Ilikuwa ni siku ya tarehe 12 Dec 2011 nikiwa Oil com Ubungo nikiwa namsubiri mgeni wangua akitokea mkoani,akaja jamaa mmoja mweusi hivi,wakati nawasha gari langu,akaniomba nimpe hela,eti gari yake imeisha mafuta na pia kadi yake ya ATM imenesa kwenya ATM na hana msaada,nikamwonea huruma hasa nikijua shida ya magari, pia nikamwomba namba yake ya simu ili tutafutane na aweze kuresha hiyo elfu kumi, na hapo alikuwa ana funguo za gari na akanionesha Suzuki nikamwamini,kwa utafiti wangu binafsi nimekuja kugundua huyu jamaa anaitwa LUSAJO MWAIPYANA.Huyu jamaa ukimpigia simu hapokei akipokea anajifanya yuko mbali sana shambani na kuwa mtawasiliana baadaye ilhali hapigi simu wala nini.Chukueni tahadhari na huyu jamaa..