China na Afrika zinajitahidi kutafuta njia zao za maendeleo

ldleo

JF-Expert Member
Jan 9, 2010
1,010
1,036
VCG111463369622.jpg
Tarehe 18 Desemba ni siku ya maadhimisho ya miaka 45 tangu sera ya mageuzi na ufunguaji mlango ianze kutekelezwa nchini China. Katika kipindi hicho, China sio tu imefanikiwa kujiinua kiuchumi, na mafanikio yake kuwa dhahiri kwa wote, bali pia imetoa usaidizi mkubwa kwa maendeleo ya Afrika na wazo muhimu - ni sahihi kuchunguza kwa uthabiti njia ya kisasa ambayo inafaa hali halisi ya nchi yenyewe, jambo ambalo linaweza kufanikiwa.

Mwaka 1978, katika kipindi cha mwanzo cha kutekeleza sera ya mageuzi na ufunguaji mlango, China ilikuwa moja ya nchi maskini zaidi duniani. Kwa mujibu wa viwango vya Benki ya Dunia, Pato la Taifa la China kwa mtu mmoja mmoja lilikuwa ni chini ya dola za Kimarekani 160, lakini Pato la Taifa la nchi za Afrika zilizo Kusini mwa Sahara lilikuwa dola za kimarekani 490. China haikufikia hata theluthi moja ya wastani wa nchi za Afrika.

Miaka 45 baadaye, China sio tu imekuwa nchi ya pili kwa uchumi mkubwa duniani, lakini mchango wake katika maendeleo ya uchumi wa dunia pia umedumu kwa zaidi ya asilimia 30 kwa miaka mingi. Mafanikio ya miaka 45 ya mageuzi na ufunguaji mlango ya China yanathibitisha kwamba umaskini si hatima ya watu wa China, na pia kila nchi inaweza kuondokana na umaskini na kupata ustawi. Kama China imeweza kufanikiwa, na hata nchi za Afrika pia zinaweza kufanikiwa.

Vilevile, miaka hii 45 pia imeshuhudia jinsi China na nchi za Afrika zinavyosonga mbele bega kwa bega. Katika mazingira ya utandawazi wa dunia, uhusiano kati ya China na Afrika umebadilika kutoka China kutoa msaada wa upande mmoja kwa Afrika hadi kuwa ushirikiano wa kunufaishana kwa pande zote. Hasa katika sekta ya uchumi na biashara, China na Afrika zimepata maendeleo makubwa, ambapo kiwango cha biashara baina ya pande hizo mbili kimeongezeka kutoka dola za kimarekani milioni 765 mwaka 1978 hadi dola bilioni 282 mwaka 2022, ikiwa ni ongezeko la zaidi ya mara 300.

Wazo la "eneo maalum la kiuchumi" pia limeonekana hatua kwa hatua katika sehemu nyingi za Afrika - wamejifunza kutokana na uzoefu wa China katika nyanja nyingi kama vile vifaa vya huduma vya ndani, uendeshaji na usimamizi. Juu ya hili, gazeti la "Financial Times" la Uingereza lilisema kwa uwazi kwamba jambo muhimu katika mafanikio ya sekta ya uzalishaji viwandani ya nchi za Afrika ni kufuata "mfano wa China."

Mwaka 2013, ili kuimarisha mageuzi na ufunguaji mlango, China ilipendekeza ujenzi wa pamoja wa "Ukanda Mmoja, Njia Moja" BRI, ambao ulipata mwitikio mkubwa kutoka nchi za Afrika. Kama mahali muhimu pa utekelezaji wa Pendekezo hilo kati ya China na Afrika, Kenya ni mnufaika mkubwa. Wiki hii, China na Kenya kwa pamoja zimeadhimisha miaka 60 tangu kuanzishwa kwa uhusiano wa kibalozi kati ya nchi hizo mbili.

Huenda baadhi ya watu hawajui kwamba katika kipindi cha miaka 10 iliyopita, China imefanya kongamano la ushirikiano wa kimataifa kuhusu BRI mara tatu, ambapo serikali mbili za Kenya zimeshudhuiwa zikibadilisha uongozi wake. Hata hivyo, Rais wa zamani Uhuru Kenyatta na Rais wa sasa William Ruto wote walikuja wenyewe kuhudhuria hapa mjini Beijing. Hii inaonyesha uungaji mkono na utambuzi kamili wa Kenya juu ya Pendekezo hilo, kwa sababu limeleta manufaa dhahiri kwa maendeleo ya taifa la Kenya na uboreshaji wa maisha ya watu.

Hatma zinazofanana zinazipa China na Afrika hisia ya kuwa karibu moja kwa moja, na pia kufanya uzoefu wa maendeleo ya China kuwa wenye maana maalum kwa Afrika. Nchi za Afrika za leo zina rasilimali nyingi za watu na manufaa mengine, ambayo ni sawa na hali ya taifa la China baada ya mageuzi na ufunguaji mlango.

Hata hivyo, ikilinganishwa na China ya wakati huo, ni wazi vijana wa Afrika wa sasa wameelimika zaidi na wameunganishwa zaidi na dunia, wamejaaliwa mawazo mengi, uhai na ubunifu na kutengeneza mustakabali wao na wa nchi zao. Tunatumai kuwa nchi za Afrika pia zitaweza kukomboa nguvu za uzalishaji na kuunda miujiza ya maendeleo kupitia mageuzi na ufunguaji mlango. Katika mchakato huu, China na Afrika zinaweza kuaminiana kabisa na kuelekea kwenye njia zao za kisasa kwa pamoja.
 
Back
Top Bottom