 
3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom