Kwa mfano huu wa Daktari nafikiri hiyo ni zawadi au shukrani kwani walitoa baada au alimjengea baada na hakukuwa na mzingira yeyote ya kuomba kabla ya huduma na wala kurudi tena kuomba msaada baada ya kutoa au kujenga.Lakini ni viongozi wangapi ambao hupewa ufadhili na wafanyabiashara au baadhi ya watu ukifichwa kama ushabiki na mapenzi? Madaktari wangapi hupewa "asante" na baadhi ya wagonjwa matajiri baada ya kunusuru maisha yao au ya wale wawapendao? Nakumbuka daktari mmoja ambaye alijengewa nyumba na mhandisi mmoja wa Kimarekani kule Mbeya baada ya daktari huyo kuokoa maisha ya mke wa mhandisi! Sasa sijui kama ile ilikuwa rushwa au asante tu!!
Hapa itategemea na msimamo wa huyo Daktari na lengo la huyo aliyejenga hiyo nyumba na kama alijenga kwa kushukuru hawezi kurudi na kutotaka kupanga foleni na kama Daktari hana tabia ya kupindisha sheria first come first to be saved then ataendelea na majukumu bila ya matatizo na kama kuna ambaye atahudumiwa bila ya kufuata utaratibu wowote ni yule wa emergency na hapa kama Daktari anajua kazi yake na muungwana atawaomba radhi wagonjwa waliotangulia kwa kuwafahamisha umuhimu wa kumuona huyu ambaye maisha yake yapo hatarini zaidi na wagonjwa wanakubali wanapoelezwa hali halisi na kuiona.Hapatakuwa na muingiliano wowote kwani wote walifanya kwa nia njema.Aliyetoa alitoa kwa nia njema na aliyepokea alipokea kwa njia njema.Kabla ya kutoa hakuombwa na kabla ya kupokea hakuomba.Rejea yule Waziri wako aliyepita kwenye yale maduka ya kina Bushiri et al.KNKCU, ila unafikiri huyo Mhandisi leo akipatwa na kaugonjwa na akaenda hospitalini kweli atasubiri kwenye foleni? au huo msaada wake umemnunulia ufunguo wa ofisi ya daktari wetu? Kama amemsaidia kumjengea nyumba Daktari huoni kuwa huyo Mhandisi anastahili angalau kidogo kupata kaujiko akifika ofisini kwa daktari ukilinganisha na sisi wengine ambao hata kufagia nyumba ya daktari hatujafagia?
Kabla hatujaenda mbali naomba nikuulize nini uelewa wako kuhusu neno Rushwa?kwa hiyo kama mtu hakuomba au kuonesha kuomba akapewa basi inawezekana isiwe rushwa...!!
MAELEZO YAKO HAPO ONGEZA NA HAKUJENGA MAZINGIRA AU MIANYA YAKUMFANYA MTU AMPE CHOCHOTE AU AMFANYIE CHOCHOTE KWA MINAJILI YA KUPEWA HUDUMA AMBAYO KWA MUJIBU WATARATIBU AU SHERIA ALITAKIWA AMHUDUMIE KAMA MOJA YA KUTIMIZA WAJIBU WAKE KIKAZI.kwa hiyo kama mtu hakuomba au kuonesha kuomba akapewa basi inawezekana isiwe rushwa...!!
Watayarishaji wa hayo matangazo ni nani? waombwe watayarishe na matangazo yanayohusu Rushwa kubwa kubwa kama za mikataba inayofanywa na viongozi na wahisani ,Bila ya kusahau viongozi na wawekezaji tena itolewe kwa Lugha zote mbili kiswahili na kiingerza ili jamii ifadike na ujumbe uwafikie na wahusika wasio wazawa.Kwa kweli nakerwa sana na matangazo yanayorushwa na television ya taifa ya kupiga vita rushwa ambayo yameandaliwa na Taasisi ya Kupiga Vita Rushwa Tanzania. Hapo unaoneshwa traffic akisimamisha daladala halafu anapewa rushwa ya shs 5,000/= analiachilia. Au unaonyeshwa hakimu akimwachia mtuhumiwa baada ya kupewa rushwa ya kama shs 30,000 (kama niliziona vyema kwenye TVT) Vile vile, kuna nesi analazimisha rushwa itolewe ili mgonjwa apigwe X-Ray.
Kweli, hizi rushwa ndizo zinaonekana mbovu sana katika taifa na za kukemewa mpaka kwenye runinga? Mbona hamtuonyeshi mfano wa kigogo mmoja akiingia mkataba wa kuleta/kununua umeme Tanzania? Au wa kununua rada? Au kujenga twin towers za benki kuu? Hizi ni rushwa ambazo kila mtanzania, (pamoja na wewe unayetarisha matangazo hayo) ameathirika. Bei ya umeme imepanda, na kuna tetesi tena kuwa itapanda mwezi wa sita. Priorities zetu za kupiga rushwa ziko wapi? Mmewapigia kelele weee Hakielimu kuwa wanatoa matangazo ya kudhalilisha taaluma za wafanyakazi wa serikali, nanyi mmeanza kufanya hayo hayo. Lakini naamini kuwa mmeanza kufanya hivyo ili ku-divert attention ya wananchi kwenye hizo rushwa kubwa kubwa ambazo zinafanywa na viongozi wa serikali.
Haya, endeleeeni. Labda ndio the best approach. Mimi nayaunga mkono mawazo ya Doc. Mwakyembe wakati wa kujadili mswada wa kupiga vita rushwa.