Benki ya Dunia yaitaka Kenya kubadili Sheria inayolazimisha Makampuni kuweka 'Server' zake ndani ya Nchi

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,376
8,120
1697831556420.png

Benki ya Dunia (WB) imeitaka Kenya kufanya mabadiliko ya Sheria inayoweka ulazima kwa kampuni Nchini humo kutunza #TaarifaBinafsi 'Data' kwenye 'Server' zilizohifadhiwa ndani ya Nchi na sio nje ya Nchi, lengo likiwa ni kurahisisha Uwekezaji wa Huduma za Kidijitali kutoka Mataifa mengine.

Kwa mujibu wa WB, Sheria hiyo inaweka vikwazo vya Kibiashara kwa Huduma za Dijitali hasa wakati ambao makampuni makubwa duniani kama vile Google, Meta, TikTok, Netflix, Oracle, Apple na Microsoft yakizidi kufungua fursa za Uwekezaji nchini humo na kuwa chanzo muhimu cha Ajira na Mapato ya Kodi.

Aidha, Benki ya Dunia imeitaka Serikali kufanya maboresho kwenye Sheria ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi pamoja na Sera ya Mfumo wa Taarifa za Afya ili kupitisha viwango vinavyolingana na vinavyoweza kushirikiana katika kuelekea Soko moja la Taarifa Binafsi la Kikanda.

Mwaka 2019 Kenya ilitunga Sheria ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi ambayo inatambua kuwa ni Taarifa Binafsi vitu vyote vinavyohusisha Rangi Asili ya Mtu, Hali ya Afya, Kabila, Dhamira, Imani, Vinasaba, Alama za Vidole, Maelezo ya Mali, Hali ya Ndoa, Majina ya Watoto, Wazazi, Mke, Mume na Jinsia ya Mtu.

Chini ya Sheria hii, Mkusanyaji au Mchakataji anaweza tu kutoa Taarifa Binafsi za Mtu nje ya mipaka kwa idhini ya Kamishna wa Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi. Kenya ni miongoni mwa Nchi 31 za Afrika kati ya 54 ikiwemo Tanzania ambazo zina Sheria za Kulinda Taarifa Binafsi.

==============
The World Bank has asked Kenya to revoke a law that forces companies to store sensitive personal data on servers located within the country as one of the ways to ease trade in digital services with other countries.

The global lender says such curbs are hindering cross-border trade in digital services.

It has asked Kenya to upgrade the current Data Protection Act and related instruments such as the Health Information System Policy to scrap requirements for data localization and adopt compatible and interoperable standards, in a move towards a single regional data market.

“In particular, Kenya may seek to reduce data localisation requirements at least for privately generated personal data within its legal framework,” said the World Bank in its Country Economic Memorandum for Kenya.

This comes at a time when thousands of digital service providers including global giants such as Google, Meta, TikTok, Netflix, Oracle, and Microsoft operate in Kenya making them a crucial cog in job creation and economic output.

As the world rapidly digitizes, data has been referred to as the “oil of the digital economy”, underlining the great power that its controllers such as banks, e-commerce firms, telecommunications companies, content sites, health facilities, schools, and digital service providers wield. To safeguard this increasingly huge volume of sensitive information being held by private entities, Kenya enacted the Data Protection Act, of 2019 which requires data handlers to host it locally in what is known localization.

Some of the sensitive data identified by the law include the natural person’s race, health status, ethnic social origin, conscience, belief, genetic data, and biometric data.

Others are property details, marital status, family details including names of the person’s children, parents, spouse or spouses, sex, or the sexual orientation of the subject.

Under the Act, data controllers or processors can only share specific sensitive information across borders with the approval of the Data Commissioner. Kenya is among 31 African countries out of the 54 that have enacted data protection laws as of February 2020.

WORLD BANK
 
Back
Top Bottom