Pombe ilimfanya apoteze utu wake, akose familia yake na kumzika mama yake mzazi

P Didy Wa Tanzania

JF-Expert Member
May 6, 2022
2,376
3,891
Leo nataka niwape kisa cha anko wangu moja hivi wa mtaani ambae kwa sasa ni marehemu, ubaya pia sikubahatika kwenda kumzika.

Wakati wa makuzi yangu nilibahatika kulelewa katika mtaa ambao umezungukwa na watu wenye dini. Mtaa ambao nilikuwa naishi ulikuwa na misikiti miwili, madrasa tatu na kanisa mmoja. Lakini mtaa huo huo ulikuwa na ma anko ambao pia ni walevi. Walevi ambao walikuwa wanakunywa chibuku kwa sasa wote ni marehemu, Mungu awapunguzie adhabu ya kaburi uko walipo.

1. Huyu anko wa kwanza yeye alikuwa ni mlevi na mtata, kisa cha kuja mjini na kuwa mlevi kiasi kile inasemekana alichoma msikiti huko kijijini kwao. Na alikufa kwenye jumba ambalo alijamaliziwa, siku hiyo alikunywa gongo bila kula, malaika mtoa roho akasema anko wake nyoka Mayele leo sikuachi ng' oo.

2. Huyu anko wangu wa pili yeye alikuwa mlevi lakini mnyonge, siyo mtu wa kuongea sana, alikufa baada ya kuugua kisukari na figo zilijaa maji, tumbo likamvimba akafa.

3. Huyu anko wangu wa tatu ambaye nataka kumzungumzia leo, huyu alikufa ghafla tu akiwa kasimama barabarabi, alidondoka chini ndiyo ile nipite tena, yaani alivyodondoka ndiyo akafa hapo hapo.

Sasa chanzo cha kutaka kuadithia kisa cha huyu anko wa tatu kipo hivi, huyu anko yeye kwanza ni Mzanzibar tena wale Wazanzibar wenye asili ya Kiarabu siyo kama wakina Fei Toto. Kabla hajawa mlevi alikuwa na kazi yake na mtoto wake mmoja, ila pombe ikambeba ikabidi ndugu wa mkewe waingilie kati. Jamaa akatoa talaka yule mwanamke akaolewa sehemu nyingine.

Akapindukia kwenye ulevi zaidi mpaka akakosa makazi ya kuishi, akawa analala kwenye banda la video na mchana kula yake anaipata kwa kukodi mkokoteni na kukusanya takataka majumbani.

Inasemekana siku ambayo mama yake mzazi alipokufa huyu bwana yeye hakuambiwa, kwani wosia wa mama yake mzazi wa ndugu wa huyu anko wa tatu ulisema, hata kama nikifa mtu fulani asije kwenye maziko yangu na wala asiambiwe kama naumwa.

watu wakaufata wosia, yeye akaja kupata taarifa za msiba siku tatu mbele baada ya maziko ya marehemu mama yake. Kama nilivyoanza kusema hapo awali mtaa niliolelewa ulikuwa na watu wa dini, sasa kuna tajiri mmoja alikuja na wazo la kujenga bar na bar ikajengwa pale mtaani.

Ila wazee wa mtaa wakaona hata, hili swala alipo sawa kabisa, wakaenda mahakamani kufungua shauri la malalamiko hawaitaki ile bar. Maana licha ya kuwa ile bar inaleta usumbufu wakati wa usiku miziki na walevi, pia biashara ya madada poa ilianza.

Cha kushangaza siku ya kwenda mahakamani huyu anko wangu wa tatu naye alienda mahakamani kupinga kuwa ile bar iondolewe pale mtaani. Watu tulimshangaa na tukamuuliza wewe unalewa unakuwaje leo hii unataka bar iondelewe, akajibu "Tatizo siyo sisi, tatizo watoto. Sisi ndiyo tushaharibika, tushakuwa walevi, je, na watoto wetu wawe walevi?"


Mjomba alimalizia kwa kusema "Ebu nenda kasome Surah Ya - Sin aya ya 12. au nenda kasome Mwanzo 1: 31." Baada ya siku hiyo sina kumbukumbu nyingine ya kukutana na yule anko wa tatu, ila nilisikia tu kuwa kaacha pombe na kaoa. Baadae nikasikia kuwa anko kashafariki, kadondoka tu chini kafariki.

"Mungu akupunguzie adhabu ya kaburi Anko MO."
 
Kama katubia mungu anasamehe hyo ndo maana ya kuomba kuwa na mwisho mwema.. inshallah mungu amuhifadhi.
 
Back
Top Bottom