TANZIA: Bi Kidude afariki dunia!

TANZIA: Bi Kidude afariki dunia!

Rest In Peace Bibi Kidude!

bi+kidude.jpg


kidudee.jpg

Tukinaoooooooo!
 
Mzee wa fasjet yuko uholanzi sijui atawahi...
Na bi kidude mwenyewe mwislam hachelewi kuzikwa...
 
RIP Bi Kidude, lazima nimzike bibi huyu aliyeitangaza ZNZ ulimwenguni kote
Nimejifunza mengi kupitia nyimbo na istoria yake kwa ujumla. Mwenye enzi Mungu mwingi wa rehema amlaze mahala pema peponi
amina
 
RIP Bibi Kidude,
Poleni wote tulioguswa na Msiba huu.


Kwa Taarifa zilizopatikana punde, ni kuwa yule mwimbaji maarufu na mkongwe wa muziki wa Mwambao FATMA BINTI BARAKA alimaharufu kama Bi Kidude amefariki hii leo...

Taarifa hizo pia zimethibitishwa na ndugu wa karibu wa Bi Kidude! Chanzo cha umauti ni maradhi yatokanayo na uzee!

Bi Kidude amefariki ktk hospitali ya Hindu Mandal... Atakumbukwa kwa umahili wake ktk nyimbo za Taarabu ndani na nje ya nchi...alama ya Utamaduni wa Mzanzibar ktk matamasha ya muziki kama ZIF na Sauti za Busara.

...itakumbukwa hivi karibu Bi Kidude na baadhi ya Wanamuziki nguli kama Muhidin Ngurumo walitunukiwa Nishani ya heshima ktk mambo ya muziki pale Ikulu....

---

Wasifu Wake:

Mwanamuziki mkongwe katika Taarab Fatuma Bint Mbaraka maarufu kwa jina la Bi Kidude amefariki dunia muda mchache uliopita huko Bububu Zanzibar, sehemu alikokuwa anaugulia kwa kipindi sasa. Mwili wake utahamishiwa kwake Rahaleo na mazishi yatakuwa kesho. Bi Kidude alizaliwa katika kijiji cha Mfagimaringo, alikuwa binti wa mchuuzi wa nazi, hakuna anayejua haswa Bibi huyu alizaliwa tarehe ngapi, kuna hata mawazo kuwa alikwishafikisha miaka 102.

Katika mwaka 1920 tayari alikuwa amekwisha anza kuimba katika vikundi vya sanaa kule kwao, mwaka 1930 alijiunga na Egyptian Musical Club ya Dar es Salaam na kuzunguka miji mingi ya Tanganyika wakati ule , mwaka 1940 alirudi Zanzibar ambako awali alikuwa amekimbia kwa kuwa aliozwa kwa nguvu na mtu aliyemzidi sana umri.


Bi Kidude pia liwahi kuimba na Sitti Binti Sadi wakati wa ujana wake, na katika maisha yake Bi Kidude amekwisha zunguka mabara yote akiimba katika majukwaa na wanamuziki maarufu ulimwenguni.
 
aiseee jk kapata safari ya zanzibar...kamiss maziko ya sambeke.... RIP Bi kidude....

yoyo Mzee wa fastjet anaunganishia huko huko kutoka Amsterdam,London kwa Thatcher direct kwa Bi, Kidude na atawahi ingawa alilalamika kuwa misiba ya Kiislamu wanawahi kuzika sana na kutopata muda wa kushiriki kuzika misiba mingi kama ya Wakiristo.
 
Last edited by a moderator:
Tukiangalia kwa haraka haraka ni kwamba ana umri huu

Alianza kuimba 1920-2013 = 93
Tuseme alianza kuimba akiwa na umri wa miaka 15+93= 108

Mwenyenzi MUNGU aiweke roho ya marehemu mahala pema peponi!

Aamen!
 
Back
Top Bottom