TANZIA: Mwana JF amefariki dunia

TANZIA: Mwana JF amefariki dunia

MAY GOD bless KANJUNJU it was a really nice name!
 
Raha ya milele umpe ebwana na mwanga wa milele umwangazie ampumzike kwa amani...amina
 
Hapa ndio naona umuhim wa kutumia jina kamili na sahihi.
Maana Mungu anamjua na atamuita kwa jina lake alilopewa na wazazi na sio Kanjunju.

Ningeomba Jf Mods wangekuwa kwenye usajili wanaweka Page ya mtu kujaza Profile kamili ambalo litakuwa limefichwa na Mods(Hiden profile).

Tunajifunza kutokanana matukio.

Maana hata nikienda Msikitini kusali sijui hata nimuombee vipi,ila mungu ni mjuzi zaid maana ndio ameleta yote haya na anajua liombwalo.

Ila majina kamili na kwenye profile la mtu ni muhim sana,maana hapa ingekuwa rahisi sana Mod ku retrieve data na kutupa jina kamili ili tufanye maombi kwa jina lililoandikwa mbinguni siku ya kuzaliwa na siku ya mwisho.

Na wale wote ambao aliokwazana nao kwenye baadhi ya uchangiaji wa Topics humu,basi nawaomba wamsamehe.Maana humu sote tunajuan jinsi tunavyovurugana kwenye kuchangia mada hadi kufikia kutukana.

Mungu Amlaze mahala Pema Peponi (Ameen)

Hapa majina ni siri kwa kwenda mbele, R.I.P Kanjunju.
 
Napenda kutoa taarifa hii rasmi kwa wana JF wote na Mods kwa ujumla kuwa tumeondokewa na mwanachama mwenzetu ambaye alijiunga na Jukwaaa hili tangu Octoba 2010. Alikuwa anatumia ID ya Kanjunju. Hivyo tunaomba tumwombee. Alifariki dunia katika hospitali ya Mkoa Ruvuma wiki iliyopita. RIP Kanjunju. Taarifa hii ni kwa mujibu wa ndugu wa karibu sana. Mods tunaomba katika listi yenu mumweke inactive.
poleni sana wafiwa Mumgu aiweke mahala sitahiki roho ya malehem Ameni
 
Back
Top Bottom