Tanzia: Smile afiwa na mama yake mzazi.

Status
Not open for further replies.
Ninasikitika
kuwataarifu kuwa mwenzetu Smile, amefiwa na mama yake siku ya alhamisi
huko Moshi na mazishi yanatarajiwa kufanyika huko huko Moshi.
Kama tujuavyo wengi wetu humu ndani tunaishi kama ndugu, rafiki, baba,
mama, shemeji, wapenzi n.k.
Kwa niaba na ridhaa yake ninachukua jukumu hili kuwapeni taarifa nyote.
Kwa kipindi hiki atakuwa akipatikana kwa namba hii 0768-036880.

Tuungane katika kumuomba Mungu amjaalie na kumuongezea nguvu katika
kipindi hiki kigumu.

Amina.

R.I.P Mama smile, Bwana alitoa Bwana ametwaa jina la Bwana libarikiwe.
 
Ninasikitika kuwataarifu kuwa mwenzetu Smile, amefiwa na mama yake siku ya alhamisi huko Moshi na mazishi yanatarajiwa kufanyika huko huko Moshi.
Kama tujuavyo wengi wetu humu ndani tunaishi kama ndugu, rafiki, baba, mama, shemeji, wapenzi n.k.
Kwa niaba na ridhaa yake ninachukua jukumu hili kuwapeni taarifa nyote.
Kwa kipindi hiki atakuwa akipatikana kwa namba hii 0768-036880.

Tuungane katika kumuomba Mungu amjaalie na kumuongezea nguvu katika kipindi hiki kigumu.

Amina.

Asante kwa taarifa Mkuu....Be of good and courageous heart Smile....Thanda's family is with you during this hard time that you are encountering.....
 
Ni habari ambayo tusingependa kuisikia.
Pole sa Smile. Maombi yangu kwako; BWANA akutie nguvu na kukupa faraja yake ktk kipindi hiki kigumu.
AMIN
 
Mungu Akupe Faraja Angalau Kupunguza Machungu,
Mungu Ampe Heri Aendako Mama Yetu,
Amina!
 
Kwa kuwa siku zote tunaamini katika kweli, kwa kuwa tunaamini kuwa kuna Mungu, hakuna sababu ya kuhuzunika sana, kwa sababu tunajua kuwa mama yetu anakwenda kuishi maisha mengine baada ya haya yenye kila aina ya matatizo.
Tunaamini mama sasa amekwenda kuishi maisha ambayo hakuna presha, wala malaria, wala ugonjwa wa namna yoyote!

R.I.P. Mama Smile
 
Last edited by a moderator:
Pole sana dadaetu Smile, Mungu ukujalie nguvu na azidi kukupa moyo mkuu, tumwombee mama ili Mungu ampumzishe pema mbinguni!!!
 
Last edited by a moderator:
Dada Smile pole sana, ni Maombi yetu Mungu azidi kuwatia nguvu na kuwaimarisha kipindi hiki kigumu sana cha kuondokewa na mpendwa wenu, pia mkapate kumaliza salama, Mungu akapate kuwa faraja yenu. Poleni sana.
 
Pole sana Smile! Roho ya Marehemu ipate rehema kwa Mungu, apumzike kwa amani. Amen!
 
Pole sana. Mungu akupe wewe na familia nzima nguvu ya kuweza kuukabili msiba huu.
 
Pole Smile, MAN PROPOSE AND GOD DISPOSE, JIPE MOYO, MUNGU ATAMFUFUA MAMA YAKO SIKU YA MWISHO.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom