Tanzania tunaweza kuwa na wataalamu wa kuchunguza mitumba ya ndege, reli, mabehewa na vichwa vya treni?

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
47,018
144,376
Baada ya ufafanuzi wa Waziri wa Fedha kuhusu namna mitumba hiyo itavyokuwa inaingizwa nchini, haya ndio baadhi ya maswali ninalojiuliza na mpaka sasa sina majibu.

Je, wewe hapo uliopo, unaamini tunao wataalamu wa kukagua vifaa kama hivyo?

Je, si kweli kuna wakati itahitajika teknolojia katika ukaguzi wa vifaa na mitambo ya aina hiyo?

Je, hizo teknolojia tunazo au tutatumia za hao hao wanaoutuuzia?

Au itabidi tuingie mikataba na makampuni kutusaidia kufanya huo ukaguzi?

Risk ya kununua ndege used, inaweza kuwa justified na risk ya kununua magari used?

Na je, tumepata wapi uzoefu wa kukagua vyombo hivi mpaka tujiamini kuanza sasa?

Au kuna udharura wa kiwango hicho?

Au udharura uliopo ni muda mchache uliobaki kufika 2025?

Bongo kila siku afadhali ya jana!
 
Wabongo ukishawapatia tu 10%, kwisha habari yao. Wataruhusu/wataidhinisha kila aina ya takataka/madudu.

Uzalendo kwa nchi yao ni 0! Siku zote maslahi binafsi ndiyo kipaumbele chao.
 
Kwani sababu ya kununua vichwa na mabehewa ya treni mitunda, ndio hiyo sababu ya kununua magari used.

Magari mapya na mitumba yote yako sokoni hapo ilala kwa mnyamani ama Nyerere road. Lakini vichwa vya treni vipya haviko displayed sokoni kwa mnyamani. Inachukuwa miaka kadhaa mchakato wa kutoa order mpaka utengenezewe.

Umuhimu na justifications za kununua hiyo mitumba ya Magari na Ndege/Tereni vinaweza vikawa sawa.
 
Baada ya ufafanuzi wa Waziri wa Fedha kuhusu namna mitumba hiyo itavyokuwa inaingizwa nchini, haya ndio baadhi ya maswali ninalojiuliza na mpaka sasa sina majibu.

Je, wewe hapo uliopo, unaamini tunao wataalamu wa kukagua vifaa kama hivyo...
Kile kispika kina mwili kama mnyoo ndo kimetoa hiyo kauli eti wataalam ndo watajiridhisha kama mtumba unafaa, katika dunia iliyojaa umafia si mtoa huduma anaweza kutenga pesa ya maana ya kuja kuwahnga hawa wataalam ucharwa tukaletewa majeneza ya kuja kuwamaliz watanzania .kwa nin tunafanya vitu kama hatujaenda shule
 
Ujinga ujinga tu...
Yaani kama Taifa tunakwama sana!
Tulipaswa kudhibiti mitumba ili kuleta hamasa kwenye ubunifu na maendeleo ya teknolojia.
Lakini kufungulia soko la mitumba ni kukoswa ujinga!!
 
Baada ya ufafanuzi wa Waziri wa Fedha kuhusu namna mitumba hiyo itavyokuwa inaingizwa nchini, haya ndio baadhi ya maswali ninalojiuliza na mpaka sasa sina majibu.

Je, wewe hapo uliopo, unaamini tunao wataalamu wa kukagua vifaa kama hivyo?

Je, si kweli kuna wakati itahitajika teknolojia katika ukaguzi wa vifaa na mitambo ya aina hiyo?

Je, hizo teknolojia tunazo au tutatumia za hao hao wanaoutuuzia?

Au itabidi tuingie mikataba na makampuni kutusaidia kufanya huo ukaguzi?

Risk ya kununua ndege used, inaweza kuwa justified na risk ya kununua magari used?

Bongo kila siku afadhali ya jana!
Risk ya kununua ndege used, inaweza kuwa justified na risk ya kununua magari used?

Bongo kila siku afadhali ya jana!
 
Call a spead by its real name a spead, hilo tu. Na kama ni tatizo la kimaadili halitapatiwa ufumbuzi kwa kusubiri miaka 10 na ushee ili upate engine mpya.
 
Tunanunua vitu used sababu bajeti yetu hairuhusu kununua vipya, tunanunua vitu substandard kutoka china sababu bbajeti yetu hairuhusu kununua vipya
Mf. Mm nadrive kigari changu nlinunua 12mil, ila nina pikipiki nlibahatisha mnada wazungu wanafunga mradi nikanunua kwa 3miln ila bei yake mpya ni 15 miln ina functionality ya high na low na inaweza kulima.
Ila mchina katoa yake anauza 1.5mil
 
Mdogo wake museveni Salim Saleh alinunua helikopta 8 za. Mtumba kwa ajili ya UPDF matokeo yake kila asnayesoma magazeti anayajua.
 
Tukikomboa nchi kwa wakoloni weusi Hawa ni kuwanyonga tu hamna namna kwa jinsi walivyo linajisi na kuliaribu taifa .
 
Back
Top Bottom