Taratibu za kufuata ili kupata TIN Number

ndio maana wabongo watu wa kati na wapiga dili hawaishi,lile tangazo la msukuma halikukutosha ?
ushauri mkubwa ni ufike jieleze uambiwe ufuate maelezo lakini ni bure.
kwa hili lililotangazwa kwenye media unasita je yasiyotangazwa si ndio mnalizwa na watoto wa mjini.
 
ndio maana wabongo watu wa kati na wapiga dili hawaishi,lile tangazo la msukuma halikukutosha ?
ushauri mkubwa ni ufike jieleze uambiwe ufuate maelezo lakini ni bure.
kwa hili lililotangazwa kwenye media unasita je yasiyotangazwa si ndio mnalizwa na watoto wa mjini.
NDUGU YANGU USIDHANI ANAYEULIZA NI MJINGA SI LAZMA UJIBU UNAJUAJE KAMA MM NALIJUA TANGAZO LA HUYOO MSUKUMA ? NIMEULIZA ILI NIJUE NIPO KAZN MDA WOTE SASA KWENDA MAHALI HALAFU URUDISHWE AMA URUDI NYUMBANI KWASABABU UMEPUNGUKIWA NA KITU... NA MUDA WA KURANDARANDA KWENYE MAOFISI YA WATU SINA KWANZA KUNAKUPOTEZEANA MDA SANA NA NIMEKATA TAMAA KABISA WALIVYOSEMA HAZIFUNGULIWI JUMAMOSI NIMEUMIA SANA SANA NASIKITIKA
 
Wabongo bwana..kuingia play store na kudownload instagram au jf kila mtu anajua ila kupata TIN ya TRA hajui ataipata wapi wakati ashasema TIN ya TRA.
 
Unahitaji TIN kwa ajili ya nini? Mfano, biashara, leseni ya udereva, kutolea/kumiliki gari au pikipiki, au kulipia kodi ya majengo(property tax)? Nijibu hapo ili nikupe utaratibu.
mm na shida kwa ajili ya leseni ya udereva nisaidie
 
NDUGU YANGU USIDHANI ANAYEULIZA NI MJINGA SI LAZMA UJIBU UNAJUAJE KAMA MM NALIJUA TANGAZO LA HUYOO MSUKUMA ? NIMEULIZA ILI NIJUE NIPO KAZN MDA WOTE SASA KWENDA MAHALI HALAFU URUDISHWE AMA URUDI NYUMBANI KWASABABU UMEPUNGUKIWA NA KITU... NA MUDA WA KURANDARANDA KWENYE MAOFISI YA WATU SINA KWANZA KUNAKUPOTEZEANA MDA SANA NA NIMEKATA TAMAA KABISA WALIVYOSEMA HAZIFUNGULIWI JUMAMOSI NIMEUMIA SANA SINA NASIKITIKA
Mkuu unaposema huna muda kabisa unakosea. Wewe muda wa kufanya mambo yako unaupata jumamosi, je huyu mfanyakazi wa TRA ukitaka akuhudumie wewe mpaka jumamosi unadhani private zake yeye anazifanya lini? Mbona huyu mfanyakazi kuna huduma anazozihitaji ofisi nyingine na anajitahidi kuzipata pasipo kuathiri muda wa mwajiri wake? Panga muda wako vizuri, utapata japo nusu saa ya kufika TRA na kuhudumiwa and then urudi kufanya kazi zako. Dakika zinazotumika ku argue jf zinatosha kabisa kufika TRA ukachukua TIN yako.
 
April 08, 2016
DOMESTIC REVENUE DEPARTMENT‎
CrystalImageHandler.aspx


Re‎: ‎Application for TIN Registration‎
Dear Applicant‎;‎

The following are requirement for TIN Registration‎:‎
A‎) ‎Sole Proprietor or Individuals‎;‎
At least one of the following‎:‎
(‎i‎). ‎Birth registration certificate‎
(‎ii‎). ‎Voter registration identity‎
(‎iii‎). ‎Passport‎
(‎iv‎). ‎Affidavit from legal authority‎
(‎v‎). ‎Residential identification lellter from the Sub Ward ‎(‎Mtaa‎)‎
(‎vi‎). ‎School or university report‎
In addition two recent passport size photographs‎.‎
B‎) ‎Non Individuals‎;‎
(‎i‎). ‎For companies‎, ‎Memorandum and Articles of Association and certificate of ‎
Incorporation‎
(‎ii‎). ‎For foreign companies‎, ‎Memorandum and Articles of Association and certificate of ‎
Compliance‎
(‎iii‎). ‎For Cooperative Societies‎, ‎certificate of registration‎
(‎iv‎). ‎For Clubs and Associations‎, ‎certificate of registration‎
(‎vi‎). ‎For Partnerships‎, ‎Certificate of Registration and extract from registrar‎
(‎vii‎). ‎For Trust‎, ‎certificate of registration‎/‎incorporation as a trust‎, ‎Trust deed‎
(‎viii‎). ‎For Public Corporations‎, ‎an Establishment Act‎.‎
Together We Build Our Nation‎
Commissioner for Domestic Revenue‎
CrystalImageHandler.aspx

Mkuu unaposema huna muda kabisa unakosea. Wewe muda wa kufanya mambo yako unaupata jumamosi, je huyu mfanyakazi wa TRA ukitaka akuhudumie wewe mpaka jumamosi unadhani private zake yeye anazifanya lini? Mbona huyu mfanyakazi kuna huduma anazozihitaji ofisi nyingine na anajitahidi kuzipata pasipo kuathiri muda wa mwajiri wake? Panga muda wako vizuri, utapata japo nusu saa ya kufika TRA na kuhudumiwa and then urudi kufanya kazi zako. Dakika zinazotumika ku argue jf zinatosha kabisa kufika TRA ukachukua TIN yako.
NIPO KAZINI MKUU WANGU
 
Kama Mungu kakusaidia ukapata kaelimu hata ka cheti basi kijijini kwenu kazi wanayo haswaaa.

Sio kila kitu mtu anafahamu so anapouliza msaidie na sio kumsimanga.

Sio kosa lako unaonekana ww ni kati ya "wahaya" washamba. Ji-adjust uwe kama wenzako walioendelea.
Nani amekwambia mimi ni mhaya?ntawaita mods wakupe ban for "name calling".

Na nani amekuambia mimi nina ka elimu?na kujua TIN nayo unahitaji kaelimu ambako mleta mada yeye hana?
 
mm na shida kwa ajili ya leseni ya udereva nisaidie
Nenda TRA na copy ya kitambulisho chako. Utapewa fomu ujaze kisha upigwa picha na kuchukuliwa akama za vidole na sahihi ya kielekroniki. Baada ya hapo utapewa TIN yako.
 
TIN NUMBER YA BIASHARA SIO BURE ACHENI KUDANGANYA WATU. why sio bure? Huwezi kupata TIN number (certificate) bila kulipa with holding tax. Ukifika TRA kuomba TIN ya biashara moja ya sharti ni kuleta mkataba wa pango la biashara, ukiwapa mkataba wanakupigia with holding tax, wanakwambia kalipe kwanza hiyo ndio utapata TIN, ile kodi ya makadirio sio lazima ulipe wakati huo. Huo ndio utaratibu. Kama hauna hiyo withholding tax pesa sahau TIN. Huo ndio utaratibu niliokutana nao wakati natafuta TIN

ACHENI KUDANGANYA WATU!!!!! Si dhani kama ni lugha sahihi kutumia na hasa hasa tunapojiita GTs. Lkn naamini ungeji-homework-isha kidogo tu ungegundua TIN ni BURE. Tunalipa withoholding tax(10%) on rent sbb tumelipa kodi, vp kama ofisi/fremu ni yako mwenyewe, utalipa w/tax 10% based on what amount? Gharama uliyojengea ofisi? Mimi nilitakiwa kulipa hiyo w/tax nikawaambia silipi kodi ya pango sbb ni family premise na nilitakiwa kuthibitisha kwa kupeleka docs. Ishu ni kwamba huwez kupewa TIN wkt umekwepesha kodi yetu, w/tax lazima ilipwe kwa kila kodi ya pango utakayolipa.
Ila unaweza kutumia ujanja wa kuipunguza kwa muda lkn end of the day utatakiwa kuilipa tu.
Kama pango ni 200,000/= kwa mwez so it is 2,400,000/=kwa mwaka. therefore w/tax(10%) utakayolipa ni 240,000/=
Tafuta mkataba mwengine(utajua mwenyewe utakapo upata) utakao onyesha kodi ya pango ni 200,000/= lkn umelipa miezi miwili au mitatu yaani 600,000/= kwahiyo w/tax(10% ya 600,000) ni 60,000/=kwahiyo utakua umeipunguza kwa muda kutoka 240,000/= mpaka 60,000/= kwakweli inakera kulipa kodi kabla ujaanza biashara na kidogo ina leta saikolojiko satisfaksheni kuona badala ya kulipa 240,000 umelipa 60,000 na kuokoa 180,000/=ni nyingi sana kibiashara.
Kimsingi w/tax inabidi ilipwe na mwenye nyumba sbb yeye ndio mnufaikaji wa kodi ya nyumba lkn fanya hivyo TZ uone kama utapata hiyo nyumba au fremu yenyewe. Mpangaji ndio mwenye wajibu wa kuikata na kuiwakilisha TRA kisha receipt lazima apelekewe mwenye nyumba kama proof of payment of w/tax.
 
Nimeenda tra nimemkuta bint mmoja kanambia nitoe elfu ishirin kupata tin no
 
Nimeenda tra nimemkuta bint mmoja kanambia nitoe elfu ishirin kupata tin no
Huyo aliyekwambia umpe elfu ishirini yeye kama yeye amekosea sana. Lakini kama amrkwambia ulipie kodi hajakosea. Acha kulalamika nenda kwa boss wake hapo ofisini umuulize utaratibu wa kupata hiyo TIN na umweleze jinsi ulivyoambiwa na watumishi walioko chini yake. Atakusaidia jinsi ya kufanya.
 
Huyo aliyekwambia umpe elfu ishirini yeye kama yeye amekosea sana. Lakini kama amrkwambia ulipie kodi hajakosea. Acha kulalamika nenda kwa boss wake hapo ofisini umuulize utaratibu wa kupata hiyo TIN na umweleze jinsi ulivyoambiwa na watumishi walioko chini yake. Atakusaidia jinsi ya kufanya.
thanx! Sikutembea na hela mda huo so nikahaid ntaenda kesho kwaiyo nikimwona boss wake hata sent sitatoa?
 
Ingia tovuti ya tra, nenda ujazaji online wa tin, fuata maelekezo, ukimaliza nenda tra kuweka dole gumba. Maelezo mengine ya upatikanaji wa tin utapata tra bila wasiwasi kabisa. Ukipata tin nenda halmashauri yako kitengo cha biashara watakuelekeza ujazaji wa fomu na mengineyo, ila si bure tena ni fedha, gharama yake itategemea kule tra walikufanyia makadirio kiasi gani ya biashara yako kwa mwaka. ( wakati mwingine tra wanakwambia uende kwa tax consultant akufanyie makadirio ya mapato yako kwa mwaka, then consultant ataandika report utakayopeleka tra ili ufungue file na ulipie tax in advance).
Ndugu zangu mimi tin number ninayo nataka kufanya biashara ya miamala ya simu kama tigo pesa na m pesa Naomba kwa aliewahi kukata leseni ya biashara ya miamala ya simu anijuze ngarana ya leseni kwa biashara husika
 
Tin za sasa zinatolewa pale mahali ilipo biashara..na zinaonyesha location ya karibu naTra office..ukipata sehemu isiyo yako itakulazimu kuhamisha ,
 
Habari za muda na wakati huu,

Kuna jambo limenitatiza, naomba msaada kwa anayefahamu. Nataka kuapply for tin number nature of business ni online business na sioni haja ya kujaza location information since sitarajii kulipia kodi ya upangaji wa eneo la biashara kwani biashara nayotaka kuifanya is on my hand. Please naombeni consultation.

Je ni sahihi kujaza location while sitokuwa na physical office location?
 
online business na sioni haja ya kujaza location information since sitarajii kulipia kodi ya upangaji wa eneo la biashara kwani biashara nayotaka kuifanya is on my hand.
Pls naombeni consultation je ni sahihi kujaza location while sitokuwa na physical office location
Hapo kwenye bold, ni moja ya taarifa muhimu zinazotakiwa na mamlaka husika, ili upatiwe hiyo TIN number yako.

Nini cha kufanya:
- Tumia taarifa zilizotumika kwenye kadi yako ya mpiga kura.
- S.L.P ni muhimu - Tumia S.L.P za ofisi ya kata unapoishi.
 
Back
Top Bottom