daydreamerTZ

Senior Member
Sep 26, 2020
118
189
Kuna sababu kadhaa kwa nini unaweza kuamua kusajili kampuni. Hapa kuna baadhi ya faida za usajili wa kampuni:

1. Utambulisho rasmi: Usajili wa kampuni hutoa kitambulisho rasmi cha biashara yako. Hii inamaanisha kuwa unapata utambulisho tofauti na wewe kama mtu binafsi. Hii inaweza kusaidia kuweka mipaka ya kisheria kati ya biashara yako na masuala yako binafsi.

2. Ushirikiano wa kisheria: Kampuni ina uwezo wa kuwa na uwepo wa kisheria tofauti, kwa hiyo ina uwezo wa kufanya kazi kama mtu binafsi. Hii inamaanisha kuwa kampuni ina haki, wajibu, na uwezo wa kufanya mikataba, kuleta mashtaka, na kubeba madeni yake.

3. Ukuaji na uwekezaji: Usajili wa kampuni unaweza kusaidia kuvutia wawekezaji na kukuza biashara yako. Inaweza kuonyesha uwezo wako wa kuongezeka na kudumisha uwepo wako katika soko. Pia, kampuni ina uwezo wa kupata mtaji kwa njia ya uuzaji wa hisa au kukopa.

4. Uadilifu wa biashara: Kusajili kampuni kunaweza kuongeza uaminifu na uaminifu kwa wateja, washirika wa biashara, na wadau wengine. Inaweza kuonyesha kwamba una nia ya muda mrefu katika biashara yako na una kufuata miongozo na kanuni za biashara.

Ni vyema kushauriana na wataalam wa kisheria au uchumi ili kuelewa vizuri taratibu za usajili wa kampuni na jinsi faida hizi zinavyoweza kuhusiana na hali yako ya biashara.

Kwa msaada kuhusiana namasuala ya usajili BRELA iwe ni kampuni au jina la biashara wasiliana nasi kupitia namba 0629706263
 
1. Tofauti kati ya usajili wa Jina la biashara na usajili wa kampuni ni ipi
2. Je, mtu anaweza kusajili jina la biashara na kuanza kufanya biashara?
3. Je, mnaweza kushirikiana watu wawili katika kufanya biashara Kwa kuwa na usajili wa Jina Moja la biashara?
 
1. jina la biashara linatambulisha biashara Yako kwa mteja, na linakuwa chibi ya umiliki wako wewe, kisheria halina uwezo wa kujisimamia lenyewe, hii inatokea endapo mmiliki akitala kutumia jina la biashara tofaut na lake la asili. kampuni kisheria ni muunganoa wa watu wawil na kuendelea waliosajiliwa chini Cha Sheria ya makampuni ya 2002. kampuni inauwezo wa kushitaki na kushitakiwa, umiliki wake waweza kuwa limited liability au by guarantee kwa private company

2.kisheria hapana hii ni step ya kwanza kusajili jina baada ya hapo unapaswa kuwa na TIN no ya jina nwisho ni leseni ya biashara kutoka mamlaka husika na kwaa baadh ya biashara inahitajika vibali kabla ya leseni

3. ndiyo inawezekana hiyo sasa itaitwa partnership
 
Asante Sana Kwa Ufafanuzi mkuu
Pia unamshaurije mtu anayetaka kuanzisha biashara kuhusu kampuni na biashara binafisi in terms of taxes and Levy perspectively
 
Ushauri wako ni upi kati ya kampuni na biashara binafisi Kwa anayeanza biashara Kwa mtaji wa (10m-15m) katika nyanja ya Kodi, ushuru na Tozo mbalimbali?
 
mkuu Kodi ya makampuni binafsi in general ni 30% ya faida kwa mwaka wa mapato, lkn kwa majina ya biashara inategemeana na utunzaji wa taarifa , Kuna mfumo wa kukadiria Kwa wale wasiotunza taarifa na pia Kuna mfumo wa % kwa wanaotunza taarifa.
mtaji hauna nguvu Sana kwa upande wa kuamua lipi Bora kati ya kampuni au jina la biashara, zaidi kwa mtazamo wangu ni aina ya biashara unayoifanya na scale of operation yake . je utatumia self financing yako mwenye, je utakopa, je risk za biashara ni zipi? nk hivi vina nguvu zaidi ya kuamua maamuzi Yako.
sababu kwa mfano kwa jina la biashara liability yote inakuangukia mmiliki endapo utaingia matatizoni na hii ni kinyume ukilinganisha na limited co, ambapo liability ya owner ni kwa ule umiliki wake kwenye kampuni etc
pia baadhi ya banks huprefer mikopo kwa makampuni zaid
pia kampuni ni njia Bora ya kutunza mali zako nie ya mali binafsi etc

ko mkuu Kodi sio utaalamu wangu lakini nadhan nimekupa mwanga kidogo
 
1. jina la biashara linatambulisha biashara Yako kwa mteja, na linakuwa chibi ya umiliki wako wewe, kisheria halina uwezo wa kujisimamia lenyewe, hii inatokea endapo mmiliki akitala kutumia jina la biashara tofaut na lake la asili. kampuni kisheria ni muunganoa wa watu wawil na kuendelea waliosajiliwa chini Cha Sheria ya makampuni ya 2002. kampuni inauwezo wa kushitaki na kushitakiwa, umiliki wake waweza kuwa limited liability au by guarantee kwa private company

2.kisheria hapana hii ni step ya kwanza kusajili jina baada ya hapo unapaswa kuwa na TIN no ya jina nwisho ni leseni ya biashara kutoka mamlaka husika na kwaa baadh ya biashara inahitajika vibali kabla ya leseni

3. ndiyo inawezekana hiyo sasa itaitwa partnership
Sole Proprietorship
 
Je kipi bora nifungue kampuni yenye capital zaidi ya 50mil hata kama sina au nifungue yenye capital ya 2mil niliyo nayo?
fungua ya 2mil uliyo nayo mkuu, hiyo ya 50m itakuongezea liability kubwa sana kwa nyie wamiliki mambo yakienda kushoto, sababu kiuhalisia hauna, anza mdogo mdogo kampuni hukua boss ukiipata hiyo 60m utaupdate TU brela
 
Kwa nini taasisi za kifedha bado hazikopeshi makampuni hadi uwe na security hasa immovable assets kama nyumba au developed land na bonds?
 
moja ya sababu ni risk. Kutoa mikopo bila dhamana inaweza kuongeza hatari ya kutolipwa madeni, hasa kwa makampuni ambayo hatana historia nzuri ya malipo au ambayo yanakabiliwa na changamoto za kifedha.

Pia, immovable asset na bonds zinatoa uhakika zaidi kwa taasisi za kifedha. Wanapokopesha kwa msingi wa dhamana, wanaweza kuwa na uhakika kuwa wataweza kupata kurudishiwa fedha zao au kupata faida kutokana na mali au hati hizo, ikiwa mkopaji atashindwa kulipa deni.

kiufupi mkuu taasisi za kifedha zinafikiria hatari na usalama wa fedha zao.
 
Na kiuhalisia ni kwamba "the bank always has the edge" kama ilivyo kwenye makasino
 
Back
Top Bottom