Tanzania Yasaidia Kuleta Muafaka Kenya

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,040
2,000
Msichokijua... kuna ujumbe ambao ulitumwa na Marekani kwenda Ikulu yetu na kutoa pendekezo ambalo litakuwa wazi kabisa kwa Kenya kukubali. JK akiwa ndiye Mwenyekiti wa AU akaubeba ujumbe ule bila kuuchujisha. Ulipowekwa mezani hakukuwa na jinsi isipokuwa kukubali.

Hivi hamjajiuliza wakati Kofi aliweka manyanga chini na kususpend negotiations ikawaje apate moyo wa kuendelea tena. Marekani isipotaka jambo inakuwa vigumu kweli jambo hilo kufanyika. Baada ya nchi za Kiafrika kuachiliwa wajiamulie mambo yao wenyewe, Marekani ikaona isaidia katika kuamua mambo hayo.

Kwenye mkoba wa JK kulikuwa carrots na sticks zilizoandikwa "Made in USA". Walipoziona siyo Kibaki wala Raila aliyeweza kukataa...
 
Mtanzania

JF-Expert Member
May 4, 2006
4,817
2,000
JK was there kwa capacity ya Mwenyekiti wa Au na alikuwa mtu wa kushuhudia na si zaidi .Siamini kama Kenya wanaweza kumsikiliza JK ama Ben Mkapa maana wanajua yale ya Kenya yametokea Kiteto na Zanzibar kote damu ilimwagika

Mkuu Lunyungu,

Hapa inabidi kukubali na kumpa heshima yake JK. Hakuwa pale kwa ajili ya kushuhudia tu, ame play part yake tena vizuri. Vyombo vyote vya dunia vinasema hivyo.

Kwa hili tumpongeze rais wetu na labda pia tumbane. Kama ameweza kuwabana Wakenya wafikie makubaliano haraka, kwanini Zanzibar inaendelea kuchukua miaka?
 
Mtanzania

JF-Expert Member
May 4, 2006
4,817
2,000
Msichokijua... kuna ujumbe ambao ulitumwa na Marekani kwenda Ikulu yetu na kutoa pendekezo ambalo litakuwa wazi kabisa kwa Kenya kukubali. JK akiwa ndiye Mwenyekiti wa AU akaubeba ujumbe ule bila kuuchujisha. Ulipowekwa mezani hakukuwa na jinsi isipokuwa kukubali.

Hivi hamjajiuliza wakati Kofi aliweka manyanga chini na kususpend negotiations ikawaje apate moyo wa kuendelea tena. Marekani isipotaka jambo inakuwa vigumu kweli jambo hilo kufanyika. Baada ya nchi za Kiafrika kuachiliwa wajiamulie mambo yao wenyewe, Marekani ikaona isaidia katika kuamua mambo hayo.

Kwenye mkoba wa JK kulikuwa carrots na sticks zilizoandikwa "Made in USA". Walipoziona siyo Kibaki wala Raila aliyeweza kukataa...

Mwanakijiji,

Naona kama hapo juu sio sahihi. Annan ali suspend mazungumzo na wale wawakilishi wa ODM na PNU na akasema sasa atazungumza moja kwa moja na Odinga na Kibaki.

Haya ndio mazungumzo ambayo rais wetu alihusika na kuleta mafanikio.

Kitendo cha Annan kususpend mazungumzo na wale madalali kilikuwa muhimu mno. Aliamua kuwavaa Odinga na Kibaki ili mazungumzo yakivunjika, wao wawili wangebeba lawama zote.

Annan na timu yake wamefanya kazi kubwa mno, mimi nawapongeza sana wote hata wale ambao tulikuwa hatusikii majina yao.

JK hapa katumia vizuri sana nafasi yake kama mwenyekiti wa AU. Sasa Watanzania tuwe tayari kumkaba ili mazungumzo ya Zanzibar nayo yafike mwisho kwa mafanikio.
 
Kasheshe

JF-Expert Member
Jun 29, 2007
4,700
1,225
sasa kama JK ameweza kufanya muafaka Kenya kwa muda mfupi kiasi hicho, anashindwa nini kufanya hivyo hivyo ili kupata muafaka visiwani? Hongera sana kwa kazi nzuri JK. Waliopoteza maisha yao, mwenyezi mungu awalaze mahali pema hopefully hakutakuwa na vurugu nyingine za kusababisha maafa zaidi.

Very simple... kwa sababu yeye ni sehemu ya upande wenye tatizo... au kwa sababu huwezi kusukuma gari ukiwa ndani ya gari... lazima utoke nje ili usukume gari... no rocket science needed kung'amua hili.
 
Madela Wa- Madilu

JF-Expert Member
Mar 24, 2007
3,070
1,195
Wamepata Hio uPM unaosema Hume.

Raila ni Executive Prime Minister and Leader of Government Business in Parliament. Anateua yeye na kusimamia mawaziri. Yaani he is the Head of Government.

Kibaki is the President and Commander-in-Chief of the Armed Forces. Anamteua PM ambaye kwa sasa lazima awe Raila kulingana na maafikiano. In future huyu PM atakuwa kiongozi mwenye chama chake kina viti vingi zaidi bungeni. Kibaki kama Rais au hata Rais wa awamu nyingine hawezi mvuta PM huyu kazi. Yeye atasema tuu kwamba anataka kumfukuza kazi ila Bunge lazima iidhinishe kutimuliwa kazini kwa PM by majority vote yaani 114 Votes.

Kifupi:
1. Raila Odinga - Prime Minister, Head of Government and Leader of Government Business in Parliament. Atasaidiwa na Makamu wawili toka ODM, chama chake. Raila ndio anawapatia kazi maMinista na kuongoza baraza la mawaziri hawa. Hawezi kuwafuta kazi bila kushauriana na Kibaki. Lazima nusu wawe toka chama chake cha ODM na nusu toka kwa chama cha Kibaki na rafikize (PNU/KANU/ODM-Kenya).

2. Mwai Kibaki - President, Head of State and Leader of The Armed Forces. Atasaidiwa na Makamu wa Rais (Ambaye yeye ndiye anamuandika kazi na kwa sasa ni mpinzani aliyeibuka namba tatu Desemba yaani Kalonzo Musyoka wa ODM-Kenya).

3. ODM ina wingi wa wabunge bungeni.
4. ODM ina wingi wa makansela wa mabunge madogo ya miji na jiji (Municipal and County Councils). Mameya wa miji yote mikubwa ya Kenya- Nairobi, Mombasa, Nakuru, Kisumu, Eldoret, Garissa na Kakamega ni wa chama cha ODM.

Hapo juu kuna shule ya kutosha kumaliza mgogolo wa Zanzibar.

Lakini kama kawa SISIEMU ni magwiji wa kunyamazisha sauti za watu,lakini ni wepesi kutaka kubeba sifa wazizo stahili.

Kama ni kweli huko Kenya wameplay part kiasi hicho basi wamalize gogolo la Zanzibar.
 
Kasheshe

JF-Expert Member
Jun 29, 2007
4,700
1,225
Kwenye mkoba wa JK kulikuwa carrots na sticks zilizoandikwa "Made in USA". Walipoziona siyo Kibaki wala Raila aliyeweza kukataa...

Kuna jambo moja rahisi na linafahamika kwa kila mfuatiliaji mambo ya kimataifa...

Wamarekani ni wadhaifu sana kwenye mambo ya mediation!!! hivyo si kweli kwamba wamesaidia...

Lakini ni kweli kwamba viongozi wa ODM na PNU walishaambiwa na Akina Rice kwamba mkishindwa kupatana tutakutana kwenye mahakama ya Dunia - Hague kama watuhumiwa wa mauaji ya Kimbari....

Suala la Tanzania kuwa na uwezo wa kupatanisha liko wazi... hatuhitaji kusema zaidi... na mengi mutayaona kwenye kipindi cha Tanzania ikiwa mwenyekiti wa AU.

Tatizo lenu ni ubinafsi... munafikiri sifa ni za JK... ni za Tanzania
 
Mtanzania

JF-Expert Member
May 4, 2006
4,817
2,000
Kuna jambo moja rahisi na linafahamika kwa kila mfuatiliaji mambo ya kimataifa...

Wamarekani ni wadhaifu sana kwenye mambo ya mediation!!! hivyo si kweli kwamba wamesaidia...

Lakini ni kweli kwamba viongozi wa ODM na PNU walishaambiwa na Akina Rice kwamba mkishindwa kupatana tutakutana kwenye mahakama ya Dunia - Hague kama watuhumiwa wa mauaji ya Kimbari....

Suala la Tanzania kuwa na uwezo wa kupatanisha liko wazi... hatuhitaji kusema zaidi... na mengi mutayaona kwenye kipindi cha JK...

Tatizo lenu ni ubinafsi... munafikiri sifa ni za JK... ni za Tanzania

Kasheshe,

Kwenye hili USA, EU, UK na nchi zingine wamesaidia. Waliposema It won't be business as usual, maana yake ilikuwa kubwa sana.

Nakubaliana na Mwanakijiji hapa kwamba ule usemi wa stick and carrot huenda umesaidia sana.

Kazi ya akina Annan na JK ilirahisishwa kidogo na misimamo ya hao wakuu wa dunia. Kwenye jambo la Kenya kwa kweli dunia nzima imecheza inavyotakiwa.

Watanzania tuna haki ya kunyanyua vichwa vyetu juu ya hili maana JK na Mkapa
walikuwa kwenye timu iliyoleta mafanikio.
 
MzalendoHalisi

JF-Expert Member
Jun 24, 2007
4,002
2,000
Nimeangalia BBC wakimhoji Annan.. kweli anasema JK as a person na raisi wa Tz na mzoefu ktk EA politics was instrumental in reaching the deal!
 
Masanilo

Platinum Member
Oct 2, 2007
22,297
1,250
somebody shoot me! Hongera JK kwa kufanya kweli Kenya, natumaini the same procedure itafuatwa Zanzibar pia au sio (kama kweli ni wewe umefanya hili).

Jamani Koffi Annan, Ben Kiwira Mkapa, Graca Machel wamekuwa Kenya zaidi ya mwezi wakijaribu kuratibu na kupatanisha hizo pande mbili Kibaki na Raila. Tukumbuke pia Kufour, Desmond Tutu, Chissano Joachim na Condeleza Rice wote hawa kwa nyakati tofauti wamechangia kufikia hapo kwenye muafaka....sasa tunapokuwa wasahaurifu kiasi hicho na kumpa JK sifa kwangu inakuwa shida kumeza hili. Kikwete amekwenda kushuhudia matiliano ya sahihi makubaliano. Kama ni mchango ni very insignificant...msije aanza aandaa maandamano na mapokezi eti amefanikisha amani na zile nguo zetu za kijani na makapelo
 
Kenyan-Tanzanian

JF-Expert Member
Nov 7, 2006
302
0
Brazameni heshima mbele. Leo siku ya furaha na sio karaha jameni.

Wakuu,

Kwa kweli initiatives za amani hizi zimekuwa toka pembe nyingi tu. Wacha tuseme kwamba kila yakhee amechangia kwa kiasi fulani. Wakiwemo: Raila, ODM, Kibaki, PNU, EU, AU, UK, UA na pia Ujerumani kibinafsi kama nchi.

Lakini tusisahau wananchi wenyewe jameni. Ni kweli wengine waliuawa lakini ni kweli kwamba waKenya hawa wangekubali wizi wa kura kama mazuzu basi wangekuwa ndio wameiuwa demokrasia changa ya nchi yetu.Muhimu tumejifunza ni kwamba hakuna yule aliyedhania kwamba ni Mkenya zaidi kuliko yule mwengine atazidi kuwa na fikra hizo potevu. Extreme ethnic nationalism ndio imetiwa kitanzi na niko sure kwamba wengi watajisaisai na wengi tuu watageuza mafikra zao kuhusu kabila "adui".

Naomba hivi. Wacha tuseme kwamba Rainbow ina rangi nyingi ambazo huchangia kwa urembo wa Rainbow yenyewe. Muhimu sio nani alileta rangi nyingi kuliko nani. Mimi nawakilisha kwamba muhimu ni kwamba panapo Rainbow, mvua huwa inanyesha na jua pia inawaka sambamba. Leo hii Kenya tuna Rainbow of hope. Serikali ya kujumlisha wote. Bado kuna jua ya simanzi kwa walioumia na kuna mvua ya tumaini kwa wale tumekubali mkataba wa leo. Muhimu ni kwamba sasa viongozi wafanye hima na kuleta reforms za kikatiba, kiserikali na kisiasa ili yaliojiri yasijiri tena mbeleni.

Kwa maoni yangu Kibaki angetangaza leo kuwa Reconciliation Day au kwa lugha yetu "Siku Ya Amani". Iwe rasmi kila mwaka kuisherehekea na vizazi vijazo kama akina mjukuuangu Vini waelewe kwamba maisha alfu lela ulela zilizopotea na mali ya mabilioni ilikuwa ni kwajili gani.... Damu iliyomwagika isilale tuu mchangani ikilia pasiye na anayeiisikiza.

Karibuni kwa watani wenu wa jadi tunywe mbili au tatu baridi. Happy new year!
 
Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,040
2,000
Kuna jambo moja rahisi na linafahamika kwa kila mfuatiliaji mambo ya kimataifa...

Wamarekani ni wadhaifu sana kwenye mambo ya mediation!!! hivyo si kweli kwamba wamesaidia...

Lakini ni kweli kwamba viongozi wa ODM na PNU walishaambiwa na Akina Rice kwamba mkishindwa kupatana tutakutana kwenye mahakama ya Dunia - Hague kama watuhumiwa wa mauaji ya Kimbari....

Suala la Tanzania kuwa na uwezo wa kupatanisha liko wazi... hatuhitaji kusema zaidi... na mengi mutayaona kwenye kipindi cha Tanzania ikiwa mwenyekiti wa AU.

Tatizo lenu ni ubinafsi... munafikiri sifa ni za JK... ni za Tanzania

right on.. sikusema walisaidia katika mediation.. kitu kinachoitwa pressure wamarekani wanajua sana. Nguvu yao ya dola... usiidharau. Hasa mtu akipigwa mkwara kuwa vile viakaunti vyao pale NY vitakuwa frozen.. people will start dancing.
 
zomba

JF-Expert Member
Nov 27, 2007
17,071
0
Kwa hiyo kazi yote ya wiki kadhaa haikuwa na maana, kaja Superman Kikwete katika kikao cha masaa matano kaweza kufanya Annan na Mkapa walichoshindwa kufanya tangu January 10 siyo?

Woow, kwa nini asitumie magic touch yake Zanzibar basi?

Wote wanafaa kupongezwa, lakini ngoja nikukumbushe Mzee Roja Mila, alikuwa reserve mechi zake zilizompa sifa kuliko zote, watu wanacheza weeee akiingia yeye tu dakika za mwisho ananyuka bao sifa zote ni zake, lakini "ananyuka bao" ndio muhimu. Na hivyo ndio alivyofanya JK, watu wamecheza weeeeeee, kuingia yeye kanyuka bao.

Team nzima iliyofanya kazi Kenya inastahili sifa zote, pamoja na Kibaki na Raila wanapongezwa sana kufikia makubaliano na JK anapata golden shoes ya kuwa mfungaji bora.

Zanzibar ni matatizo mengine kabisa, huwezi kufananisha machungwa na ndizi ingawa yote ni matunda.
 
Masanilo

Platinum Member
Oct 2, 2007
22,297
1,250
Wote wanafaa kupongezwa, lakini ngoja nikukumbushe Mzee Roja Mila, alikuwa reserve mechi zake zilizompa sifa kuliko zote, watu wanacheza weeee akiingia yeye tu dakika za mwisho ananyuka bao sifa zote ni zake, lakini "ananyuka bao" ndio muhimu. Na hivyo ndio alivyofanya JK, watu wamecheza weeeeeee, kuingia yeye kanyuka bao.

Team nzima iliyofanya kazi Kenya inastahili sifa zote, pamoja na Kibaki na Raila wanapongezwa sana kufikia makubaliano na JK anapata golden shoes ya kuwa mfungaji bora.Zanzibar ni matatizo mengine kabisa, huwezi kufananisha machungwa na ndizi ingawa yote ni matunda.

Hapa Mkuu Dar Es Salaam nakupa tano, unakata mfananisha JK na Roger Milla? mmmmhh nakuelewa kazi kubwa iliishafanyika na wengine ameenda kufunga tu....
 
zomba

JF-Expert Member
Nov 27, 2007
17,071
0
Hapa Mkuu Dar Es Salaam nakupa tano, unakata mfananisha JK na Roger Milla? mmmmhh nakuelewa kazi kubwa iliishafanyika na wengine ameenda kufunga tu....

si kufunga tu... ni hivi:

JK, watu wamecheza weeeeeee, kuingia yeye kanyuka bao.
 
Ab-Titchaz

JF-Expert Member
Jan 30, 2008
14,695
1,195
Kwa hiyo kazi yote ya wiki kadhaa haikuwa na maana, kaja Superman Kikwete katika kikao cha masaa matano kaweza kufanya Annan na Mkapa walichoshindwa kufanya tangu January 10 siyo?

Woow, kwa nini asitumie magic touch yake Zanzibar basi?

Asante Mkuu Pundit kwa mawazo yako.
Lakini Kaka hio ishu ya Zenj itakua
kwa wakati wake we subiri tu.
 
Ab-Titchaz

JF-Expert Member
Jan 30, 2008
14,695
1,195
Li-Museven litakuwa limeumbuka hapa!

Hahahaha..unafurahisha!!! Kitila Mkumbo, heshima yako kaka,
Hapo umekinena wala hujakosea.Museveni
ameonyeshwa nani nd'o kizingiti hapa Easti-Zuu,
naye si mwengine bali Rais Jakaya Mrisho Kikwete.
Kuna swali?
 
Ab-Titchaz

JF-Expert Member
Jan 30, 2008
14,695
1,195
Haina shida, kama mkuu wa kaya yetu kachangia kuleta suluhu tunampongeza! Unaweza kukuta Anna, Condoleeza, Mkapa na wengine walkuwa wanacheza majokeri wakati Madume alikuwa kayalamba JK! Good job papaa, uje utuokoe na huku Pemba.

Kweli kabisa Green29...Jamaa walikua wanacheza mojoker tu
mpaka alipoingia master gamer mwenyew...Mkulu Jakaya Kikwete.
Museveni alikua na lake jambo jamani!!!
Sasa bado hio Pemba na Zenj!
 
Ab-Titchaz

JF-Expert Member
Jan 30, 2008
14,695
1,195
Wakuu heshima yenu mpawe,

Nami nataka nitoe senti tano hapa.
Ukweli ni kwamba katika hizi talks ilikua wazi
suluhu haitopatikana bila some kind of genuine
power sharing.Wakenya wamenyanyaswa siku kibao
lakini nchi za nje hawakujua hali halisi because
of the fake impression of being a peaceful nation.Hata hivyo alipoingia Kibaki mwaka 2002 watu waliexpect
jamaa atabadili mambo lakini wapi..hali ikawa ni ile ile.
La kuudhi zaidi ni wakati alipoiba hizi kura za '07.
Hapa nd'o sasa ikajulikana wazi what we were dealing
with will be more complex to solve.

Pamoja na wapambe wake, Kibaki showed us that he will
not succumb to reasoning aghalabu akiwa na watu kama kina
Martha Karua and the like kama advisors.Kumbuka huyu mama
nd'o alokuwa chanzo cha Annan kusimamisha the negotitations..she
insulted Annan and even threatened the gentleman in his face and
then walked out of the meeting.
Hapo ndipo Annan akajua
he is dealing with a psycho.Huyu mama ndiye aliyekua tuta
katika barabara ya kupata suluhisho la kudumu.Kwa hivyo Annan
akaamua enuff of these proxies,I want the real men behind
the scenes i.e. Kibaki na Raila.
Kisha ziara ya Joji Kichaka hapa Easti, hususan Bongo ilikua
kama onyo kwa Kibaki..."we are watching you closely".
Kumbukumbu za ulimwengu wa siasa zinatuashiria situation ya Somali,
Rwanda na Zimbabwe.

This time around the international community was not gonna let this pass ocz the whole Eastern African region would collapse. Afu pia wameekeza mihela kibao Kenya na East Africa kwa jumla and they would lose greatly in event of a collapse.Imagine zile hoteli kibao Kenya ziko pegged to the economies of Europe.Kuna watu Ulaya wameekeza hata retirement funds zao na mutual stocks in that industry.Sasa wewe niambie unadhani wangekaa kando wakinagalia mihela yao inalosti? Something had to give.

The last alternative which I believe was put on the table
after Condi Rice voiced it, ni the use of force.Hawa jamaa za PNU walikua washaonyesha ulimwengu mzima kwamba hao hawasikii bila nguvu/fujo kutumika.It was in their mind set kwamba watu
watapiga kelele na fujo za wiki mbili tatu a'fu things will go back to normal.Ole wao picha ilibadilika!In this end I want to
thank Raila and the opposition figures for standing their ground
and the support of the international community also.Hapa sasa amini usiamini things would have gone the Aristide way ama kama yule Bwana Charles Taylor wa Liberia.Kwa ufupi meli ingedock Indian Ocean,mzee akatumiwa Charter flight aondoke ama atalazimishwa,Kenya army pia wangeambiwa stand down or face the wrath of Joji Kichaka.Kwa hivyo nadhani hii picha ilimuogopesha huyu Mzee Kubaka na akaamua yaishe tu.
 
Madela Wa- Madilu

JF-Expert Member
Mar 24, 2007
3,070
1,195
Wote wanafaa kupongezwa, lakini ngoja nikukumbushe Mzee Roja Mila, alikuwa reserve mechi zake zilizompa sifa kuliko zote, watu wanacheza weeee akiingia yeye tu dakika za mwisho ananyuka bao sifa zote ni zake, lakini "ananyuka bao" ndio muhimu. Na hivyo ndio alivyofanya JK, watu wamecheza weeeeeee, kuingia yeye kanyuka bao.

Team nzima iliyofanya kazi Kenya inastahili sifa zote, pamoja na Kibaki na Raila wanapongezwa sana kufikia makubaliano na JK anapata golden shoes ya kuwa mfungaji bora.

Zanzibar ni matatizo mengine kabisa, huwezi kufananisha machungwa na ndizi ingawa yote ni matunda.

Umeeleza vizuri mwanzoni lakini hapo mwisho umejikanyaga.

Ukisema Zanzibar ni matatizo mengine kabisa hebu ainisha usemi wako.

Naomba uilezee kadamnasi hii ya JF Tofauti walau 2 au 3 kubwa za msingi kufanya issue ya Zinzibar iwe tofauti.

Nina hamu ya kusikia Ugumu au vikwazo vilivyopo Zanzibar kiasi cha kujustify Uharamia wa kumwaga damu ya Wapinzani.

Nina hamu ya kusikia hizo sababu.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom