Inabidi pia ueleze watu Kenya anapatia kwenye nini.
Kenya inaongoza kwa tatizo la ajira ukanda huu
Kenya inaongoza kwa rushwa mbaya ukanda huu
Kenya ina raia wenye maisha duni zaidi ukanda huu
Kenya gharama za maisha ziko juu zaidi, mbali ya kwamba wana uchumi mkubwa wakiwa wachache zaidi yetu
Kenya ina siasa chafu, sisi zina kasoro moja ndogo tu
Ukabila na ukosefu wa umoja wa kitaifa ni tatizo sugu Kenya
Kwa kukutaarifu tu, wana mabaya mengi zaidi kuliko mazuri machache waliyotuzidi, ambayo hata hivyo yanakwenda yakibadirishwa kuwazidi siku si nyingi.
Msiishi kwa stori za mitandaoni, tembeeni.
Naona umepandwa na wazimu, hizi hapa takwimu za world bank na IMF waliosema nyinyi ni low middle income na mkashangilia.
i) 32% ya Kenya ndio maskini yani wanatumia chini ya $1.9 kwa siku, Tanzania ni 60% kwa sababu hiyo idadi wanaishi chini ya $1.9 kwa siku (IMF).
ii) Kenya raia wana afya nzuri kulingana na world bank na WFP. Tanzania inaongoza eac kwa kuwa na watoto wenye utapia mlo ingawa mnapanda chakula na kuuza mpaka kenya na watoto ambao akili zao hazikui vizuri kwa kukosa lishe bora. (WFP na WHO).
iii) Ikifika kwa elimu hata usitaje ukanda huu ni Uganda tu ndio infata Kenya.(University rankings, IMF na World bank).
iv) Kwa kutimiza malengo ya maisha Kenya ni namba ya tatu afrika ikifata sychelles na mauritius.Yani mtoto akizaliwa na kusoma Kenya ako na 62% chance ya kutimiza malengo yake kwa maisha. (Human capital index report 2020)
v) Mkenya wa kawaida anaishi miaka 4 zaidi kushinda mtanzania (WHO).
v) Kwa inequality Tanzania inashinda Kenya, Tanzania iko na millionaires wengi kushinda kenya lakini pia 60% ya watu Tanzania ni maskini wa kutupwa. (IMF poverty report). Tanzania bado iko katika nchi 28 maskini kabisa duniani.
vi) Kwa miundo mbinu Tanzania iko chini sana, port ya mombasa (2.7 million teus capacity) kwa sahi ni mara 2 ya port zote nne za Tanzania nikiunganishwa na bado inazidi kupanuliwa itafikia 4 million teus mwaka 2022 december. Kenya iko na bara bara kubwa kushinda Tanzania na sahi tunajenga flyover highway ya 27km ikipita kati kati ya jiji la Nairobi kutoka kwa uwanja wa ndege.
vii) Tanzania na burundi zinaongoza eac kwa kuwa na watoto wanaofariki kabla ya kufika miaka 5. Hapa tena lishe bora na usafi iliangaziwa na World bank.
Kwa hivyo najua unataka kujipa consolation lakini hiyo propaganda yenyu yote ni kelele.