Muuza Kangala
JF-Expert Member
- Jul 21, 2021
- 2,190
- 6,905
Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza limesema Mwanaume mmoja anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka 30 hadi 35 amefariki dunia baada ya kupigwa risasi na Polisi, akidaiwa kuingia katika Benki iliyopo Rock City Mall, Mwanza.
Kwa mujibu wa taarifa ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, tukio hilo limetokea Septemba 13, 2026, saa 7 mchana ambapo Mwanaume huyo ambaye utambulisho wake bado haujafahamika, anadaiwa kuingia benki kama Mteja na kumtaka Mhudumu ampatie fedha ya kula.
Polisi imesema baada ya Mhudumu kujaribu kumpa utaratibu wa kutoa na kuweka fedha, Mwanaume huyo aliendelea kusisitiza apewe fedha, hali iliyomfanya Mhudumu kuhisi hatari na kwenda kwa Wafanyakazi wenzake kutafuta msaada.
Inadaiwa Mwanaume huyo aliruka kaunta na kuelekea kwenye vyumba vya kuhesabia fedha, akamsukuma Mhudumu na kuingia naye ndani, hali iliyozua taharuki kwa Wafanyakazi na Wateja ambapo Askari waliokuwa wakitoa ulinzi katika benki hiyo walifika na kumtaka ajisalimishe, lakini kwa mujibu wa Polisi, alikaidi amri hiyo na akitaka kuwanyang’anya silaha.
Polisi imesema Askari walimdhibiti kwa kumpiga risasi kiunoni upande wa mguu wa kulia na kusababisha jeraha lililovuja damu nyingi ambapo alibainika kuwa amefariki dunia wakati akikimbizwa Hospitalini.