Mchezaji wa Yanga Mamadou Doumbia, amefiwa na Baba yake mzazi huko Mali

Mributz

Senior Member
Aug 29, 2022
112
388
1681478106365.png

Picha: Mamadou Doumbia

TANZIA: Klabu ya Yanga imepokea kwa masikitiko taarifa ya kifo cha Baba mzazi wa mchezaji wake beki, Mamadou Doumbia, kilichotokea jana, nchini Mali.

Mamadou Doumbia anatarajia kusafiri asubuhi leo kuelekea Mali kwa ajili ya kushiriki taratibu za mazishi.

“Kwa niaba ya Wanachama, Wapenzi na Mashabiki wa Yanga, Uongozi wa Klabu ya Yanga unatoa pole kwa mchezaji wetu Mamadou Doumbia na familia yake yote kwa msiba huu na Mwenyezi Mungu awatie nguvu kwenye kipindi hiki kigumu.” imesema Yanga SC kupitia taarifa yake kwa umma.

Mungu ailaze roho ya Marehemu mahala pema peponi. Amina.

1681478214782.png
 
Utopolo muache kutoa kafara
Kama kafara tungemtoa yeye mwenyewe.
Mambo ya makafara, kochoma víwanja, kinyumenyume hayo ni ya MAKOLO.
Sisi tunaamini kwenye kusaidia watu wenye uhitaji maalum (SADAKA) ndio uchawi wetu mkubwa.
 
Back
Top Bottom