Tanzania tuna akiba ya forex ya kuagiza bidhaa na huduma nje kwa miezi sita au kutulisha wote kwa miezi mitatu

CM 1774858

JF-Expert Member
May 29, 2021
4,980
4,075

Akiba ya Fedha zetu za kigeni Rais Samia ameiongeza kwa $1.5BL sasa imefikia $6.253BL toka $4.8b mwezi March 2021​


| Pesa hii inaweza kulisha Watanzania wote kwa miezi mitatu mfululizo yaani Wale walale tu au kuagiza bidhaa na huduma nje kwa miezi 7,​

===

Namba hazijawahi kudanganya na hazitadanganya tunaposema Rais Samia Suluhu Hassan rekodi zake hazikamatiki tunamaanisha mambo kama haya ya FX reserves,

Tunaposema mwendo wa Rais Samia Suluhu Hassan unatoa matumaini mapya kila uchapo lazima kama taifa tukubaliane hivyo kwani ndivyo ilivyo,

Fedha za kigeni ni muhimu kwa nchi hasa wakati wa majanga mbalimbali yanayo weza kulikumba Taifa letu Wakati ufaao na Usiofaa,

FX reserves kwenye Jumuiya yetu ya Africa Mashariki ( EAC ) kiwango cha chini kwa nchi ni uwezo wa kuagiza bidhaa na huduma nje kwa muda usiopungua miezi 4.5,Tanzania chini ya Rais Samia tumevuka lengo na kufikia miezi 7,

FX reserves kwa kiwango cha kidunia tunapashwa kuhifadhi 20% ya kinachozunguka nchini kwenu kiasi ambacho kama nchi pia tumevuka lengo hili,

Rais Samia Suluhu Hassan pamoja na kuendekeza ujenzi wa SGR kwa zaidi ya TZS 10.2trl,Kujenga JNHPP kwa zaidi ya TZS 6.55trl,

Rais Samia pamoja na kugharamia elimu bila malipo kwa watoto wetu wote,kupandisha madaraja|mishahara wafanyakazi wa Serikali na mashirika ya Umma,

Rais Samia pamoja na kutoa mikopo HESLB ya zaidi ya Tshs 570b,anajenga vituo vya afya 220, kujenga madarasa 18,000, kujenga mabarabara na madaraja kila kona ya nchi,

Pamoja na yote hayo Rais Samia amefanikiwa kuongeza akiba yetu ya fedha za kigeni ( Gross official foreign reserves ) kwa zaidi ya $1.5BL sawa na TZS 3.5trl na sasa imefikia Jumla ya $6.253BL karibu TZS 14.4trl kutoka $4.8BL aliyoikuta,Hakika Rais Samia anamwendo,

Fedha hizi zinaweza kuagiza bidhaa na huduma nje kwa zaidi ya miezi 7 mfululizo rekodi ambayo sina hakika kama kuna Rais yeyote tangu tupate Uhuru aliwahi Kuifikia.

Hata hivyo, kwakuwa GDP per Capita yetu ni TZS 2,653.8 au $1,156.8 basi pesa hii inaweza kumlipa kila Mtanzania kwa kila siku TZS 2,700 kwa miezi mitatu mfululizo yaani asifanye kazi yeyote ale na alale tu,

Hakika Rais Samia Suluhu Hassan ni tumaini jipya linalohitaji kuungwa mkono na kila anayelitakia mema Taifa letu hapo baadae,

Baadhi ya faida za Gross official foreign reserves kwa nchi ni hizi,

Kwanza,kuiwezesha Serikali kutimiza mahitaji yake ya fedha za kigeni na mahitaji ya kuagiza bidhaa kutoka nje,

Pili,Kutoa imani kwamba Serikali inaweza ikatimiza majukumu yake ya muda mfupi kama kulipia madeni ya nje,

Tatu, Kusaidia utekelezaji wa sera za fedha na kubadilisha fedha za kigeni pamoja na uwezo wa kuingilia kuhakikisha fedha ya taifa ni imara,

Nne, Kuchangia katika mapato ya Benki Kuu kwa kuhakikisha kuna kiwango cha kutosha cha mapato kulingana na jinsi Benki inavyoweza kuhimili majanga/vihatarishi

IMG-20211010-WA0032.jpg
 
Hata wakisema tuna Dola billion 50 Nani anaweza Ku verify kile wanachosema? Huyu mama na Serikali yake kitu pekee ninachoweza kuwaamini ni salamu tu zaidi ya hapo ni uongo Tu .
BOT mkuu Wangu,


#KAZIIENDELEE KWA KASI & WELEDI ZAIDI
 
🤣🤣🤣🤣 Nimecheka kwa sauti,

Mkuu hii ni kama itatokea shida ndio zitafanya kazi kwa sasa ni akiba yetu
Wabadili hizo fedha ziwe zahabu maana pesa za kigeni nazo kwa kushuka thamani ni hazijambo,vipi thamani ya dola ikirudi 1500 Kama kipinde kile 2012...
 
Uongo upi mkuu Wangu?

Nikweli mama hataki kujivuna ila anafanya makubwa Sana



#KAZIIENDELEE KWA KASI & WELEDI ZAIDI
Makubwa haya yako wapi na hafanyi yeye sema mfumo unaanza kutengenezwa kurekebisha makosa aliyofanya na Mwendazake. Pia inawezekana vipi akatoa mafanikio hayo ambayo yalipaswa kutolewa na Waziri wa Fedha ama CAG. Tuache kudanganyana.
 
Kipindi cha mwenda zake tuliambiwa tuna akiba ya kutulisha miezi 6!Sasa hapa sielewi,inamaana kuna watu walikula za miezi
Sasa $4.8BL unawezakula miezi sita kama tutapewa bukubuku per day,

Ila kama ni GDP Per Capita isingewezekana,

Kima cha chini cha maisha Tanzania ni Tshs 2,700 kwa kichwa kwa Siku,

Sasa fanya hesabu utaona
 
22 Reactions
Reply
Back
Top Bottom