Chukulia tu hiyo hela umempa demu.
Watendee haki mademu.
Chukulia tu hiyo hela umempa demu.
View attachment 139269
anaitwa lusajo mwaipyana
huyu jamaa aliwahi kutolewa kwenye jamvini humu kuwa alimtapeli mtu. Utapeli wake huufanya kwenye atm za crdb. Hujifanya kadi yake imezama na huvaa smat na akimfuata mtu humwambia kuwa anafanya jeshini jkt. Taarifa zake za kweye face book zinaonyesha kuwa aliwahi either kusoma ama kufanya kazi kyela sekondari. Pia ni mtu ambaye amewahi kuishi lilongwe malawi na morogoro.
Mimi alinitapeli tarehe 31-1-2014, ilikuwa siku ya ijumaa. Nilienda kutoa pesa kwenye atm ya crdb ubungo kituo cha mafuta cha oil com. Pale kuna atm-mashine mbili za crdb. Nikamkuta analalamika kuwa kadi yake imemezwa na kwamba alikuwa na gari limemuishia mafuta. Alikuwa kavaa kofia na mavazi smati na tai. Akaniomba nimuazime 20,000/= na kwamba atanirushia baadaye. Nilimuamini kibinadamu na kumpa 20,000/= lakini kabla nilimwambia anipe namba yake ambayo ni 0653 222 215 na nilimuuliza anafanya kazi wapi. Akasema kuwa anafanya kazi jeshini mwenge ni mwanajeshi.
Kilichotokea baadaye ukimpigia simu hapokei kabisa simu. Katika kugoogle kwenye internet nimekuta malalamiko pia jamii forum kuna mtu alishawahi kumtapeli kipindi cha nyuma na inaonekana kuwa ndio mchezo wake. Ni vyema taasisi husika zikafanya uchunguzi juu ya tapeli huyu. Aidha, hii ni tahadhari kwa waamember wengine.
taarifa zake kweny e facebook
kawahi kuishi malawi lilongwe na morogoro
kasoma/kafanya kazi kyela sekondary
Ila wahusika wenyewe ndo wamejitapeli hapo:
unawezaje kutapeliwa kirahisi namna hii!
Duh jamaa toka 2011 hadi 2014 bado anatumia mbinu ile ile
we unapajua anapopaongelea au!!!Mkuu ubinadamu wako ulikuponza!
But akimtokea mtu mwengine, na aongozane nae hadi ndani tu! Ukiwa na dharura mbona kadi yako inatolewa mda huo huo!
Nakumbuka ya kwangu ilimezwa posta pale (Dar) nilichofanya, niliingia ndani na kuwaonesha tiket! Mbona walinitolea hapo hapo!
kweli mkuu usikiamini hata kivuli chako!!Rule no 1; Don't trust anybody!
Umenikumbusha tukio lililowaikunitokea mimi pia, ilikuwa jumamosi usiku kama saa 2 pale CRDB Tower branch (PPF TOWER) Nikitoa pesa ATM, wakati natoka nje nikakutana na mzungu mmoja
Akaniuliza "pls can u speek english!" nikamjibu poa... basi akaanza kunielezea kuwa kadi yake imezama kwenye ATM hile ni VISA ya nchi yake, so mpaka j5 ndio atapata huduma kwani (j2, Na j3 na j4 ilikuwa sikukuu ya iddi) so angeteseka sana na anaishi kariakoo hotelin akaniomba nimsaidie pesa ya kuishi siku hizo zote mpaka j5 na akanieleza vitu vingi n.k
Kwa huruma kabisa akaniomba atanirudishia mara mbili yanitakayompatia, basi nikaona siku zote zile nikampatia 100,000 nzima, akanipa namba yake ya simu basi nikaona maisha tayali tena mzungu....
Basi siku ya iddi nikaona nimtafute tushiriki naye, nikawa kigamboni naye vizuri kabisa tena kwa pesa yangu, wee ilivyofika jumatano nikipiga simu inaita weeeeeeeeeeeeeeeeeee mpaka, ijumaa akanipokea nakuniambia yupo mbali anakuja nilipo, yani mpaka leo simu inaita tuuuuuuuuuuuuuuuu, basi nimeamua kuacha tuuu
Kweli ni fundisho kubwa sana, sio kila msaadie anania nzuri na wewe ni bora kumpatia tu kuliko kukuazima.
Sio wabongo tu matapeli, mpaka wazungu ndani ya Tz.