Yoda
JF-Expert Member
- Jul 22, 2018
- 37,620
- 46,260
Kama raia, tanapoyatamini na kuyatafuta maendeleo lazima kuna ukweli tunahitaji kuufahamu vizuri.
Mojawapo ni hili la kwamba demokrasia haileti maendeleo, pia udikteta hauleti maendeleo. Maendeleo ni huru(independent) ya aina zote hizo mbili za utawala. Ndio maana unaweza kuona kuna nchi za kidikteta kama China na Urusi zimeendelea na pia kuna nchi za kidemokrasia/kiliberali kama Marekani, Australia na Canada zimeendelea pia.
Maendeleo yanahitaji kufuata kanuni za msingi wake ikiwemo uwajibikaji wa viongozi, utabirikaji wa sera na maamuzi ya nchi, utulivu wa kisiasa, umoja ndani ya nchi, meritocracy, elimu bora, kuwa karibu na waliondelea, utamaduni n.k. Kimsingi haya ni mambo yanaweza kupatikana katika udikteta(benevolent dictatorship) au demokrasia.
Kitu cha ziada demokrasia inacholeta katika taifa ni kuyafanya maendeleo kuwa endelevu, jumuishi zaidi na kuhakisha utangamano katika taifa unadumishwa hasa kwa yale mataifa yenye jamii nyingi tofauti mfano za makabila, lugha, dini.