Tanzia: LiverpoolFC afiwa na mwanae

Narudi tena majira haya nikiwashukuru wote mlionitakia Kheri katika wakati mgumu niliokuwanao tangu tar.13/12/2011 mpaka hivi sasa napata kujumuika na ndugu,jamaa na marafiki,,,,,,,,,,kwa kweli janga la kufiwa ni vigumu sana kumtoka mtu moja kwa moja kwa muda mchache lakini kwa kuwa tuna mtetesi mwenye uwezo wa yote chini ya jua na juu mbingu na hakika yote haya yatapita na atatuwezesha na tutasahau pia,,,,,sitoweza kusema mengi ila si mbaya nisema kwa kidogo sana nitakayo:

(1) Ninawashukuru sana WanaJF wa Mkoa wangu kwa jinsi walivyonionyesha uwepo wao ya kwamba tupo pamoja ktk shida na raha,Hakika uwepo wao nimeitambua na nitazidi kuitambua na hilo naomba iendelee kama kawaida yetu hapa nyumbani:

(2) Sitoweza kuwataja mmoja mmoja katika furaha yangu lakini wote jueni ya kwamba ninaziheshimu sana saalam zenu kwangu:

(3) Napenda sana furaha yangu ya familia yangu imfikie Makamanda wasiochoka katika chochote mara wasikiapo jambo na siyo wengine ni Mzee wa Rula na Pakajimmy (PJ) hakika tupo wengi sana lakini kwa niaba ya hawa napenda niwapongeze na waendelee na Moyo huu huu kwani hakika tupo pamoja nao A to Z:



Tangu awali nimeshasema sitakuwa na mengi sana ya kusema zaidi ya kuwatakia kila la Kheri katika hali yoyote tunayoifikia katika mwisho wa mwaka 2011 na kuikaribisha 2012 na nina IMANI ya kwamba tuna MUNGU aliyehai na atatuvusha tu:


LiverpoolFC Member JF
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom