Tanzia: LiverpoolFC afiwa na mwanae

Roho wa Bwana awape nguvu na hekima. Awape uvumilivu na subira katika mapito haya! Nawapa pole sana wewe na mama totoo!

Roho ya marehemu ipate rehema kwa Mungu, apumzike kwa amani. Amen. Bwana ametoa, Bwana ametwaa, jina la Bwana lihimidiwe!
 
Kumbuka tuliumbwa kwa udongo amerudi kuwa udongo,Lakini bwana atafufua siku ya mwisho.MUNGU AKUTIE NGUVU KIPINDI HIKI
 
Pole sana mkuu kwa kumpoteza future kamanda......Mungu ana kila sababu ya kufanya hivyo.....shukuru kwa kila jambo....Mpe pole sana mama....na Mungu awape nguvu katika kulikabili hili..........
 
WanaJF,

Napenda kuchukua fursa hii kuwajuza kuwa mwanaJF mwenzetu aitwaye LiverpoolFC amefiwa na mwanae mchanga leo asubuhi...
Mazishi yameshafanyika leo tarehe 13.12.2011.

Inna Lillah Waina Illahi Rajoon
Sisi ni wa Mwenyezi Mungu nasi Kwake tutarejea.


Ee Mwenyezi Mungu Walipe wafiwa kwa msiba huu na uwape badili yake bora kuliko huo...
 
Pole sana mzee wa liverpool, pole sana kaka.ndio mapito ya dunia. Bwana akutangulie na aukupe nguvu na uvumilivu ktk kipindi chote hiki cha kigumu kwako. Tupo pamoja
 
Pole sana Mkuu Liverpoolfc bila kumsahau Mama na wote walioguswa na tukio hilo. Mungu awape faraja
 
Pole sana ndugu yetu. Tunawaombea mungu awape moyo wa faraja wote mlioguswa na msiba!


Bwana ametoa, bwana ametwaa, jina la bwana lihimidiwe.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom