#COVID19 Tanzania tunatumia njia zipi kubaini wageni wanoingia nchini wamepima Covid-19 na hawaambukizi wengine?

Richard

JF-Expert Member
Oct 23, 2006
14,939
20,399
Tanzania ni nchi ambayo ilipofikia kwa sasa ipo njia panda.

Macho ya maadui bado yameelekezwa kwetu kuona tunakwenda vipi baada ya kuondokewa na hayati Magufuli na viongozi wengine waandamizi akiwemo mhandisi Mfugale.

Ajira ni tatizo kubwa sana na vijana wahitimu wa shule na vyuo wengi wao wapo mitaani wanahangaika.

Nawapongeza makundi kama ya wasanii na vijana ambao wanajaribu kujikomboa kwa kutumia njia za kihalali.

Lakini lipo pia kundi kubwa ambalo ni la wale waso na shughuli kitendo kinachopolekea kukua kwa hali ya ujambazi na uporaji nchini.

Lakini je, vipi kuhusu kundi maalum ambalo kwa kutumia uhalifu wao linaweza kabisa kutumika kufanya uhalifu wa hali ya juu- MAUAJI kwa kutumia pia virusi vya Covid-19 .

Mbinu za maadui wa Tanzania zinabadilika kulingana na tabia zetu.

Je, twatumia njia zipi kubaini wageni wanoingia nchini na kama wamepima Covid-19 na wana vyeti halali vya kuthibitisha kuwa wapo negative?

Mgeni kabla hajatua nchini ni lazima awe amepima masaa 72 kabla na ana negative results.

Je, wageni wenye positive results tumewawekea taratibu zipi vigorously kuhakikisha hawendi hukio nje kuanza kusambaza ugonjwa?

Je, vipi watanzania ambao wameambukizwa Covid-19 wanaishia kurudishwa majumbani na vijijini na hatimae kuishia kufa huko au waachiwa tu wazurure mitaani kutafuta "victims"?

Kisha baada ya kufa kwa Covid twaambiwa "amefariki baada ya kuugua kwa muda mrefu/mfupi".

Je, yawezekana kundi hili kutumia njia ya kukohoa na kupiga chafya katika mikusanyiko kwa minajili ya kutaka kuambukiza watanzania wengine?

Watanzania tuzidishe uimara wa kutazama mambo yetu ya ndani na kuhakikisha kila kitu kipo katika mstari.

Yaonekana kidogo hali bado haijatengamaa
 
Nakumbuka ile tu baada ya covid kuingia,, zilikuwepo video za raia wa Kiasia wakionekana kwenye Street camera mbali mbali wakitema mate na kupakaza kwenye ngazi,milango na sehemu nyingine nyingi.

Kisa cha Kwanza Italy kilitokea baada ya jamaa mmoja kutoroka hospitali na kuingia kwenye wodi za wagonjwa mahututi,kutoka hapo Akakata mitaa ya kutosha kabla ya kukamatwa na kuwekwa karantini.

Na nikiangalia mikoa ynye maambukizi nazidi kupata wasiwasi, kwasababu ya idadi ya wazee wanaoishi huko

All in all haya yanayawezekana kabisa
 
Nakumbuka ile tu baada ya covid kuingia,, zilikuwepo video za raia wa Kiasia wakionekana kwenye Street camera mbali mbali wakitema mate na kupakaza kwenye ngazi,milango na sehemu nyingine nyingi...Kisa cha Kwanza Italy kilitokea baada ya jamaa mmoja kutoroka hospitali na kuingia kwenye wodi za wagonjwa mahututi,kutoka hapo Akakata mitaa ya kutosha kabla ya kukamatwa na kuwekwa karantini.

Na nikiangalia mikoa ynye maambukizi nazidi kupata wasiwasi,,kwasababu ya idadi ya wazee wanaoishi huko

All in all haya yanayawezekana kabisa
Hata kuhudhurua misiba achilia mbali shughuli za kuzika, yatakiwa uangalifu maana watu husahau kanuni.
 
Huwezi kuzungumzia madhara ya UVIKO huko nchini bila Jiwe kuwa ni chanzo cha kushamiri kwa ugonjwa huo hadi vifo lukuki!

If you are keen observer utakubaliana na mimi ugonjwa huu uliondosha watanzania wengi walio& wasio maarufu kwa kasi ya ajabu mnano January na February..! Guess what Kwa aina ya imani ambayo ilikua ni typical brainwashing kwa wabongo Jiwe alifanikiwa kuaminisha ugonjwa huu haupo nchini watu waliacha kujali kuchukua tahadhari zote zilizokuwa zikitolewa na wataalam..

Wataalam wetu nao waliwekwa kwapani na kuisaliti taaluma watoto wa mjini huita "mazima mazima" waliambiwa waseme tu ni changamoto "ndogo ndogo" za upumuaji huku jiwe akisema corona ni "futa" ukipiga mvuke linapotea...takwimu wala madhara ya ugonjwa huu kuanzia hapo hayakuonwa kwa wengi ila kuna watu wana majonzi na hasira kwa kuondokewa na ndugu zao huku wataalam (waziri na naibu wake) wakiwa ni wataaluma kwenye utabibu wakifanya mizaha kwenye mitandao! Kwenye hili na nilichoona kwa leo cha kupokea chanjo huyu waziri na naibu wake wanapaswa wawaombe radhi watanzania kwa madhara waliyosababisha hasa kwa kumsupport jiwe na ucheleweshaji chanjo for sure they should be held accountable..

Pichani ni maigizo yaliyogharimu maisha ya watu
images (22).jpeg
 
Back
Top Bottom