Taratibu za kufuata ili kupata TIN Number

Kupata tin no ni lazima ufike ofisi za TRA wachukue taarifa zako upigwe picha na kuweka alama za vidole/finger print
Tin inatolewa bure kwa maelezo haya ni kwamba huwezi kupata tin no online ama passport online yakupasa kufika katika ofisi zao
 
TRA ili wakupate lazima uwe na ofisi , bila kuwa na ofisi utawezaje kupata leseni au EFD machine, kama hutaki kuwa na ofisi just proceed na biashara bila TIN
 
Kama unataka kupata Tin Number bila kuweka sehemu unayoishi ni kwenye kupata leseni ya gari/pikipiki.
 
Nenda kasajili jina la biashara Brela kwanza wakishakupa Cheti, unakipeleka TRA ukiwa na nakala ya mkataba wa ulipopanga ofisi ya biashara yako na vitu vingine kadhaa wanavyovihitaji. Watakupatia TIN

Kisha unaambatanisha Copy ya TIN, Cheti Cha Usajili ( Brela ), Mkataba wa eneo la ofisi, Copy ya kitambulisho Nk. vyote hivi unaenda navyo kwa afisa biasha katika wilaya husika huyu ndiye atakayekupatia Leseni ya Biashara.

Nimejaribu kukumbuka kumbuka, ila uwe tayari na usumbufu wa kipuuzi kutoka kwa watumishi wa umma.

USITOE WALA KUPOKEA RUSHWA TAFADHARI.
Vema kaka.....nimekuelewa vizuri.
 
TIN number hutolewa bure lakini hupewi mpaka wakukadirie kodi kulingana na biashara yako ilivyo then baada ya kulipa kodi ya awamu ya kwanza ndio wanakupa TIN number kuhusu leseni nenda manispaa ya kinondoni for more details au wadau watajazia.
Hapa umedanganya kidogo mkuu.... tin no. Unaweza ukawa nayo kwa harakat zingine tu.... sio lazima uwe na lesen ya business

Sent from "La -Vista"
 
Ndugu zangu mimi tin number ninayo nataka kufanya biashara ya miamala ya simu kama tigo pesa na m pesa Naomba kwa aliewahi kukata leseni ya biashara ya miamala ya simu anijuze ngarana ya leseni kwa biashara husika
mada kama hizi hazinaga wachangiaji kabisa, hili swali hata mie nilikuwa nalo lakini wajuzi wako bussy wanadiscuss ya tundu lissu
 
Tembelea ofisi ya TRA iliyokaribu na wewe, uombe form ya kujaza kwa ajli ya kuomba tin number, kwenye form hiyo utaainisha TIN unayomba ni ya biashara na baadae utapata TIN yako. Baada ya kuipata TIN yako utaenda kwenye kitengo cha kodi ambapo watakukadiria kodi kulingana na biashara yako na hapo utaomba utaratibu wa kupata leseni
 
Wakuu naomben kujuzwa kwa yule anayefaham namna ya kupata tii namba kwajili ya biashara . utalatibu ukoje,vigezo gan wanatumia nk
 
Wakuu naomben kujuzwa kwa yule anayefaham namna ya kupata tii namba kwajili ya biashara . utalatibu ukoje,vigezo gan wanatumia nk
Hujaeleweka mkuu
Una maanisha kupata TIN namba? Kama ndiyo unamaana hiyo! Kwa wepesi nenda ofisi za TRA zilizo jirani na eneo unalofanyia biashara utapewa fomu ambayo utajaza na itahitaji uambatanishe na vielelezo kama mkataba wa eneo lako la biashara na barua ya Mwenyekiti/Afisa mtendaji wa eneo lako.
Regards
 
WaTz wengi wavivu kusoma. Swali hili limejibiwa mapema kabisa lakini mtu anafungua thread na kutupia swali kabla ya kufuatilia mjadala wengine wamesemaje.
 
Habari wanajamvi,

Ningependa kufahamu jinsi ya kupata leseni ya biashara bila ya kuwa na ofisi.
Kutokana na nature ya biashara yangu inakuwa vigumu kuwa na ofisi kwa sababu huwa naandaa mzigo kutoka mkoani na kuupeleka moja kwa moja kwa watu walionipa order bila ya kukaa na mzigo.Sababu ya pili capital yangu ni ndogo hivyo nashindwa kulipia pango.

Naomba msaada wenu namna gani nitaweza kupata TIN na hatimaye leseni ya biashara bila ya kuwa na eneo la kazi.

Nafanya biashara ya samaki wa Mwanza ambayo nayo inahitaji leseni ya maliasili, na maliasili wamegoma kunipa hiyo leseni mpaka niwe na leseni ya biashara kutoka halmashauri.

NAWASILISHA!
 
Hio avatar yako inafurahisha mkuu..
Kuhusu leseni ya biashara na TiN, kwa mfumo wa biashara yako sidhani kama watakunyima, umejaribu kuomba?
 
Kigumu ni eneo la bihashara ,au TIN number?
Tafuta chumba ata kidogo sehemu ambayo unaweza kumudu, ata huko uswazi then endelea na mchakato.
Vinginevyo tumia mbinu ya " medani" kama ulivyoshahuriwa.
 
Back
Top Bottom