Tanzania tuliona Corona kwenye kuku na mbuzi tukawawajibisha wafanyakazi Maabara ya Taifa; China wanaona Corona kwenye kuku wanajiuliza wameingiaje!

Synthesizer

JF-Expert Member
Feb 15, 2010
11,143
18,774
Juzi hapa China ilikuta kwamba baadhi ya mifuko ya kuku na kamba ilikutwa ina wadudu wa Corona (Covid-19). KIlichofuata ni kwamba serikali ya China ilianza kujiuliza maswali mengi kuhusu jinsi gani hao wadudu waliingia kwenye kuku na kamba ambavyo viliagizwa kutoka nchi ya Brazil.

China walienda mbali pia, na kufuatilia wote walioshika hiyo mifuko ya kuku na kamba wapimwe ili kujua kwamba wako salama.

Jambo hili lilinikumbusha kipindi kile ambapo raisi wetu aliitangazia dunia kwamba walipeleka sampuli za mapapai na mbuzi kwenye maabara ya Taifa, na vipimo vilivyotoka positive basi shutuma nyingi zikatolewa kwa maabara! Nakumbuka kuna watu walisimamishwa kazi kwa ajili ya kukuta virusi vya Corona kwenye papai na mbuzi!

Yaani uwezo wetu wa kufikiri uliishia kwenye kudhani kuwa wafanyakazi wa maabara walifanya uzembe au udanganyifu kwenye kupima papai na kukuta lina virusi vya Corona! Kwa kuwa na fikra kama hizi pale ambapo watu kama Trump wa Marekani wakiziita nchi zetu majina ya kuudhi tutakuwa na uhalali wa kukasirika?

Sasa baada ya tukio hili la hina nimejiuliza sana. Je ni kweli sisi Waafrika tuna namna yetu ya kufikiri na kuamua mambo tofauti na watu wengine? Sijui kama lile papai lililokutwa na virusi vya Corona lilitoka nyumbani kwa nani, kwa sababu watu wa nyumba ile wote walipaswa kupimwa huenda wao ndio waliliambukiza papai virusi vya Corona! Hata hivyo ni furaha kujua kwamba hawakuumwa na kupoteza maisha.

Source: Two Chinese cities find traces of coronavirus in imported chicken wings and frozen shrimp
 
Ukiona umeandika thread ndeeeeefu halafu hakuna hata majadiliano na watu wanaipita tu ujue kuwa Thread hiyo haieleweki...
 
Najisikia vibaya kuikandamiza race yetu ila siku zote ukweli lazima ukuumize.

Africans sijui nini hasa cha matatizo yetu. nimekuwa nikijiuliza kwanini mabara mengine yanazidi kukua na kugundua vitu vipya kila siku? ila majibu yanakuja mengi na kushindwa kujua lipi ni sahihi.

Kwanini whites na sio sisi?
Ukiangalia kabla ya ukoloni kuja Africa. whites tayari walishabuni saa tayari. tayari walikuwa na watu wenye faida kwenye jamii yao mf Newton.
Kwakua sisi hatuna historia kabla ya ukoloni hivyo sisi ukilinganisha na mfumo wa maisha yetu ya leo basi nadhani kwenye miaka ya 1650 tulikua tukivaa magome ya miti.

Tatizo ni nini Waafrika?.
 
Mkuu hakuna aliyekukataza kuchunguza Oil ilikuwaje na Corona.
 
Ukiona umeandika thread ndeeeeefu halafu hakuna hata majadiliano na watu wanaipita tu ujue kuwa Thread hiyo haieleweki...
Hahaha! Mkuu, sikutaka wale wadandiaji waje na maneno yao ya kipuuzi. Hivyo nimeiandika kwa mtu anaejua kusoma kuelewa. Acha hao wengine waende kwenye thread za Waziri kapiga sita!

Hebu ona basi, hata wewe umeona hii thread ndefu mno kusoma!
 
Najisikia vibaya kuikandamiza race yetu ila siku zote ukweli lazima ukuumize.

Africans sijui nini hasa cha matatizo yetu. nimekuwa nikijiuliza kwanini mabara mengine yanazidi kukua na kugundua vitu vipya kila siku? ila majibu yanakuja mengi na kushindwa kujua lipi ni sahihi.

Kwanini whites na sio sisi?
Ukiangalia kabla ya ukoloni kuja Africa. whites tayari walishabuni saa tayari. tayari walikuwa na watu wenye faida kwenye jamii yao mf Newton.
Kwakua sisi hatuna historia kabla ya ukoloni hivyo sisi ukilinganisha na mfumo wa maisha yetu ya leo basi nadhani kwenye miaka ya 1650 tulikua tukivaa magome ya miti.

Tatizo ni nini Waafrika?.
Afrika tuna mawazo mengi sana ya jinsi ya ku-survive; Mishahara kidogo na hiyo kidogo tulishe family, tusaidie ndugu wa ukoo, tusaidie upande wa wakwe, tusaidie mtoto wa jirani kaja toka kijijini hana sehemu ya kulala, tuwape polisi wakitubambikia kesi, tufikirie adha ya usafiri wa daladala kurudi nyumbani, tuwaze kodi ya nyumba imefika, nk, nk.

Sasa saa ngapi utawaza mambo ya maabara na kubuni?
 
Kugundua vitu vingine mbali ya kuwa na maisha ya kujikimu maana maisha pia lazima yaendelee kuna brain wash kubwa sana kwa waafrika hadi imefikia tukiwa na mtafaruku tunampelekea mzungu kushitakia. Ni aibu na wazungu wanatuona tunaakili za kitoto. Desturi zetu leo ni uncivilised, ukisema korona haina formal tiba tumia njia mbadala wasomi wanasema haijawa proved kisayansi lkn wazungu wanatumia na ina jina kabisa "hot toddy".
Kwenye ugunduzi ni mfano mzuri wa wale wa Umeme wa Magufuli system ya wasomi haikuwakubali. Ukigundua bunduki kama yule wa Iringa alikuwa ana kamatwa. Well ni ubinafsi na kutokujitambua. Mzungu keshafanya damage kwetu sisi, leo hii ukifika Ulaya, Australia na kwingineko chinese herbs shops za kumwaga, waafrika aibu.
 
Mie nadhani tatizo la Afrika ni kwamba tuna wivu wa kijinga sana.

Jirani akigundua kitu kizuri badala ya kumpongeza, kwa sababu za kibinafsi za wivu tunatafuta namna a kumkwamisha, na kama tuna madaraka ndio linakuja hilo la kusema kwa nini umetengeneza helikopta au bunduki bila kibali. Kama kibali kinahitajika la msingi basi ni wewe unipongeze na kunipatia kibali sio kunitishia kuniweka ndani.

Na Afrika kila tunapokosea hatutaki kujifunza kutokana na kosa, bali tunatafuta mtu wa kumlaumu. Mara nyingi wa kwanza kulaumiwa ni viongizi wa vyama vya upinzani. Wa pili nchi za nje - mabeberu.

Na tangu nyakati zitulazimishe kuingia mfumo wa vyama vingi, tumeingiliwa na kirusu kibaya sana cha kuona kwamba kukubali wazo lolote zuri la kutoka mtu asiye chama chetu basi ni kuwapa nafasi wao waje wawe chama tawala. Kwa hiyo hata kama wazo lao ni nzuri sana kuzidi wazo letu, au hata kama wakionyesha wazi sana kwamba tnakosea katika kufanya jambo fulani, tutawaambia wanapinga kila kitu, hawataki maendeleo, sio wazalendo nk.

Haya ni matatizo makubwa sana ndani ya Afrika
 
Back
Top Bottom