Tanzania yakabidhi msaada wa chakula kwa Msumbiji

Habari za Zanzibar

JF-Expert Member
Joined
Dec 18, 2024
Posts
593
Reaction score
419
TANZANIA YAKABIDHI MSAADA WA CHAKULA KWA NCHI YA MSUMBIJI

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imekabidhi msaada wa tani 500 za mahindi kwa Serikali ya Jamhuri ya Msumbiji kufuatia mafuriko yaliyoikumba nchi hiyo kutokana na mvua kubwa zilizonyesha.

Msaada huo umekabidhiwa Machi 24, 2026 na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Mahmoud Thabit Kombo (Mb) kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Shehena hiyo ya mahindi iliwasili jijini Maputo na ndege ya mizigo ya Shirika la Ndege la Tanzania na kupokelewa na Ujumbe wa Serikali ya Msumbiji uliongozwa na Waziri wa Mipango na Maendeleo, Mhe. Salim Cripton Valá,

Akikabidhi msaada huo, Mhe. Kombo alielezea uhusiano wa karibu na wakindugu uliopo baina ya Tanzania na Msumbiji ulioasisiwa tokea enzi za waasisi wa mataifa hayo mawili, Baba wa Taifa, Hayati Mwl. Juliaus Kambarage Nyerere na Hayati Edward Mondlane. Waziri Kombo alisema kufuatia udugu huo, Rais Dkt. Samia amemtuma kufikisha msaada huo ili uweze kuwapunguzia adha waathirika wa mafuriko hayo.

"Kwa niaba ya Serikali ya Tanzania, Rais Samia anatoa salamu za pole kwa Rais wa Msumbiji, Mhe. Daniel Chapo na watu wa Msumbiji kwa ujumla kutokana na madhila yaliyosababishwa na mafuriko haya na ameahidi kuwa Tanzania ipo tayari kundelea kutoa msaada kwa Msumbiji katika nyakati zote", Waziri Kombo alisema.

Wakati wa ziara hiyo, Mhe. Kombo alipata nafasi ya kukutana na kuzungumza na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Msumbiji Mhe. Maria Belvinda Levy kuhusu kuendeleza na kuimarisha uhusiano na ushirikiano baina ya nchi hizi mbili, hususani kwenye masuala ya kiuchumi.

Serikali ya Msumbiji imetoa shukrani za dhati kwa kupokea msaada huo kutoka kwa ndugu zao Watanzania ambao unabainisha taswira ya ukaribu na ushirikiano wa kweli uliopo baina ya nchi mbili hizi.

IMG-20260325-WA0005.jpg
IMG-20260325-WA0019.jpg
IMG-20260325-WA0004.jpg
IMG-20260325-WA0050.jpg
IMG-20260325-WA0052.jpg
IMG-20260325-WA0038.jpg
 
View attachment 3562354View attachment 3562361View attachment 3562370View attachment 3562377View attachment 3562379View attachment 3562386
Tanzania tuna Ndege ya mizigo yenye uwezo wa kubeba Tani 500?
 
Tanzania hatuna Ndege ya mizigo yenye uwezo wa kubeba hata tani 100. Wewe mleta mada Tani 500 unafiri mchezo?
Au ulimaanisha Tani 50?
Upo sahihi. Ndege ya kwanza ya Tanzania ya mizigo Boeing 767-300 ina uwezo wa kubeba tani 54 kwa mara moja. Hata ile ndege kubwa ya Mizo ya Ukraine iliyolipuliwa na Urusi Antonov An-225, ambayo ndo ilikuwa ndege kubwa ya mizigo duniani, iilikuwa na uwezo wa kubeba tanii 250 tu.
20260325_084312.jpg
20260325_084302.jpg
bucharest-romania-october-07-2021-600nw-2468918053.jpg
Antonov-AN-225-Mriya.jpg
32904_FB17359EE650B783-2 (1).jpg
 
Sheikh Kombo pia ametumia wasaa huo airport kutuma salama za chama dola kongwe kwa chama dada FRELIMO katika hotuba ya makabidhiano ya mzigo wa kwanza wa msaada mahindi kwa Mozambique

24 March 2026
Maputo, Moçambique

TANZÂNIA ENTREGA AJUDA ALIMENTAR A MOÇAMBIQUE

View: https://m.youtube.com/watch?v=vqnHo5TenBs
O Governo da República Unida da Tanzânia entregou 500 toneladas de milho ao Governo da República de Moçambique, em resposta às inundações que atingiram o país devido às fortes chuvas.

A ajuda foi entregue em 24 de março de 2026 pelo Ministro das Relações Exteriores e da Cooperação da África Oriental, Mahmoud Thabit Kombo , em nome da Presidente da República Unida da Tanzânia, Dra. Samia Suluhu Hassan.

O carregamento de milho chegou a Maputo em um avião de carga da Tanzania Airlines e foi recebido por uma delegação do Governo moçambicano liderada pelo Ministro do Planejamento e Desenvolvimento, Salim Cripton Valá.

Ao entregar a ajuda, o Ministro Kombo descreveu as relações estreitas e fraternas que existem entre a Tanzânia e Moçambique, estabelecidas desde os tempos dos fundadores das duas nações, o Pai da Nação, o falecido Mwl. Juliaus Kambarage Nyerere, e o falecido Edward Mondlane. O Ministro Kombo afirmou que, em virtude dos laços de fraternidade, o Presidente Dr. Samia o enviou para entregar a ajuda humanitária, visando aliviar o sofrimento das vítimas das inundações.

"Em nome do Governo da Tanzânia, o Presidente Samia expressa suas condolências ao Presidente de Moçambique, Daniel Chapo, e ao povo moçambicano em geral, pelas dificuldades causadas por essas inundações, e prometeu que a Tanzânia está pronta para continuar prestando assistência a Moçambique em todos os momentos", declarou o Ministro Kombo.
1774735526274.jpeg

Durante a visita, o Ministro Kombo teve a oportunidade de se reunir e conversar com a Primeira-Ministra da República de Moçambique, Maria Belvinda Levy, sobre o desenvolvimento e o fortalecimento das relações e da cooperação entre os dois países, especialmente em questões econômicas.

O Governo de Moçambique expressou sua sincera gratidão pela ajuda recebida de seus irmãos tanzanianos, o que evidencia a proximidade e a verdadeira cooperação que existe entre os dois países
 
Tanzania hatuna Ndege ya mizigo yenye uwezo wa kubeba hata tani 100. Wewe mleta mada Tani 500 unafiri mchezo?
Au ulimaanisha Tani 50?

Upo sahihi. Ndege ya kwanza ya Tanzania ya mizigo Boeing 767-300 ina uwezo wa kubeba tani 54 kwa mara moja. Hata ile ndege kubwa ya Mizo ya Ukraine iliyolipuliwa na Urusi Antonov An-225, ambayo ndo ilikuwa ndege kubwa ya mizigo duniani, iilikuwa na uwezo wa kubeba tanii 250 tu.
Kwani nyinyi mliishia darasa la ngapi?
 
Shehena hiyo ya mahindi iliwasili jijini Maputo na ndege ya mizigo ya Shirika la Ndege la Tanzania na kupokelewa na Ujumbe wa Serikali ya Msumbiji uliongozwa na Waziri wa Mipango na Maendeleo, Mhe. Salim Cripton Valá,

Kwani nyinyi mliishia darasa la ngapi?
Ulivyo uliza swali watu watahisi wewe msomi.. Kabla ya kuuliza swali umesoma Thread?
 
Umeandika chuki zisizo na msingi.
Neno limetumika Tanzania, Tanzania ni muungano wa Tanganyika na Zanzibar, mahindi yamelimwa Tanganyika, pesa zilizotumika ni za Tanganyika kwani Zanzibar haichangii chochote. Nieleze chuki iko wapi wakati mtu w Zanzibar anagawa rasilimali zinazotoka Tanganyika labda kama wewe ni mnufaika.
 
Back
Top Bottom