Tanzania Tycoons List...

Matajiri wa Tanzania wezi - Ndesamburo

na Ratifa Baranyikwa, Dodoma
Tanzania Daima~Sauti ya Watu

MBUNGE wa Moshi Vijijini. Philemon Ndesamburo (CHADEMA) ameliambia Bunge kuwa matajiri wa Tanzania ni wezi hasa kutokana na mambo ya kifisadi yalivyofumka bungeni katika siku za hivi karibuni.

Ndesamburo aliyasema hayo jana alipokuwa akichangia bajeti ya Wizara ya Viwanda, Biashara na Masoko kwa mwaka wa fedha wa 2008/09.

Akizungumzia sekta ya viwanda ilivyoshindwa kuendelea hasa kutokana na ufisadi na uendeshaji mbovu wa serikali, Ndesamburo alisema: "Matajiri wa Tanzania ni wezi tumeona mambo yaliyofumka hapa bungeni"

Alisema Tanzania imeshindwa kuendelea kwa sababu ya kutofuata taratibu za kibiashara.

Alimshangaa Rais Jakaya Kikwete kutoa mikopo maarufu kama ya mabilioni ya JK kwa ajili ya kuwasaidia Watanzania na kuonya kuwa hali hiyo ni hatari na itawalemaza wananchi.

"Tunapochukua fedha tunasambaza kwenye Saccos na kwa machinga hii nchi tunaiharibu fedha za JK hazitarudi, yeye anasema zitarudi namshangaa Tanzania yenyewe ina madeni na serikali haina tabia ya kurudisha madeni. Je, kwa mtu mmoja mmoja itarudi? Wanasema ni zawadi za uchaguzi.

"Hii tabia ya kugawa fedha kama karanga inadumaza watu, inalemaza badala ya kufanya uchumi ukue unalemaa…fedha ipo tunakosa Management, ni nini tunafikia huko tunakuwa taifa la kuomba omba. Kisaikolojia ukifikiri wewe ni maskini utakufa maskini," alisema.

Katika hilo, alisema kuna haja ya Tanzania kutafuta namna ya kuwatajirisha matajiri wachache, ili waweze kuendeleza wengine kuliko kutoa mikopo kwa kila mtu.

Aidha, alisema njia pekee ya kuondokana na utaratibu mbovu wa kutozingatia taratibu wa kibiashara ni kuwa na utaratibu wa kutumia mtaji wa kuanzia biashara.

"Unapokuwa kwenye venture capital itakudhibiti ukikopa fedha kwa ajili ya kujenga shule utajenga shule kuliko ilivyo hivi sasa, unakopa fedha kwa ajili ya kujenga shule zikija unajenga kiwanda na ndiyo kitu kinachotushinda katika kuleta maendeleo na hili jambo tukianza kila mkoa tutaendelea," alisema.

Akizungumzia viwanda ambavyo vimekufa katika jimbo lake la Moshi, Ndesamburo alisema kama serikali imeshindwa kuendeleza viwanda katika jimbo hilo wampe, ili aweze kuvifufua na hatimaye wakazi wa Moshi waweze kufaidika.

"Niliwaambia bungeni kama serikali imeshindwa kufufua viwanda wanipe nifufue….narudia tena serikali nipeni viwanda Moshi nifufue niviendeleze nitafute wawekezaji, vurugu zitakuwa hakuna kama tunataka viwanda viendelee, serikali ifikiri upya kuwasaidia Watanzania, " alisema.

Aidha, mbunge huyo amelalamikia njia ya reli inayopita Moshi kufungwa na kuhoji sababu ya kutoiendeleza njia hiyo.

"Njia ya reli ya Moshi imefungwa na ni sehemu kubwa ya uchumi wa nchi yetu, ingekuwa inafanya kazi Burundi wangeitumia na nchi nyingine katika kusafirisha mizigo kutoka katika Bandari ya Mombasa hivi tumepungukiwa akili au maarifa? Mi nafikiri tumepungukiwa kiitikadi," alisema.
 
Katika baadhi ya nchi, utajiri wa mtu si wa kificho na huwa kuna listing zinazoonyesha matajiri mbalimbali na kiasi cha mali walizonazo. Yeyote ambaye ana facts za nani anaweza kuwa tajiri wa kwanza Tanzania anaweza akamwaga facts hizo hapa na chanzo cha utajiri wake.

Ni kweli ingawa sijasoma yote yaliyochangiwa kwa wenzetu sio kificho kwa sababu utajiri unatokana na kiasi ambacho unalipa kodi. Yaani inajulikana kwa mwaka umeingiza kiasi gani na umelipa kodi kiasi gani.

Matajiri wetu hiyo ya kuonyesha wamelipa kodi kiasi gani ni kichekesho. Tuanze kubadilika na kila Mwananchi ajulikane amelipa kodi kiasi gani kama anafanya kazi au biashara na hiyo ndio siri kubwa ya wenzetu kupiga hatua. Hivi sasa wanaolipa kodi kwa haki ni wafanyakazi ambao wanakatwa moja kwa moja kutoka kwenye mishahara yao na kuna baadhi wanakatwa na hiyo pesa hata hazina haifiki.
 
Khoryere, nadhani sasa tumefikia pazuri, kama kunauwezekano wa kupata listi ya walipa kodi wakubwa TRA then kodi wanayolipa bila ya shaka itakuwa proportional na mapato yao.

Lakini hata kama kuna makampuni yanayomilikiwa na watu ambao wana hisa kubwa bado kiasi cha kodi ambacho kampuni hiyo inalipa kinaweza kikatupatia picha halisi.

Je kuna reference yoyote ya large tax payers inaweza kupatikana?

Mkuu sasa hao TRA wanakua wanazi kodi haipo fair kwa every one Ukweli ni kwamba matajiri ambao wanajulikana ni wa upinzani kodi yao ni kubwa kuliko wale wa CCM. na pengine hawalipi kabisa wanaleta ulalamishi
Lakini wa upinzani hakuna mzaa
Yaani hawana kipimo maalum ukiearn million 10 kodi yako hii lakini wao wanawekaujanja ujanja tuu
 
"Tunapochukua fedha tunasambaza kwenye Saccos na kwa machinga hii nchi tunaiharibu fedha za JK hazitarudi, yeye anasema zitarudi namshangaa Tanzania yenyewe ina madeni na serikali haina tabia ya kurudisha madeni. Je, kwa mtu mmoja mmoja itarudi?

I dont agree with this statment, evidence shows at all levels kwamba the low income population have a lower default rate then Higher income individualds and tend to respect sheria zaidi because they know its all they can do kwenye Tanzania yetu ya "wananchi" na "wenyenchi".
 
“Tunapochukua fedha tunasambaza kwenye Saccos na kwa machinga hii nchi tunaiharibu fedha za JK hazitarudi, yeye anasema zitarudi namshangaa Tanzania yenyewe ina madeni na serikali haina tabia ya kurudisha madeni. Je, kwa mtu mmoja mmoja itarudi?

I dont agree with this statment, evidence shows at all levels kwamba the low income population have a lower default rate then Higher income individualds and tend to respect sheria zaidi because they know its all they can do kwenye Tanzania yetu ya "wananchi" na "wenyenchi".

But still that does not mean that they will pay back. Money is money, regardless of the sheria.
 
But still that does not mean that they will pay back. Money is money, regardless of the sheria.

I agree with u, my point is that there those above the law and there those who have to abide by the law in TZ, the have nots who these saccos are targeting are for people who are not immune to prosecution or exclusion. This makes them more wary to repay back money as opposed to the likes of Mustafa Mkullo our Minister of Finance or Freeman Mbowe for that sake...
 
Peter Noni wa Planatel Ali Mfuruki wa InfoTech, Ami Mpungwe...George ali wa tanconsult....or are all these small fish in a big pond...
 
Muulizeni Mzee Ndesa ajira kwenye kampuni zake zimekaaje zaidi ya ndugu, jamaa na kabila yake? Nenda pale Keys Hotel hapa Dar, utadhani uko KIBORLONI! Halafu anakataa Wamachinga wasipewe hela. Matajiri WAZAWA hawafai, bado wana safari ndefu ya kujifunza.
 
Mkuu ninakuheshimu sana ila you can't make a list of rich people out of speculations.May I know under what criteria you listed the above as richest Tanzanians?
Thread yako inauliza jee hii ndiyo list ya matajiri wa Tanzania then hapo hapo umeshajibu na kusema kuwa listi ya Matajiri Tanzania ni hii iliyopo hapa chini.
 
Uchambuzi wa: https://www.jamiiforums.com/showthread.php?p=265428#post265428 (Unaweza kuongeza majina unayoyajua katika thread hii) unaonyesha kuwa listi ya Matajiri Tanzania ni hii iliyopo hapa chini.

Ingawa hakuna takwimu juu ya utajiri walionao na kiasi gani cha pesa walichonacho, swali la msingi ni: Je tunajifunza nini kutokana na jitihada zao za biashara au kupata utajiri? Je, inawezekana Watanzania wengine wakafanya jitihada na kufanikiwa kama wao?

The List

  1. Said Salim Bakhressa: AZAM - Grain milling, corporate finance, passenger sea transportation, plastic packaging, marketing, polypropylene bags, other branches of engineering field, food industry, drinking water

  2. Aziz Abood: Abood buses,factories,truck company,tv&radio,properties)
  3. Nasoro: Doll trailers, superstar buses, royal buses, major shareholder-mtibwa sugar,kagera sugar, city water, truck company, properties
  4. Mohamed Dewji: Mohamed enterprises, factories, properties
  5. Rostam Aziz: Caspian; Vodacom
  6. Reginald Mengi: The IPP Group, Financial Consulting firm (IPP Consulting), Coca-Cola (Coca-Cola Kwanza, Bonite Bottlers and Kilimanjaro Spring Water), (IPP Bodycare Ltd (IPP Media). These include The Guardian Ltd; Nipashe, Alasiri, Kasheshe, Independent Television Ltd. (ITV), East Africa Television (EATV, formerly Channel 5)), Radio ONE, Sky-FM (in a joint venture with BBC) and East Africa Radio.
  7. Michael Ngaleko: Presicion Air Ltd
  8. Fidahussein: Africarriers,properties including heidary plaza, raha towers, zahra towers etc
  9. Yusuph Manji: Quality Group; Properties, Trucks
  10. Andrew Chenge: Worth US$ 1million (over 1 billion Tanzania shillings) in an overseas offshore account
  11. Nazir Mustafa Karamagi: Tanzania International Container Terminal
  12. Edward Ngoyayi Lowassa
  13. Mohammed Aboud
  14. Tarimba Abbas
  15. Philemon Ndesamburo
  16. Alex kajumulo
  17. Freeman Mbowe
..


Huyo Mbowe hizo fweza mnahesabia na zile anazodaiwa na NSSF? Na huyo kajumulo vipi kweli ana pesa ya kuingia kwenye orodha?? Naona mmemsahau Mjasiliamali Basil Pesambili Mramba hapo
 
Mkuu ninakuheshimu sana ila you can't make a list of rich people out of speculations.May I know under what criteria you listed the above as richest Tanzanians?
Thread yako inauliza jee hii ndiyo list ya matajiri wa Tanzania then hapo hapo umeshajibu na kusema kuwa listi ya Matajiri Tanzania ni hii iliyopo hapa chini.

Kevo, sio mimi. Soma vizuri maelezo:

Uchambuzi wa: https://www.jamiiforums.com/showthrea...428#post265428 (Unaweza kuongeza majina unayoyajua katika thread hii) unaonyesha kuwa listi ya Matajiri Tanzania ni hii iliyopo hapa chini.
 
Muulizeni Mzee Ndesa ajira kwenye kampuni zake zimekaaje zaidi ya ndugu, jamaa na kabila yake? Nenda pale Keys Hotel hapa Dar, utadhani uko KIBORLONI! Halafu anakataa Wamachinga wasipewe hela. Matajiri WAZAWA hawafai, bado wana safari ndefu ya kujifunza.

Bora hao wa Kiboriloni kuliko waKenya na wahindi.

Hebu fikiria zaidi. Ili mtu afanye biashara au kakiwanda kadogo anahitaji vitu vingapi? Kwa akili za wengi watafikiria tu hela. I think it requires more than money. In maana kama mtu hana hivyo vingine na akapewa tu fedha zitaishia bila kizifanyia chochote .NA hasa kama kati ya hivyo vitu atakuwa hana interpreneuship ,planning, hardworking , na bahati he/she is bound to fail despite the JK Billions.

Au atazitumia kama alivyoeleza Ndesa. Maana yake hazitarudi. Hebu mabenki waeleze ukweli kama hizo fedha zimerudi na kwa kiwango gani.
 
Tumtafute Mtanzania maskini kuliko wote tumchangie elfu mmoja mmoja, angalau tumnunulie jembe na mbegu aweze kujiondoa kwenye umaskini huwo maisha... vile vile ingekua sio mbaya tukampatia elfu tano kila mwezi hadi hapo atakapo weza kujitegemea...
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom