Tanzania vs China na maendeleo yake

ONJO

JF-Expert Member
Jun 1, 2022
215
261
Habari zenu..

Leo tujifunze kutoka kwa wachina.

Tangu 1950s nchi ya Tanzania na china kimaendeleo zilikuwa sawa.

Tangu hapo walijitokeza wanafalsafa wakiishauri china wakisema ''taifa ili liweze kuendelea lazima liwe na watu''.Nchi ya china ilianza kutekeleza sera hiyo kwa kuhamasisha watu wazaliane,ikiwa na lengo kwamba ikipata watu basi itajipatia nguvu kazi ambayo itatekeleza sera za maendeleo ya china ikiwemo shughuli za kilimo na viwandani.

Tangu Tanzania inapata uhuru mwaka 1961,watu wa china walikuwa wengi,na sera zote za kimaendeleo zilikuwa zikitekelezwa ndipo utofauti ukaanza kuonekana.China ikakua kwa kasi na tanzania ikawa inakuwa kidogokidogo mpaka ilivyo leo.

Kwa sera ya china kuhamasisha watu wazaliane simanishi kwamba na tanzania iige sera hiyo bali kupitia hiyo ijifunze kuwa taifa ni watu.

Tujionee wenyewe..

Akili+afya=mtu kamili mwenye nguvu ya kulitumikia taifa.

ELIMU BURE
Serikali ilifanya jambo la busara kuanzisha sera ya elimu bure kuanzia sekondari mpaka advance ikiwa na lengo la kuondoa ujinga(akili).Bigup.Na taifa letu laitaji wasomi ili lipige hatua kiMaendeleo.

AFYA BURE
Kama sera ya china ya kuhamasisha watu wazaliane kwa wingi najua sisi watanzania tupo wengi zaidi ya mil 60.Na bado wanazaliana cha kufanya ni kujikita katika kuimarisha afya za watu.
@Serikari inahamasisha kila mtu awe na bima kwa ajili ya kupunguza gharam za matibabu kwa kulipia 30000/= Kila mwaka
hata hivyo wananchi wa vijijini hawajaweza kuafford kwa umasikini wao,wengi wao wanakufa kwa kukosa huduma hata zile za kulipia mojamoja hawawezi kwa sababu ya ugumu wa maisha.
@Ningependa kuishauri serikali kama vile ilivyoweza kutekeleza elimu bure.Ifanye pia kwenye sekta ya afya.Kila Mtu awe anatibiwa bure kwa kufanya hivyo tutaimarisha nguvu kazi ya taifa ambayo ni watu.

MAJI BURE
maji yana umhimu mkubwa kwa wananchi,kwani yanahitajika kwa kila kitu majumbani pamoja na shughuri zote hasa za maendeleo.
@naishauri serikali mradi wa maji uhusike na kumpelekea mwananchi moja kwa moja nyumbani kwake bila gharama yoyote.Isipokuwa mwananchi atakuwa anakatwa gharama za maji kadiri anavyotumia (bill) na hii itaondoa changamoto za maji hasa maeneo ya vijijini.

UMEME BURE
mradi wa umeme nao ujikite kumpelekea mwananchi umeme bure hasa maeneo ya vijijini.Hata hivyo gharama ya mwananchi kuhusu matumizi ya umeme yakatwe kwenye kulipia units, na hii itasaidia kwa maeneo ya vijijini kuipata huduma ya umeme kwa urahisi.
PESA ZITATOKA WAPI

Kama serikali itakuwa na uthubutu wa kutekeleza miradi hiyo inaweza ikakopa kama inavyofanya kwenye miradi mingine kwani najua inaweza gharimu hata zaid ya trilion 500.Ni gharama kutekeleza lakini faida yake ni ya milele vizazi hata vizazi.Hapa mnaweza mkaona kumbe development is the gradual process.

Angalizo
kukopa sio dhambi kwaajili ya kutekeleza productive sectors.

See you NA ONJO.
 
Back
Top Bottom