Tanzia: Mwanajamvi afariki Dunia.

Nafikiri ni wakati muafaka sasa kwakila mwanajamvi kuwa na mahusiano ya kweli na baadhi ya wana Jamvi wengine behind Our Fake identities ili at least tuweze kusaidiana na kupeana taarifa sahihi na muhimu za matukio kama haya. JF is a community. R.I.P WASAIMON.
 
RIP wasaimon

Nimepigiwa simu jioni hii, dakika kadha zilizopita kuwa Mwanajamvi mwenzetu anayekwenda kwa ID ya wasaimon amefariki dunia muda kama dakika 45 zilizopita, katika hospitali ya Selian hapa Arusha, na sasa hivi ndiyo anaingizwa chumba cha ubaridi.
:A S cry::A S cry:

Taarifa hizo zinasema kuwa amenguka akiwa katika harakati za kuonana na Daktari, akiwa amesindikizwa na baba yake mzazi.

Wasaimon alijiunga na jamvi 6.10.2010.

Binafsi nilikuwa nafahamiana sana na wasaimon, alikuwa ni mtu wa kutoa ushauri wa hekima sana kuhusiana na maisha ya miaka hii, na alikuwa mpiganaji asiyechoka, akitumikia kampuni mojawapo ya Tours mjini Arusha. Naelekea msibani, nitawajuza kinachojiri.
wasaimon alivinjari hapa majukwaani hadi juzi 14.01.2013, na naambiwa kuwa hadi jana alikuwa mzima wa afya.
Ameacha Mke na watoto 3.

Mungu Ilaze Roho ya Marehemu wasaimon Mahala Pema Peponi.

Baadhi ya comment za wanajamvi:

1.
user-online.png
Janjaweed
he was positive, God fearing, blessed na wa kupeana moyo. Its a loss, hasa kwa wakati huu ambao JF imejawa zaidi na watu type yangu

2.
user-online.png
KABOBA

kaka hayo hapo juu ndio maneno yako ya mwisho kwangu! Akilini kwangu yatakaa! Na moyoni kwangu nitayaweka ,,nitajitahidi kwa nguvu zangu zote na kwa akili zangu zote na kwa moyo wangu wote nihudhurie mazishi yako! Japo nikuone kwa mara ya kwanza na ya mwisho ndugu yangu! Ulale salama wasaimon!​



UPDATE1.
Mpaka sasa hivi (0940am)wanasubiriwa Baba zake wakubwa na wadogo ili wafanye kikao cha maamuzi ya mahala pa kuzika(kuna option mbili, kuzika Arusha au Kusafirisha kwenda kwao Mbeya).
Pia aliyekuwa Mwajiri wake yuko njiani tokea Nairobi, anakuja kusaidiana na familia kupanga hatima ya marehemu.

UPDATE 2.
MAZISHI NI
JUMAMOSI (19/01/2013) HAPAHAPA ARUSHA, NADHANI KWENYE PUBLIC CEMETRY NJIRO. MTAKAOWEZA TAFADHALI TUWE PAMOJA SIKU HIYO.[/QUOTE]
 
Last edited by a moderator:
Alikuwa na ID ngapi??

RIP
Irrelevant,Childish, Nincompoopish, sluggish, crookish, absent minded question!
Wrong timing, insensitive, perpatratish kind of question!
Jifunze kukua, panga chumba, kukaa na wazazi hadi umri huo utabaki kuwa mrembo tu!
 
Back
Top Bottom