Tanzania yasaini mikataba 19 ya nchi na nchi ambayo haina tija kwa Taifa

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,376
8,118
Imeelezwa kuwa Tanzania imesaini mikataba 19 ya uwekezaji wa nchi na nchi (BIT) hadi kufikia mwaka 2022, ambayo baadhi yake bado haijaridhiwa.

Akizungumza leo Agosti 02, 2023 katika mjadala wa Twitter space ulioendeshwa na Mwananchi, Mhariri wa Takwimu wa Kampuni ya Mwananchi Communications Limited (MCL), Halili Letea amesema Tanzania ina mikataba ya aina hiyo kwa lengo la kumlinda mwekezaji.

Mjadala huo umebeba mada ya ‘Je kuna tija yoyote kwa Tanzania kuendelea na mikataba ya uwekezaji wa nchi na nchi (BIT)?’

Wakati Tanzania ikiwa imeshaingia katika mikataba 19 ya uwekezaji wa nchi na nchi (BIT), Mkurugenzi Muunganiko wa Mtandao wa asasi za kiraia na vyama vya wafanyakazi (TATIC), Olivier Costa ameonya kuwa mikataba aina hiyo haina tija kwa Taifa.

Akizungumza katika mjadala wa Twitter space ulioendeshwa na Mwananchi leo Agosti 02,2023 ukibebwa na mada ‘Je kuna tija yoyote kwa Tanzania kuendelea na mikataba ya uwekezaji wa nchi na nchi (BIT)?, Costa mikataba ya aina hiyo ina vitu vingi vinavyohitaji umakini ili kunufaika.

“Mikataba ya BIT ina vipengele vingi vinavyotufanya kama nchi tusiendelee ikiwemo hata kushindwa kufanya mabadiliko ya sheria.

“Hazina tija kwetu, kesi ni nyingi ambazo zinagharimu fedha nyingi, ambazo zingetumika kwenye maendeleo,” amesema.

Katika maelezo yake, Costa ametoa mfano wa wa kesi zote ambazo Tanzania imeshatikiwa fedha nyingi zilizotumika zilipaswa kuelekezwa kusaidia kwenye maendeleo.

“Kuna nchi ambazo zimeanza kutoka kwenye hii mikataba, kama ambavyo ilifanyika kwa mkataba wetu dhidi ya Uholanzi, hili linaweza kufanyika kwa BIT nyingine,” ameshauri.

Naye Mshauri wa Biashara za Kimataifa na Uwekezaji, Jackson Roselian amesema uwepo wa mikataba ya aina hiyo, hakuangaliwi wawekezaji.

“Kikubwa wanachoangalia ni tija atakayopata kutokana na uwekezaji na hali ya usalama. Hakuna ushahidi wa kutosha kwamba mikataba ya BIT inavutia wawekezaji,” amebainisha.

MWANANCHI SPACES
 
Back
Top Bottom