Tanzania Yasaidia Kuleta Muafaka Kenya

Naomba UTUPATIE mifano hai ya hiyo Flip flop ya ODINGA

IDIMI:
Naona wewe sio mfuatiliaji mzuri wa mambo yanavyokwenda huko Kenya, hasa kuhusu huu mgogoro wa uchaguzi. Ungekuwa unauelewa mzuri usingeandika hayo hapo chini; ambayo ni kinyume kabisa na ukweli!

Idimi unahuhakika na ulicho andika au umeteleza?
Kwa Mimi ninavyo jua Ni mtu mwingine mwenye ku-short change wenzake wakikubaliana nae, na Sio Raila

Kama nitakuwa nimeteleza mtanisamehe kwani ni ubinadamu tu. Maoni yangu niliyaandika kutokana na mada zilizopita (mada ya Uchaguzi wa Kenya) za hapa hapa JF, kwamba mara ya kwanza Raila alikuwa anakataa hii nafasi ya uwaziri mkuu ambayo ilipendekezwa, akitoa sababu kwamba huko ni kukubali kwamba Kibaki alishindwa kihalali uchaguzi wa mwaka jana.
Kama nimekosea mnisahihishe.
 
Issue haikuwa kwenye nafasi ya waziri mkuu per se, issue ilikuwa ni kuwa kwenye katiba na sio makubaliano tu. Kumbuka kuwa hata 2002 Kibaki aliahidi kuwa angecreate nafasi ya waziri mkuu kwenye MoU lakini alivyopata uraisi akabadili mawazo.

Odinga hakutaka kurudia the same mistakes kama ile ambayo CUF huwa wanafanya zanzibar kwa kukubaliana na ccm kuwa uchaguzi utakaofata utakuwa huru na ikifika wakati wa uchaguzi ccm wanacheza the same game na muda mwingine kutumia jeshi kuua watu.... mambo yote kwenye maandishi!
 
Nashukuru kwa elimu hiyo.
 
..Lakini huyu ndugu kibaki hakushinda uchaguzi, sasa inakuwaje tena apewe nafasi katika mgawanyo wa madaraka??? Nini maana ya uchaguzi??? Huu mgawanyo wa madaraka utawapa jeuri viongozi ving'ang'anizi afrika kuendelea kung'ang'ania madaraka kinyume na matakwa ya wapiga kura.

Ni kweli watu wamepoteza maisha. Ni kweli watu wamepoteza mali zao, wapendwa wao nk. Lakini hii haitoi justification ya power sharing. Huyu kibaki alipaswa kufunguliwa mashtaka katika mahakama za kimataifa. Ndiyo. Ushahidi upo kwamba huyu jamaa hakushinda uchaguzi. Sasa inakuwaje leo hii anashirikishwa katika kushea madaraka. Haya ni matusi kwa watu wa kenya. Ni lesson gani nchi nyingine za africa zijifunze kutoka kenya???

Halafu la kushangaza zaidi eti Mkapa naye ni mmoja kati ya ma TX katika hiyo tume. Huku nyumbani tuhuma zinamsakama kila kukicha. Mnategemea nini hapo wakuu???

Inaonekana huu utamaduni wa magharibi hatuuwezi. Umetushinda. Tubuni utaratibu mwingine wa utawala. Shame on us Africans.
 
wewe ndio una hasira hapa baada ya juhudi za kutaka kufungia JF na kukamata wana JF kushindwa sasa umeamua kuja hapa na kuflood hii forum na pumba zako!

Kama unajua hili natumai utaacha kujikombakomba kwake kwa sasa!

Wewe vipi unamchukia kwa kuwa ulimkosa? mie nakunywa nae kahawa huyo kariakoo, wewe jee?
 
Nami naungana na wengine wote kumpongeza JK ni heshima kwa Tz na yaweza kuwa chanzo cha amani Kenya!

Annan anafanya mediation under AU ambaye Raisi wake ni JK

Hii ni nzuri kwani yaonnyesha Afrika we can solve our own problems sii lazima wazungu wahusike!

Hongera JK, Hongera TZ, Hongereni Kibaki na Raila, Hongera AEC, hongera AU

Pia tusimsahau mzee BWM na mama Grace Mandela!

Kama walivyosema wengine- sasa iwe nguvu kubwa Darfur na Somalia as Burundi, DRC na Uganda hali zimeanza sasa kutengemaa!

JK atapewa sifa when due. Kwa hili labda tumpongeze kwa kushuhudia utiaji sahihi maana ukweli ni kwamba haiwezekani makubaliana haya mazito yawe yamefikia in 2 days baada ya yeye kwenda. Ndio nasema siku zote ile nchi imekosa mafanikio ya kiuongozi kiasi kwamba inatulazimu tulazimishe na kudandia mafanikio ambayo hayapo. Bahati nzuri haya mambo hayahitaji ku-force, huwa yanakuja spontaneously.

Tumpongeze Koffi Annan kwa kuwa mvumilivu sana maana hawa jamaa wamemtesa sana hadi kufikia hapo. Japokuwa alikuwa anafanya kazi kwa mwamvuli wa UN na AU, tusisahau kuwa AU yetu ilishindwa katika hatua za awali kabisa kutatua huu mgogoro simply because viongozi wengi ndani ya AU akiwemo Rais wetu ambaye pia ni mwenyekiti wake wanakosa moral authority ya kutatua huu mgogoro maana kilichotokea ndio hicho wamekuwa wakifanya katika nchi zao bali tu wao hawakukamatwa kama mwenzao wa Kenya. Huyu BWM ndio kabisa haipaswi hata kumtaja hapa maana yeye alienda huko kuficha madhira yake, hana chochote na ninaamini akina Odinga walikuwa hata hawana muda wa kumsikiliza.

Tunawapongeza sana wananchi wa Kenya kwa kutoa shinikizo kubwa kuhakikisha viongozi wao wanakaa mezani na kutatua matatizo yaliyojitokeza. Bila shinikizo la wananchi hii ndio ingekuwa imetoka hivyo kama ilivyotokea kule kwetu. Sasa akina Maalim Seif wajue kwamba bila shinikizo la wananchi wa Zanzibar akina Makamba na Msekwa wataendelea kuwachekea hadi uchaguzi mwingine wa 2010 ambao nao watawanyang'anya ili waanze mwafaka mwingine ifikapo 2011!
 
wewe ndio una hasira hapa baada ya juhudi za kutaka kufungia JF na kukamata wana JF kushindwa sasa umeamua kuja hapa na kuflood hii forum na pumba zako!

Kama unajua hili natumai utaacha kujikombakomba kwake kwa sasa!

Hata ingekuwa kweli nnauwezo wa-kuifunga nisinge ifunga, duhhh, niifunge nikose kuona viroja kama vyako hivi? (mara nanihii mara nanihii) unanshangaza! kajisemea super,(huyu watu wa dar pale kkoo na upanga wanamjua sana, wewe nnauhakika huwezi kumjua kwa sababu nadhani umetokea moshi kama sikosei).
 
tumshukuru Mungu! Nina rafiki wengi waKenya, nilikosa raha.
So, can we safely say Mr Kibaki is now officially only a CEREMONIAL PRESIDENT? Kama wa Germany au HRE Queen of England? KT help, pls
 
Washafanikisha kuitoa mada Kenya kuipeleka Zanzibar.

Yote nini? JK asisifiwe, ama kweli kuna watu wanajuwa kuchukia.
 
Haya Mkuu wewe endelea "kunywa kahawa" na mtu mwenye ndoa!

Ukija Dar tuna kukaribisha gahwa. Tena unajuwa sie watu wa pwani tukinywa Gahwa huwa na vikoi tuu (sijui kama unajuwa kikoi?) au kwa jina lingine msuli tu, Of course huku kwetu joto sana.
 
Tunashukuru kwamba Heshima ya Tanzania mbele ya Maifa inaendelea kupaa!!!

Huu ni mtaji wetu mkubwa kwa waTanzania... hili ndilo tunaloweza tu! Tunawashukuru waliowakilisha Tanzania vizuri (BM, JK).

Tunashukuru Umoja wa Afrika kwamba kweli sasa AU yaweza maliza matatizo yetu bila kuwahitaji wajomba wa Amerika na Ulaya.

Kama kuna sehemu JK na BM wanastahili Maandamano ya Pongezi ni Hapa! na Kwa kweli kwa Majirani zetu watafurahi kwetu sisi kushangalia utulivu wao.

National Media
 
K-T,

Ahsante- sasa next important step pamoja na haya yote ni Kibaki na Raila kurejea ktk Urafiki wao kama ilivyokuwa kabla ya 2002!

Ili wakati mwingine iko shida wenyewe wawili waweze ongea kama marafiki!
 
Mwafrika wa Kike na Dar es Salaam- tunaomba ustaarabu!

Kwani hatuwezi kuchangia bila kugombana?

Magomvi yenu yanapunguza utamu wa hii thread!
 
tumshukuru Mungu! Nina rafiki wengi waKenya, nilikosa raha.
So, can we safely say Mr Kibaki is now officially only a CEREMONIAL PRESIDENT? Kama wa Germany au HRE Queen of England? KT help, pls

Thats what it looks like.
Kibaki kawa kama ceremonial President.
Muhimu ni kua Raila is executive PM
anayeongoza serikali.Hii poa kabisa maana
hapa ndipo Kibaki na watu walikua wakiiba
hela.
Huu mkataba bado mbali sana kua streamlined maana kadri
siku zinavyozidi tutapata maswala ya kutatua utata.
Mathalani iwapo kura zinapigwa na anayeshinda urais
pia naye chama chake kina viti vingi bungeni..je inakuaje.
Chukulia kama vile Raila angekua ameshinda Presidential
elections na pia awe na wabunge wengi je inakuaje.Does
he become both President and Prime Minister?..or Does the
winning party have both President and PM?What happens to
the opposition MPs when we have more than 2 parties running?
What happens when PNU affiliated Ministers pledge loyalty to
Kibaki and not Raila?

Kwa ufupi wakuu hapa bado kuna ishu za kulainishwa na pia
tujue kua huyu Kibaki bado has all the powers under the
current constitution...asije aka-rubbish kila kitu by not convening Parliament as expected...ama they can drag their
feet before any meaningful constitutional amendments are
enacted.Kwa hivyo bado kazi ipo!!!

Huu mkataba japo umeleta maelewano, siamini kama kweli
umeaddress the problem of who won the elections.Tunajua
Raila alishinda na kwa kweli angepewa jukumu la kutengeza
serikali yake na sio kugawana viti.
Naomba kuwasilisha.
 
JK atapewa sifa when due. Kwa hili labda tumpongeze kwa kushuhudia utiaji sahihi maana ukweli ni kwamba haiwezekani makubaliana haya mazito yawe yamefikia in 2 days baada ya yeye kwenda. Ndio nasema siku zote ile nchi imekosa mafanikio ya kiuongozi kiasi kwamba inatulazimu tulazimishe na kudandia mafanikio ambayo hayapo. Bahati nzuri haya mambo hayahitaji ku-force, huwa yanakuja spontaneously.

Tumpongeze Koffi Annan kwa kuwa mvumilivu sana maana hawa jamaa wamemtesa sana hadi kufikia hapo. Japokuwa alikuwa anafanya kazi kwa mwamvuli wa UN na AU, tusisahau kuwa AU yetu ilishindwa katika hatua za awali kabisa kutatua huu mgogoro simply because viongozi wengi ndani ya AU akiwemo Rais wetu ambaye pia ni mwenyekiti wake wanakosa moral authority ya kutatua huu mgogoro maana kilichotokea ndio hicho wamekuwa wakifanya katika nchi zao bali tu wao hawakukamatwa kama mwenzao wa Kenya. Huyu BWM ndio kabisa haipaswi hata kumtaja hapa maana yeye alienda huko kuficha madhira yake, hana chochote na ninaamini akina Odinga walikuwa hata hawana muda wa kumsikiliza.

Tunawapongeza sana wananchi wa Kenya kwa kutoa shinikizo kubwa kuhakikisha viongozi wao wanakaa mezani na kutatua matatizo yaliyojitokeza. Bila shinikizo la wananchi hii ndio ingekuwa imetoka hivyo kama ilivyotokea kule kwetu. Sasa akina Maalim Seif wajue kwamba bila shinikizo la wananchi wa Zanzibar akina Makamba na Msekwa wataendelea kuwachekea hadi uchaguzi mwingine wa 2010 ambao nao watawanyang'anya ili waanze mwafaka mwingine ifikapo 2011!

Mimi natoa shukrani sana kwa Annan hasa hasa maana JK na BM sijui kama wangalikuwa na la kusema mbele ya Wakenya .Waliona watanzania wakikimbilia shimoni Mombasa kukwepa mauji wakati CCM inapora madaraka .So BM hana la kuwaambia Wakenya hapa dume ni Annan.JK tangia gogoro limeanza hadi linaisha kaenda kwenye kuweka sahihi pekee .
 
Mwafrika wa Kike na Dar es Salaam- tunaomba ustaarabu!

Kwani hatuwezi kuchangia bila kugombana?

Magomvi yenu yanapunguza utamu wa hii thread!

Kweli Mkuu, nikimsifu JK huyu mdada anachukia sijui kwa nini wakati hata gazeti la Kenya limemtaja JK ndie aliyewezesha. Mnyonge mnyongeni haki yake mpeni na kama hajapewa haki yake mimi niko tayari hata kugombana kwa yeyote yule anaenyimwa haki yake Mkuu.

Kwa hiyo mwafrika wa kike akubali tuu JK kafanya kazi nzuri na anastahili sifa kwa hili.
 
K-T,

Ahsante- sasa next important step pamoja na haya yote ni Kibaki na Raila kurejea ktk Urafiki wao kama ilivyokuwa kabla ya 2002!

Ili wakati mwingine iko shida wenyewe wawili waweze ongea kama marafiki!

Mzalendohalisi,

Heshima yako upewe.
Sidhani kama Raila na Kibaki walikua marafiki
hapo awali.Wakati wa kampeni ilidhihirika wazi
kua Kibaki alikua anamtumia Raila kupata Urais.
Hili ni jambo Raila hatosahau kamwe.Hebu angalia
body language ya hawa mabwana wakati wa kutia sahihi
mkataba.Kibaki wapambe wake ni jamaa la kabila lake na
wengi wao wanachuki isio kifani dhidi ya wajaluo.Kwa hivyo
kazi ipo hapo!!
 
Kweli Mkuu, nikimsifu JK huyu mdada anachukia sijui kwa nini wakati hata gazeti la Kenya limemtaja JK ndie aliyewezesha. Mnyonge mnyongeni haki yake mpeni na kama hajapewa haki yake mimi niko tayari hata kugombana kwa yeyote yule anaenyimwa haki yake Mkuu.

Kwa hiyo mwafrika wa kike akubali tuu JK kafanya kazi nzuri na anastahili sifa kwa hili.

Weka link ya gazeti la Kenya linalo sema ni JK ndiye kawezesha jambo hili kuisha tafadhali .
 
Back
Top Bottom