TANZIA: Bi Kidude afariki dunia!

TANZIA: Bi Kidude afariki dunia!

Pole kwa ndugu / jamaa wafiwa na wapenzi wa muziki asilia wa mwambao. R.I.P Bi Kidude.
 
Rest In Peace Bibi Kidude!

bi+kidude.jpg


kidudee.jpg
 
So sad !
R.I.P Bi Kidude!
Mungu Amuweke mahara pema peponi...
 
Napita tena, sijui kaka atakatisha ziara Denmak,

Maana alikuwa mshkaji wake kweli, labda ataomba maziko yamsubirir subiri.

RIP Bi Kidude, mskaji wa bro.. Napita tena jamani.
 
You have done your bit in ths world and now God deemed it fit for you to take a well deserved rest.

Rest In Peace Bi Kidude; you did us proud.
 
Mwanamuziki mkongwe katika Taarab Fatuma Bint Mbaraka maarufu kwa jina la Bi Kidude amefariki dunia muda mchache uliopita huko Bububu Zanzibar, sehemu alikokuwa anaugulia kwa kipindi sasa. Mwili wake utahamishiwa kwake Rahaleo na mazishi yatakuwa kesho. Bi Kidude alizaliwa katika kijiji cha Mfagimaringo, alikuwa binti... wa mchuuzi wa nazi, hakuna anayejua haswa Bibi huyu alizaliwa tarehe ngapi, kuna hata mawazo kuwa alikwishafikisha miaka 102.
Katika mwaka 1920 tayari alikuwa amekwisha anza kuimba katika vikundi vya sanaa kule kwao, mwaka 1930 alijiunga na Egyptian Musical Club ya Dar es Salaam na kuzunguka miji mingi ya Tanganyika wakati ule , mwaka 1940 alirudi Zanzibar ambako awali alikuwa amekimbia kwa kuwa aliozwa kwa nguvu na mtu aliyemzidi sana umri.
Bi Kidude pia liwahi kuimba na Sitti Binti Sadi wakati wa ujana wake, na katika maisha yake Bi Kidude amekwisha zunguka mabara yote akiimba katika majukwaa na wanamuziki maarufu ulimwenguni
Mungu Amlaze Pema Peponi Bibi yetu. Amen
 
Back
Top Bottom