Synthesizer
JF-Expert Member
- Feb 15, 2010
- 11,129
- 18,737
Juzi hapa China ilikuta kwamba baadhi ya mifuko ya kuku na kamba ilikutwa ina wadudu wa Corona (Covid-19). KIlichofuata ni kwamba serikali ya China ilianza kujiuliza maswali mengi kuhusu jinsi gani hao wadudu waliingia kwenye kuku na kamba ambavyo viliagizwa kutoka nchi ya Brazil.
China walienda mbali pia, na kufuatilia wote walioshika hiyo mifuko ya kuku na kamba wapimwe ili kujua kwamba wako salama.
Jambo hili lilinikumbusha kipindi kile ambapo raisi wetu aliitangazia dunia kwamba walipeleka sampuli za mapapai na mbuzi kwenye maabara ya Taifa, na vipimo vilivyotoka positive basi shutuma nyingi zikatolewa kwa maabara! Nakumbuka kuna watu walisimamishwa kazi kwa ajili ya kukuta virusi vya Corona kwenye papai na mbuzi!
Yaani uwezo wetu wa kufikiri uliishia kwenye kudhani kuwa wafanyakazi wa maabara walifanya uzembe au udanganyifu kwenye kupima papai na kukuta lina virusi vya Corona! Kwa kuwa na fikra kama hizi pale ambapo watu kama Trump wa Marekani wakiziita nchi zetu majina ya kuudhi tutakuwa na uhalali wa kukasirika?
Sasa baada ya tukio hili la hina nimejiuliza sana. Je ni kweli sisi Waafrika tuna namna yetu ya kufikiri na kuamua mambo tofauti na watu wengine? Sijui kama lile papai lililokutwa na virusi vya Corona lilitoka nyumbani kwa nani, kwa sababu watu wa nyumba ile wote walipaswa kupimwa huenda wao ndio waliliambukiza papai virusi vya Corona! Hata hivyo ni furaha kujua kwamba hawakuumwa na kupoteza maisha.
Source: Two Chinese cities find traces of coronavirus in imported chicken wings and frozen shrimp