TANZIA: Mwanamuziki Papa Wemba afariki dunia

TANZIA: Mwanamuziki Papa Wemba afariki dunia

Asubuhi ya Jumapili April 24 2016 taarifa zimeanza kusambaa juu ya kifo cha mwimbaji Mkongwe kutoka Congo DRC aitwae Papa Wemba ambaye imeripotiwa amefariki baada ya kuanguka jukwaani akiwa anatumbuiza huko Ivory Coast.
9a887fcc7e5c6aaae3992fac0fd9a16b.jpg
8a09f43b440e339830f8ed9026064187.jpg
a30cb66162b1edfa26c23afbf170e094.jpg
 
Amefarikia akiwa anatumbuizi wimbo wake wa tatu jukwaani akiwa sambamba na Magic system.Ameafariki dunia huko Abdijan Ivory Coast alikokuwa akitumbuiza kwenye tamasha.

Chanzo:Mwananchi online
 
Dah nimemkumbuka kwenye kitu alichoimba na papaa mukulu the binadamu JB Mpiana
Kibao kinachoenda kwa jina la Cavalier Solitaire, hapo ndio sauti za hao wakuu zilizipambanua
 
besti kwani kofi na papa walikuwa maadui? Mbona waliimba pamoja wimbo wake up miaka ya 80
umeshasema best kuwa miaka ya 80,walikuwa hawapatani kabisa,hata kwenye harusi ya kanisani ya Papa Wemba mwaka 2014 Koffi hakualiwa,kama Diamond na Allikiba sasa ni maadui ingawa mwanzoni walikuwa wanapatana
 
Vyuma kama yeye vimebaki vichache nadhani bozi na sikumbuki kama jose kiambukuta kama yu hai dilu dilomona aaah simaro lutumba chini panapeleka.
 
Vyuma kama yeye vimebaki vichache nadhani bozi na sikumbuki kama jose kiambukuta kama yu hai dilu dilomona aaah simaro lutumba chini panapeleka.
Na mwingine aliyebaki ni Nyoka Longo wa zaikolangalanga. Na Sam Mangwana mzee wa yo kabibi!
 
Kwani wanaokuwa Paris huwa hawafi ama?
Anyway Mungu amlaze mahala anapo stahili.
Namaanisha ni muda mfupi tu nilimwona kwenye TV akiwa Paris anahojiwa kuhusu hiyo Concert ya Abdjan,tena akasema mwezi May atakuwa Angola,na mwezi June atakuwa Nairobi,issue siyo kuwa Paris ila nilimwona akiwa buheri wa afya,kwa hujaona jinsi nilivyomalizia sentensi yangu au wewe umeona Paris tu?sema nikutafutie visa na nauli nikupe uende ukaangalie EURO CUP 2016
 
Back
Top Bottom