Tanzania tuna akiba ya forex ya kuagiza bidhaa na huduma nje kwa miezi sita au kutulisha wote kwa miezi mitatu

CM 1774858

JF-Expert Member
May 29, 2021
3,076
2,000

Akiba ya Fedha zetu za kigeni Rais Samia ameiongeza kwa TZS 2.3T sasa imefikia $5.8b toka $4.8b mwezi March 2021 | Pesa hii inaweza kulisha Watanzania wote kwa miezi mitatu mfululizo yaani Wale walale tu hakika Tanzania tuko vizuri Sana kwa sasa.​


"Hakuna kama Samia "​


Namba hazijawahi kudanganya na hazitadanganya tunaposema Rais Samia Suluhu Hassan rekodi zake hazikamatiki na mwendo wake unatoa matumaini mapya kila uchapo lazima kama taifa tukubaliane hivyo,

Fedha za kigeni ni muhimu kwa nchi hasa wakati wa majanga mbalimbali ambapo kwenye Jumuiya yetu ya Africa Mashariki ( EAC ) kiwango cha chini kwa nchi ni uwezo wa kuagiza bidhaa na huduma nje kwa muda usiopungua miezi 4.5 mfukulizo wakati kidunia tunapashwa kuhifadhi 20% ya kinachozunguka,

Rais Samia Suluhu Hassan pamoja na kuendekeza ujenzi wa SGR kwa zaidi ya TZS 10.2trl, Kujenga JNHPP kwa zaidi ya TZS 6.55trl, kugharamia elimu bila malipo kwa watoto wetu, kupandisha madaraja|mishahara wafanyakazi wa serikali,kutoa mikopo HESLB ya zaidi ya Tshs 570b,anajenga vituo vya afya 220, kujenga madarasa 18,000, kujenga mabarabara na madaraja kila kona ya nchi,

Pamoja na yote hayo Rais Samia amefanikiwa kuongeza akiba yetu ya fedha za kigeni ( Gross official foreign reserves ) kwa zaidi ya $1BL sawa na Tshs 2.3trl na sasa imefikia Jumla ya $5.8BL karibu Tshs 13.34trl kutoka $4.8BL aliyoikuta,Hakika Rais Samia anamwendo,

Fedha hizi zinaweza kuagiza bidhaa na huduma nje kwa zaidi ya miezi 6.4 mfululizo rekodi ambayo sina hakika kama kuna Rais yeyote tangu tupate Uhuru aliwahi Kuifikia.

Hata hivyo, kwakuwa GDP per Capita yetu ni TZS 2,653.8 au $1,156.8 basi pesa hii inaweza kumlipa kila Mtanzania kwa kila siku TZS 2,700 kwa miezi mitatu mfululizo yaani asifanye kazi yeyote ale na alale tu,Hakika Rais Samia ni tumaini jipya linalohitaji kuungwa mkono na kila awaye.

Baadhi ya faida za Gross official foreign reserves kwa nchi ni hizi,

Kwanza,kuiwezesha Serikali kutimiza mahitaji yake ya fedha za kigeni na mahitaji ya kuagiza bidhaa kutoka nje,

Pili,Kutoa imani kwamba Serikali inaweza ikatimiza majukumu yake ya muda mfupi kama kulipia madeni ya nje,

Tatu, Kusaidia utekelezaji wa sera za fedha na kubadilisha fedha za kigeni pamoja na uwezo wa kuingilia kuhakikisha fedha ya taifa ni imara,

Nne, Kuchangia katika mapato ya Benki Kuu kwa kuhakikisha kuna kiwango cha kutosha cha mapato kulingana na jinsi Benki inavyoweza kuhimili majanga/vihatarishi

IMG-20211010-WA0032.jpg
 

KENZY

JF-Expert Member
Dec 27, 2015
20,198
2,000
🤣🤣🤣🤣 Nimecheka kwa sauti,

Mkuu hii ni kama itatokea shida ndio zitafanya kazi kwa sasa ni akiba yetu
Wabadili hizo fedha ziwe zahabu maana pesa za kigeni nazo kwa kushuka thamani ni hazijambo,vipi thamani ya dola ikirudi 1500 Kama kipinde kile 2012...
 

Rufiji dam

JF-Expert Member
Feb 20, 2020
2,245
2,000
Uongo upi mkuu Wangu?

Nikweli mama hataki kujivuna ila anafanya makubwa Sana#KAZIIENDELEE KWA KASI & WELEDI ZAIDI
Makubwa haya yako wapi na hafanyi yeye sema mfumo unaanza kutengenezwa kurekebisha makosa aliyofanya na Mwendazake. Pia inawezekana vipi akatoa mafanikio hayo ambayo yalipaswa kutolewa na Waziri wa Fedha ama CAG. Tuache kudanganyana.
 

CM 1774858

JF-Expert Member
May 29, 2021
3,076
2,000
Kipindi cha mwenda zake tuliambiwa tuna akiba ya kutulisha miezi 6!Sasa hapa sielewi,inamaana kuna watu walikula za miezi
Sasa $4.8BL unawezakula miezi sita kama tutapewa bukubuku per day,

Ila kama ni GDP Per Capita isingewezekana,

Kima cha chini cha maisha Tanzania ni Tshs 2,700 kwa kichwa kwa Siku,

Sasa fanya hesabu utaona
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom