Mimi binafsi,Nalaani hiki kitendo cha kudekezwa Kwa nchi zetu hizi za Africa,
Najua, nitaungwa mkono na wachache hasa ambao wamewahi kutafuta maisha kupitia mikono ya ndugu na jamaa zao, waliishi kama watumwa wakiwa huko, lakini ukiongea nao leo, wengi Wao wametusua maisha kushinda hata watoto wa familia zile walizokuwa wakiishi Kwa mateso na unyanyasaji
Nachoomba, tuwapigeni vita mafisadi wote wanaojilimbikizia Mali na wizi selikarilini, tupigeni vita uzembe mahali popote pale kazini
Tuwakataeni mafisdi wote wanaotoka Vyama Vyote, na tupate viongozi wenye uchungu na nchi, wakali, wasiopendelea, tupate katiba bora, Upinzani wa Vyama uimarishwe, tujenge nchi yetu,
Tena kama ikiwezekana, Vyama vyenyewe vianze kutuletea watu wasio na makandokando, waanze wenyewe kukataa mafisadi kwenye Vyama vyao huko huko kabla hata hawajatuletea huku kuwapigia Kura,
Chama chochote kama ni kikwazo Kwa nchi yetu, tuseme basi,
Tukiweza la kuzuwia wizi na uzembe kazini, hatujitaji misaada[/QUOTE]