Chuck j
JF-Expert Member
- Jun 17, 2011
- 2,358
- 815
Naombeni kwa mwenye kujua jinsi ya kupata TIN Number.
Asanteni
====================================
Asanteni
HABAR WAKUUU,
Nnaomba msaada kwa anaejua ni njia zipi nizitumie kupata Tin number ya TRA kwa ajili ya kampuni, nmesajili kampuni brela la usambazaji wa vifaaa, nnahitaj nipate TIN ya mlipa kodi ndo nianze operation,,, msaada kwa mwenye ujuza tafadhar
====================================
Nenda kasajili jina la biashara Brela kwanza wakishakupa Cheti, unakipeleka TRA ukiwa na nakala ya mkataba wa ulipopanga ofisi ya biashara yako na vitu vingine kadhaa wanavyovihitaji. Watakupatia TIN
Kisha unaambatanisha Copy ya TIN, Cheti Cha Usajili ( Brela ), Mkataba wa eneo la ofisi, Copy ya kitambulisho Nk. vyote hivi unaenda navyo kwa afisa biasha katika wilaya husika huyu ndiye atakayekupatia Leseni ya Biashara.
Nimejaribu kukumbuka kumbuka, ila uwe tayari na usumbufu wa kipuuzi kutoka kwa watumishi wa umma.
USITOE WALA KUPOKEA RUSHWA TAFADHARI.
Kama ni kampuni ni hivi,
1. MOA
2. Registration
3. Extract
4. Mkataba wa mahala pa biashara ulioshuhudiwa na wakili
5. Utambulisho wa shareholders
6. Barua ya utambulisho wa serikali za mitaa pale unapofungua biashara, yaani ulipopanga
7. Kama ni pako uwe na uthibitisho
8 Picha mbili zilizogongwa mhuri wa mwenyekiti wa serikali za mitaa
9. Jiandae kulipa kodi ya mwaka huu yaani unaweza kukadiriwa 150K na kutakiwa kulipa nusu.
10. Usumbufu wa hapa na pale
ACHENI KUDANGANYA WATU!!!!! Si dhani kama ni lugha sahihi kutumia na hasa hasa tunapojiita GTs. Lkn naamini ungeji-homework-isha kidogo tu ungegundua TIN ni BURE. Tunalipa withoholding tax(10%) on rent sbb tumelipa kodi, vp kama ofisi/fremu ni yako mwenyewe, utalipa w/tax 10% based on what amount?
Gharama uliyojengea ofisi? Mimi nilitakiwa kulipa hiyo w/tax nikawaambia silipi kodi ya pango sbb ni family premise na nilitakiwa kuthibitisha kwa kupeleka docs. Ishu ni kwamba huwez kupewa TIN wkt umekwepesha kodi yetu, w/tax lazima ilipwe kwa kila kodi ya pango utakayolipa.
Ila unaweza kutumia ujanja wa kuipunguza kwa muda lkn end of the day utatakiwa kuilipa tu. Kama pango ni 200,000/= kwa mwez so it is 2,400,000/=kwa mwaka. therefore w/tax(10%) utakayolipa ni 240,000/=
Tafuta mkataba mwengine(utajua mwenyewe utakapo upata) utakao onyesha kodi ya pango ni 200,000/= lkn umelipa miezi miwili au mitatu yaani 600,000/= kwahiyo w/tax(10% ya 600,000) ni 60,000/=kwahiyo utakua umeipunguza kwa muda kutoka 240,000/= mpaka 60,000/= kwakweli inakera kulipa kodi kabla ujaanza biashara na kidogo ina leta saikolojiko satisfaksheni kuona badala ya kulipa 240,000 umelipa 60,000 na kuokoa 180,000/=ni nyingi sana kibiashara.
Kimsingi w/tax inabidi ilipwe na mwenye nyumba sbb yeye ndio mnufaikaji wa kodi ya nyumba lkn fanya hivyo TZ uone kama utapata hiyo nyumba au fremu yenyewe. Mpangaji ndio mwenye wajibu wa kuikata na kuiwakilisha TRA kisha receipt lazima apelekewe mwenye nyumba kama proof of payment of w/tax.