Baadhi ya watu ndio wanaofanya tunaona watu wa Dar Mna Roho mbaya kwa ndugu zenu wanaokuja kuwatembelea

Mkulima na Mfugaji

JF-Expert Member
Jul 26, 2013
1,013
1,634
Naomba nitoe ushuhuda wangu niliofanyiwa na mtu wangu wa karibu

Huyu kijana tulikua pamoja katika harakati za utafutaji

Nakumbuka mimi nilikua ni miongoni mwa watu tuliokua tunamiliki magheto vijijini yale magheto ya vijijini
Huyu kijana nilikua nalala nae kwenye Ghetto langu kwani tulikua tumeshibana sana

Baada ya harakati za shule na vyuo na ajira kuwa na changamoto mimi nikasalia kijijini mwenzangu alipata kazi mjini

Ila katika kuhangaika kuna jamaa aliniunganisha kwenye kampuni moja ya kilimo na mifugo ambao iko Dar
Ile kampuni ikataka nipeleke vyeti vyangu physical na wanione

Aisee jamaa wakwanza kumjulisha alikua ni yule jamaa yangu alietoka kijijini kwetu kwamba wiki ijayo nakuja kuna mchongo nafatilia naomba unipe hifadhi ya siku mbili tu hapo kwako,kwani nilijua jamaa ana Gheto na hakua na mke

Jamaa alionyesha kufurahi na kunihakikishia sehemu ya kulala ipo na hata kula ni juu yake hata nikikaa mwezi
Mimi nikamwambia wala kuhusu chakula asihofu nimejipanga kwa hizo siku mbili na mimi dar nitakaa siku mbili tu shida yangu ni sehemu ya kulala tu kwani bajeti yangu ni ndogo

Siku ya safari inafika jamaa namwambia kesho ndio ile safari jamaa akanitoa hofu na kusema hataenda kazini ili aje anipokee

Aisee huwezi amini kuanzia kibaha napiga simu hazipokelewi na message hazijibiwi

Nilichanganyikiwa mpaka abiria niliekaa nae jirani akaniuliza kwani una nini mwanangu alikua ni mama mtu mzima ikabidi nimuelezee mwanzo mpaka mwisho

Mimi nilikua natoka Tanga ila huyu mama alipandia gari segera ila ni mtu wa Arusha

Yule mama alichonambia kama asipopokea simu Twende nyumbani kwangu akipatikana atakuja kukuchukua
Huwezi amini mpaka naingia Ubungo simu ilikua haijibiwi

Yule mama nilenda nae kwake akanitambulisha kwa familia yake

Mpaka usiku jamaa nampigia simu hola ikabidi nikae kwa yule Mama mpaka nimalize shughuli zangu nikarudi kijijini nikiwa na hasira na jamaa

Narudi kijijini nakuta habari zimezagaa kwamba nilienda kuomba kukaa kwa jamaa na ndugu zake ndio walikua wanasambaza hivyo

Nilichoka
 
Usipende kufikia kwa watu ambao hawapo vizuri kiuchumi huyo kakukwepa maana Hana Maisha hapa mjini.
 
Sasa je ulifanikiwa kupata hiyo kazi dar, na huyo jamaa yako kasahau ya zamani alafu roho yake kubwa tu, kashindwa kukusaidia hata Kama kulala chini tu, ilimladi kakupokea, baada ya hapo ulisha kutana naye? Mwisho wa ubaya aibu.
 
Back
Top Bottom