Tanzia: Ezekiel Malongo wa TBC afariki dunia

Tanzia: Ezekiel Malongo wa TBC afariki dunia

TBC mnatakiwa mjitathin upya yale mnayotangaza au viongozi mnaowashabikia hawajawahi kusababisha umaskini na vifo kwa wasio na hatia na maskini wanaokosa hata hela ya kununulia piritoni.

Vinginevyo wote mtapukutika.
Kuna mtu ambaye hatakufa?
 
[ Uliyosemaninkweli kbs ni ndg yangu alikuwa anaishi kitaa huku kimara nadhai alishaachishwa kz TBC QUOTE=nyumbatatu;13153477]Niliwahi kukutana naye mwaka jana, hata sikufikiria kumweka kwenye kundi la watu mashuhuri hata kwa ngazi ya mtaa. Tulikuwa tunapiga soga za siasa, kuna vitu sensitve aliviongea nikashtuka, alipoondoka nikawauliza wenzangu huyu nani, nilipoambiwa ni Ezekiel Mwalongo, sikuishia kushangaa bali pia nilihuzunishwa uchakavu aliokuwa nao, wanaomfahamu wakaongeza kuwa jamaa anapiga viroba hatari na ndio vilivyomchakaza. Mengine siyajui. so sad. R.I.P.[/QUOTE]
 
R.I.P EZe

huyu bwana hakuwa employee wa TBC anymore, pia lately alikuwa alcohol addict ,

Most of time alishinda kwa mzee mtawa.
 
poleni sana familia yote ya marehemu E. malongo. tutakukumbuka sana hasa sisi wapenzi wa mpira wa miguu hakika ulikuwa unatangaza vizuri sana.
 
Afriiiiiiiiiiiika moto!! Kombe la dunia 2002 ,Cameroon kamtandika Saudi Arabia 1 -0. Iliamsha ari ya kuendelea kusikiliza. Kwa utangazaji wa mpira wa Miguu,hata Charles Hillary atanisamehe kwa huyu marehemu.
Enzi hizo taarifa ya habari RTD ikianza ''Hii ni taarifa ya habari kutoka Radio Tanzania ........'' kabla hajajitamka jina tu basi tunashindana kutambua sauti ya mtangazaji husika. Joseph Masome,Seleman Mzee,Shaban Kisu,Juma Nkamia,Juma Ngodae,Halima Mchuka,Zawadi Machibya to mention few,tulikuwa tumewanywa' sauti zao(ila nilikuwa Messi wao katika kuwakariri(kujipa promo muhimu)). Hakika kilikuwa kizazi cha dhahabu,siku hizi shirika linaboa kama Timu ya Taifa.
RIP Ezekiel Malongo
 
Kwa nn alitoka TBC, enzi hizo niko advance alikuwa anatangaza radio free africa, then kapotea kimiaaa tusijue aliko na kipaji chake kizuuuri
 
Nakukumbuka pale Royal college of journalism urafiki baada ya kupata lecture mizinga ya konyagi inahusika, dah maisha yana mengi tangulia mkuu njia yetu sote!

Hata mi nimesoma nae pale
 
Maisha ya duniani kwa mwanadamu ni sawa na msafiri aliyepumzika chini ya mti wenye kivuli....akisubiri muda wake ufike ili aendelee na safari yake.....vifo vya wapendwa wetu vitukumbushe kuwa duniani sio makazi yetu ya milele bali ni wapita njia tu......na busara iliyokuu sio kukiogopa kifo bali ni kujiandaa na maisha baada ya kifo.....HII NI KWA WOTE WANAOAMINI......
 
kukuweka wewe sawa ni kwamba. Baada ya kutoka Rtd alikwenda Sahara media
Binafsi sijawahi kumsikia akitangaza RFA....

Asante kwa taarifa though...

Lengo langu lilikuwa ni kutaka jukwaa lielewe kwamba Malongo (R.I.P) aliondoka TBC kitambo tofauti na muanzisha mada alivyowasilisha kiasi cha kuonekana amefariki akiwa mtumishi wa TBC...
 
Kwan huyu bado alikuwepo tbc?
Nilimsikia zaman sana wakat aktangaza mpira. Kas yake kutangaza mpira hata dj halid hagus
R.I.P brother..
 
Back
Top Bottom