Tanzania Tycoons List...

Wakuu Jmushi1 na Kakalende;

Chanzo cha orodho hiyo ya matajiri ni kutoka hapa hapa JF na katika mpangilio wake haimaanishi kuwa walio juu ndiyo matajiri zaidi. Bado hatujafikia stage hiyo mpaka tupate details za kutosha.
 
Sumaye,Diallo,Mramba
Kuna mhindi mmoja arusha anamiliki maduka ya BENSON
 
Tumtafute Mtanzania maskini kuliko wote tumchangie elfu mmoja mmoja, angalau tumnunulie jembe na mbegu aweze kujiondoa kwenye umaskini huwo maisha... vile vile ingekua sio mbaya tukampatia elfu tano kila mwezi hadi hapo atakapo weza kujitegemea...

Wako wengi mno wengine sio maskini but wakisikia hilo dili kila mtu atachangamkia
 
kutoa list ya majina ya watu na kusema kuwa ni matajiri wakubwa wa tanzania bila ya kuwa na takwimu halisi za utajiri wao sio sahihi kabisa.nadhani kingeanzishwa chombo au taaasisi ya kutoa orodha ya watu matajiri sana na kiasi cha utajiri wao kama inavyofanya jarida la FORBES.mimi binafsi kuna watu ambao nawasikia kuwa ni watu wenye ukwasi wa hali ya juu hapa kwetu lakini hawafahamiki kwa watu.
 
Mbona Lowassa sijaona jina lake popote pale? Kati ya Lowassa na Chenge nani ana vijisenti zaidi?
 
Mimi binafsi sioni kama mabinlioni ya Kikwete yanalenga kuondoa umasikini.

Kwa kweli ikiangalia kwa undani utagundua kuwa zile hela zilitolewa kupunguza kelele baada ya sderikali kukosa namna ya kudanganya zaidi kuhusu ajira milioni moja za JK na mengine mengi aliyoahidi.

Nataka niwahakikishie wanajukwaa kuwa mabilioni ya JK hayajaaminishwa kurudishwa hata kidogo bali yanafanya kazi ya kisiasa ya kupunguza lawama kwa serikali ya CCM.
Wafanye nini zaidi ya hilo? Imebaki kudanganya tu!!
 
Pundamilia!!!
Naona wazi kuwa hujamwelewa Ndesamburo na pia una jukumu la kumpinga.
Please read between the lines to see reality
 
Pundamilia!!!
Naona wazi kuwa hujamwelewa Ndesamburo na pia una jukumu la kumpinga.
Please read between the lines to see reality

Mkuu Kamende,
Ahsante kwa comment yako, lakini hujaniambia wewe umemuelewa nini huyu Mh Mbunge. Nitafurahi kama utanieleza jinsi ulivyomuelewa huku ukifanya marejeo halisi ya hizo comments zangu hapo juu.

Unaposema kuwa nina jukumu la kumpinga nadhani hauko sahihi kwani hapa kwenye hii forum tunakutana watu tofauti na kujadiliana kwa mapana na marefu, kushindanisha hoja na wala siyo baraza la kufikirika. Ndesamburo siyo malaika ni binadamu kama binadamu wengine. Sasa hivi tunajadili yale yaliyotoka kinywani mwake.
 
Kuna tajiri mmoja anaitwa KINANDA anamiliki magari mabasi mengi sana ametoka sehemu moja na Dewji na nahisi yeye ndo alimpa Dewji mtaji.Yuko Singida
 
Mbona Lowassa sijaona jina lake popote pale? Kati ya Lowassa na Chenge nani ana vijisenti zaidi?


Angalia vizuri utaona jina la Lowassa namba 12,chini ya Nazir Karamagi.

Vipi kuhusu wale wanaomiliki migodi kule Arusha.
 
Na hayo makampuni ya nje yenye kuhodhi mali zetu utajiri wao uko counted upande upi?
Kwa mfao kama kuna kampuni ina asilimia zaidi ya 60 ama 70 kwenye resources zetu kama vile gold nk....Hiyo asilia ya mapato yao ya faida inaangukia wapi?
Je ni vigezo gani hapa vinavyotumika kusema huyu ni tajiri kuliko huyu?
Ni muhimu sana kama tukiwa na matajiri wakubwa Tanzania ambao pia ni wazalendo la sivyo weusi mtakoma kuringa!
 
Mbowe ni HIPC (Highly Indebted Political Chairman kwa mujibu wa maelezo yaliyowawi kutolewa hapahapa jamvini...so muondoe mara moja,,,ana madeni kibao na ndio maana anatumia ruzuku ya chama angalau kurudishia baadhi ya madeni
 
Umemsahau David Mosha Wa Inter Consult ni mwanzilishi wa akiba bank pamoja na mashamba kadhaa huko moshi na tanga , msimamizi wa kilimanjaro international air port pamoja na kileo
 
Siri ya tajiri anaijua mwenyewe.Binafsi sina la kujifunza kutoka kwao.Wengi ni utata mtupu!Ni utata mtupu hata kwa matajiri wakubwa wa dunia.Data tunazo.
 
Tumtafute Mtanzania maskini kuliko wote tumchangie elfu mmoja mmoja, angalau tumnunulie jembe na mbegu aweze kujiondoa kwenye umaskini huwo maisha... vile vile ingekua sio mbaya tukampatia elfu tano kila mwezi hadi hapo atakapo weza kujitegemea...

CottonEyeJoe,
Ni wazo zuri sana, lakini ujue kwa kufanya hivyo tutachangia karibu 1/3 ya Watanzania wote.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom