China yarekebisha hatua zake za kukabiliana na COVID-19

ldleo

JF-Expert Member
Jan 9, 2010
1,010
1,035
VCG111417208339.jpg
Kuanzia tarehe 8 mwezi Januari, China imerekebisha hatua zake za kukabiliana na janga la COVID-19 kutoka ngazi A hadi B. Kwa mujibu wa hatua mpya, watu walioambukizwa na virusi vya Corona hawatawekwa karantini tena, na watu wanaoingia nchini China kutoka nchi za nje pia hawatalazimishwa tena kupima virusi.

Katika miaka mitatu iliyopita, China imechukua hatua madhubuti katika kukabiliana na janga la COVID-19, na kuepusha maambukizi makubwa ya virusi vya kiasili na virusi aina ya Delta ambavyo ni hatari sana, na kupunguza kwa kiasi kikubwa idadi ya vifo vya watu. Hatua hizo pia ziliipatia China muda wa kutafiti chanjo na dawa. Katika miaka mitatu iliyopita, viwango vya maambukizi ya virusi vya Corona na vifo vilivyosababishwa na virusi hivyo nchini China vilikuwa chini zaidi duniani. Wakati viashiria vya maendeleo ya binadamu duniani vilipopungua kwa miaka miwili mfululizo, viashiria hivyo nchini China vilipanda kwa nafasi 6, na wastani wa umri wa kuishi wa Wachina umeongezeka kutoka miaka 77.3 mwaka 2019 hadi miaka 78.2 mwaka 2021.

Tangu mwaka jana, China imekuwa inafuatilia sana hali ya maambukizi na mabadiliko ya virusi, kuongeza kiwango cha chanjo kwa wananchi kwa juhudi zote, na kufanya maandalizi ya kukabiliana na maambukizi makubwa kwa umakini. Hivi sasa virusi vya Omicron vimekuwa virusi vikuu vya Corona duniani, na ingawa virusi hivyo vina uwezo mkubwa wa kuambukiza, lakini sumu yake imepungua kwa kiasi kikubwa. Wakati huo huo, kiwango cha chanjo kwa wananchi nchini China kimezidi asilimia 90, na kiwango hicho kwa watu wenye umri wa zaidi ya miaka 60 kimezidi asilimia 85. Baada ya tathmini ya kina kuhusu virusi hivyo, China imerekebisha sera na hatua zake, kwa kufuata mwelekeo wa hatua za kuzuia na kudhibiti janga la COVID-19 duniani, na matumaini ya watu kurejesha maisha ya kawaida. Wakati huo huo, hali hii haimaanishi kwamba China imeacha kabisa juhudi za kukabiliana na janga hilo, bali China kwa sasa imeweka kipaumbele katika kulinda wazee haswa wale wenye magonjwa sugu.

Wakati huo huo, China pia imeboresha sera yake kuhusu watu wanaoingia na kutoka nchini China. Hatua ambayo itasaidia kurejesha mawasiliano ya watu kati ya China na nchi za nje, kuongeza uwekezaji na kukuza utalii, na hatua hii imepongezwa na nchi mbalimbali duniani zikiwemo nchi za Afrika.

Mtaalamu wa masuala ya kimataifa wa Kenya, Cavince Adhere anaona kuwa, marekebisho ya hatua za China za kukabiliana na janga la COVID-19 ni jambo zuri kwa uchumi wa dunia, na yatahimiza maendeleo ya uchumi duniani, haswa utalii. Amesema kwa mujibu wa takwimu za Shirika la Utalii Duniani, kabla ya mlipuko wa janga hilo, China ilikuwa miongoni mwa nchi zinazoongoza duniani kwa matumizi ya kiutalii katika nchi za nje, na marekebisho ya hatua za kukabiliana na COVID-19, sio kama tu yatanufaika soko la utalii barani Asia na Ulaya, bali pia yataleta faida kubwa kwa sekta za utalii barani Afrika.
 
Back
Top Bottom