Tanzania tulikosea wapi na Kenya walipatia wapi?

Elimu yetu ni mfu, kwa ufupi tunamfumo wa elimu ya kusoma historia za maandishi ya wengine kuanzia kwenye hesabu hadi baiolojia hivo tunawaandaa wanafunzi kukariri hizo historia ili wajibu mitihani na sio waweze kujitegemea haipo hiyo na ndio maana anaekushauri ujiajiri nae kaajiriwa,
 
Nilitaka kuandika haya ila nashukuru umenisaidia kusema.
Mtoa mada amesumuliwa tu kuwa Wakenya wana maisha mazuri akaamua kuleta uzi hapa.
Bahati nzuri Kenya niliwahi kukaa raia wao wana maisha magumu mno kuliko kawaida.
Kule kama hauna kazi rasmi ya kukupatia mshahara kwa mwezi maisha ni magumu mno kuingiza hata buku ni bahati nasibu.
Inabidi pia ueleze watu Kenya anapatia kwenye nini.

Kenya inaongoza kwa tatizo la ajira ukanda huu
Kenya inaongoza kwa rushwa mbaya ukanda huu
Kenya ina raia wenye maisha duni zaidi ukanda huu
Kenya gharama za maisha ziko juu zaidi, mbali ya kwamba wana uchumi mkubwa wakiwa wachache zaidi yetu
Kenya ina siasa chafu, sisi zina kasoro moja ndogo tu
Ukabila na ukosefu wa umoja wa kitaifa ni tatizo sugu Kenya

Kwa kukutaarifu tu, wana mabaya mengi zaidi kuliko mazuri machache waliyotuzidi, ambayo hata hivyo yanakwenda yakibadirishwa kuwazidi siku si nyingi.

Msiishi kwa stori za mitandaoni, tembeeni.
 
bongo unakaa stand unaomba nauli unapata unaenda posta,unaosha magari unarudi na elfu 3,easy tu.

halafu mtu anaponda ujamaa.
 
Wakenya ndio watu wa kwanza kuanza kulima maua na kusafirisha nje wakaambukiza na mikoa ya Arusha kilimo cha maua, jiulize huo mfumo wa kilimo wa kutumia greenhouse walianza wakenya ndio ukaja hadi Tanzania, na Tanzania kwa position iliyopo ingepata viongozi makini jumlisha bandari tu ya DSM basi biashara ingeshamiri sana na ukanda wote huu ungechangamka na kututegemea lakini ndio hivo
 
Yes na hiyo ndio kitu kinafanya maisha ya bongo kuwa marahisi.
Tanzania kuna watu asilimia 70 hawana kazi maalum inayotambulika lakini wanaishi maisha safi kabisa na wanasababisha foleni wengine utawakuta wanashinda kwenye vijiwe vya kahawa huku wanasikilizia simu iite baadae pesa inaingia na watoto wanakula vizuri wanalala mahali pazuri pia wanasoma shule nzuri,lakini kenya kama hauna kazi maalum unakuwa umechoka kama chokoraa,wakikaa kijiweni hawaingizi hata mia.
Kama umewahi kufika Arusha ukaona staili ya maisha ya watu wa Arusha ndio ilitaka kufanana na Kenya.
bongo unakaa stand unaomba nauli unapata unaenda posta,unaosha magari unarudi na elfu 3,easy tu.

halafu mtu anaponda ujamaa.
 
Yes na hiyo ndio kitu kinafanya maisha ya bongo kuwa marahisi.
Tanzania kuna watu asilimia 70 hawana kazi maalum inayotambulika lakini wanaishi maisha safi kabisa na wanasababisha foleni wengine utawakuta wanashinda kwenye vijiwe vya kahawa huku wanasikilizia simu iite baadae pesa inaingia na watoto wanakula vizuri wanalala mahali pazuri pia wanasoma shule nzuri,lakini kenya kama hauna kazi maalum unakuwa umechoka kama chokoraa,wakikaa kijiweni hawaingizi hata mia.
Kama umewahi kufika Arusha ukaona staili ya maisha ya watu wa Arusha ndio ilitaka kufanana na Kenya.

si ndio hapo mkuu.

magufuli hajaajiri watu ajira zilizobeba watu wengi miaka zaidi ya 4,lakini ni hakuna kilichobadirika mtaani.
 
Mtanzania wa leo ni Pimbi!
605758310.jpg
 
yes ukiwa mjanja bado life linasonga.
Halafu bongo bado kuna fursa nyingi sana ambazo bado watu hawajaziona na kuzichangamkia kwa sababu bado tuna ule utamaduni wa kuchagua kazi ya kufanya.
Ila kuna wageni kama wachina au wanaijeria huwa wakija wanazivamia na kupiga mamilioni halafu wabongo wanashtuka baadae sana.
si ndio hapo mkuu.

magufuli hajaajiri watu ajira zilizobeba watu wengi miaka zaidi ya 4,lakini ni hakuna kilichobadirika mtaani.
 
Kuna sababu nyingi zilizoleta tofauti kubwa katika nyanza nyingi kati ya Tanzania na Kenya iliyopata Uhuru miaka miwili baada ya sisi. Sababu kubwa kabisa ni elimu iliyoharibiwa toka Awamu ya Kwanza muda mfupi tu baada ya Uhuru katika juhudi ya kuleta elimu nzuri ya Kitanganyika tofauti na ile ya Kikoloni. Elimu hiyo mpya ilikuwa na makosa mengi yaliyoadhiri ubora lakini kosa kubwa kabisa ilikuwa kuondoa kabisa Darasa la Nane ambalo lilikuwa la mwisho Shule za Msingi. Hii ikawa sawa na kubomoa msingi wa nyumba ukaendelea kujenga nyumba ukitegemea itakuwa imara ya kudumu. Kenya nao waliiga mtindo huo lakini waligundua kosa hilo mapema na kurekabisha miaka michache tu baadaye na kurudisha Darasa la Nane hadi leo badala yake waliondoa kabisa Form Six. Wakenya wakaja na mfumo wa 8-4-4 ikiwa na maana ya miaka 8 Msingi, miaka 4 Sekondari na miaka 4 Chuo Kikuu digrii ya kwanza. Hii ina maana Form Five ilihamishiwa Chuo Kikuu kumuandaa mwanafunzi kuingia Chuoni. Huu ndo mfumo uliokuwapo Chuo Kikuu cha Makerere kabla ya Uhuru wa nchi zote tatu za Afrika Mashariki. Zambia wao walifutilia mbali Form Five na Six wakabaki na Form Four tu na wanafunzi wao wanapokelewa vyuo vyote duniani wa kwetu wa Form Six wakikataliwa. Bahati mbaya sana toka Awamu ya Kwanza kila Waziri anayeteuliwa kuongoza Wizara ya Elimu alikuja na mbinu zake za kuboresha elimu lakini amekuwa akimaliza kwa kuharibu zaidi. Matokeo yake sasa hivi kila kiongozi Serikalini, Bungeni na Mahakamani ana PhD ambayo haijulikani ni ya Chuo gani wala fani gani ikileta hisia tofautitofauti juu ya elimu ya viongozi wetu.
Kwa sasa tuna mfumo mpya unaitwa CBC ( 2-6-3-3-3) bali si 8-4-4
 
Inabidi pia ueleze watu Kenya anapatia kwenye nini.

Kenya inaongoza kwa tatizo la ajira ukanda huu
Kenya inaongoza kwa rushwa mbaya ukanda huu
Kenya ina raia wenye maisha duni zaidi ukanda huu
Kenya gharama za maisha ziko juu zaidi, mbali ya kwamba wana uchumi mkubwa wakiwa wachache zaidi yetu
Kenya ina siasa chafu, sisi zina kasoro moja ndogo tu
Ukabila na ukosefu wa umoja wa kitaifa ni tatizo sugu Kenya

Kwa kukutaarifu tu, wana mabaya mengi zaidi kuliko mazuri machache waliyotuzidi, ambayo hata hivyo yanakwenda yakibadirishwa kuwazidi siku si nyingi.

Msiishi kwa stori za mitandaoni, tembeeni.
Weee acha kupotosha. Acha kusema mambo kama uko gengeni au bar, bila takwimu. Yote uliyasema yanahitajia ushahidi na takwimu. Umejuaje inaongoza kwa tatizo la ajira ukanda huu? Kenya ina raia wenye Maisha duni Zaidi? Kweli? Hata gharama ya Maisha ni jambo relative. Kenya wana pato kubwa zaidi per capita kuliko Tanzania, ndiyo maana mkawafungia wasije wakamaliza kununua mashamba yenu.
Sipendi mtu anayejisemea kwa chuki na emotions bila facts. Hayo ungeyasemea bar tu. Wana mabaya mengi kuliko sisi? My ar..!
 
napotosha kwa misingi gani??,yafaa utulize kichwa kisha ujue maana mtu kaandika nini.haipendezi unakurupuka tu kujibu.

mimi kutokukupa data haimaanishi ninachosema ni uongo,useme unataka data za nini??

pato kubwa zaidi(per capita)unajua ni kitu gani na namna linavyopatikana??au ndio kukariri??per capita ni jumla ya pato la taifa kwa mwaka gawanya kwa idadi ya watu,embu nieleze uhalisiauko wapi hapo kwa mtu mmoja mmoja??tuliwafungia sababu kila mtu ana kwao,kama wana pesa si wanunue ardhi nchini kwao!!!kwanini tuwakaribishe waje kununua kwetu!!!

hakuna chuki,labda kama umeamua kuiita chuki ili kujenga kichaka cha kujibia hoja.
 
Huna mantiki ndugu yangu. Na pengine mzee wangu! Kwanza wanikosoa kwa dhana ya per capita, kana kwamba hii yatumiwa Kenya pekee. Tukisema per capita Tanzania inaifanya kuwa nchi ya pato la katikati ya chini…..hiyo wakubali! Lakini Kenya...nongwa, siyo?. Punguza jazba ndugu yangu, aliye mbele yuko mbele tu. Kenya yatupita sana. Na hayo mapungufu ambayo nayaita 'changamoto' nani hanayo? Litakalokukasirisha Zaidi ni habari hii kuwa kama tukiendelea na siasa hizi za kujipiga kifua na kutoa povu, tusichanganyike na dunia na kujifunza….miaka kumi kutoka sasa Kenya itakuwa zaidi yetu mara mbili (Wakati miaka ya 2005-8 tulikuwa twaikaribia, kiasi miaka miwili tulikuwa mbele yao kwa mapato!). Hawatatuzidi kwa uchumi tu, bali kisiasa, kijamii na.….furaha ya Maisha (joie de vivre). Wee utabakia kuchukia tu. Chuki namna hii dhidi ya mtu aliyetangulia kwa juhudi zake, ndiyo huwafanya wengine wakawa wachawi, chunga! Nasikitika utawala huu umefanya 'uzalendo' kuwa na tafsiri mbaya sana, ya kubeza, kuwatazama chini na hata kuchukia wengine. Maana hasa ya uzalendo ni kuipenda nchi yako kiasi cha kutaka kuiga yote mazuri ya nchi nyingine.
Hebu nikukasirishe Zaidi: Juzi Kenya imelipa deni lake loke kwa Uingereza! Tanzania kwa miaka minne iliyopita imekopa dola bilioni 9! Hiyo ni rekodi haijawahi kufanywa. Unajua na kusoma Kiingereza wewe? Basi soma ripoti za nje pia. Ndiyo maana aliyesema tumekosea 'elimu' hakukosea kabisaaaaa. Haki ya Mungu!
 
Tanzania na Kenya zilipata uhuru mapema miaka ya 1960s. Leo zinakaribia miaka 60 tangu zipate uhuru.

Nchi hizi mbili ni kama makaka wawili waliozaliwa tumbo moja ila kila mmoja kachukuwa njia tafauti katika kutafuta maisha. Na kwa mtazamo wa haraka Tanzania imefeli vibaya sana katika miaka yote 60 wakati Kenya angarau anapigia hatuwa kwenda mbele japo kuwa kwa mwendo wa ponda.

Tanzania imeshindwa hata kuinuka bado inapiga usigizi wa mtoto mchanga. sasa swali la kujiuliza Tanzania tumekosea wapi na kenya wamepatia wapi? Swali hili nitalijibu simple sana kenya pamoja na makosa mengi lakini kwenye upande wa elimu walipatia kwa kiwango kikubwa.

Mkenya wa darasa la saba anaweza kumzidi marifa mtanzania wa form six. Tanzania elimu yetu ni zero tangu enzi za Nyerere. Yaani elimu yetu sio ya kuelimisha bali ni ya kufaulu mitihani. Ndio maana tuna watu wenye PHD lakini matendo yao na fikira zao ni kama mtu ambaye hajaenda shule kabisa.

Kwa mfano ukiangalia PHD holders wa Tanzania wengi wanafanya kazi za kuteuliwa na watawala kama wa kuu wa mikowa au mawaziri. na ukiangalia performances zao ni ziro. Kwanini? Kwasababu wao kitu mhimu kwao ni cheo sio matokeo. Kwasababu tangu wakiwa mashuleni walifundishwa kufaulu mtihani mwisho wa muhula ndio mhim kuliko kuelewa.
Rubbish.
 
sikumbuki kama kunasehemu nimeandika per capita inapimwa kwa namna hiyo kenya peke yake.halafu sina jazba labda wewe ndugu yangu ndio sababu hata kuruka mistari unaona utachelewa.

siasa hizi hizi tutaenda nazo,maana lengo ni kuboresha maisha ya mtazania mmoja mmoja,sio kukuza GDP ambayo haiakisi maisha ya watu.

sijui kama nawewe ni mkenya au ni mtz,ila nikupe taarifa mbaya,deni la kenya limefikia 70% ya pato la taifa,na itakwenda kuwa kubwa zaidi mpaka rais aliyepo atkapoachia nchi.

nimekubali tokea awali,kenya wanatuzidi baadhi ya mambo,hii habari ya kusema wametuzidi mbaali ndio inanisukuma nikuulize wanatuzidi namna gani!!!
 
Utakufa huku ukiwa na mawazo duni, pole.
 
Sasa hapo umefanya la maana, kuuliza:
1- Wanatuzidi 'quality' elimu. Hii ni elimu bora, si bora elimu
2- Wanatuzidi ukubwa wa uchumi
3- Wanatuzidi uhuru na haki za raia
4- Wanatuzidi pato la mtu binafsi
5- Wanatuzidi kwa uenevu wa mtandao wa internet (Yaani watu wengi wana broadband internet nyumbani). Watanzania wengi internet wanaiona kwenye simu tu (hii ina maana kubwa kwa wanaojua maana!)
6- Wanatuzidi kwa 'quality of life' (kama wajua)
7- Katika Nyanja nyingine nyingi pia: stock market, exchange rate, mipango miji, barabara (ya 7 Afrika, Tanzania hata haimo katika 10 bora!) Kuna Library nyingi zaidi mjini Mombasa tu kuliko hata Tanzania nzima;
Lakini pengine twawazidi kwa baa nyingi, bendi nyingi za muziki naa….ndiyo, pengine Tanzania mtu aweza kukaa tu bila kufanya kazi na akapata hela na kula (kama alivyosema mmoja!).
Hii siyo kuiweka chini nchi yangu Tanzania, ila nasema tunayobidi tuige. Na kwa kweli, baadhi ya maendeleo ya Kenya ni kwa sababu za Kihistoria. Pia, Tanzania tuna mustkbali mzuri Zaidi (kama…) kuliko Kenya. Kikubwa Zaidi ninachokichukia ni watu kudanganywa-danganywa. Ukweli hapa Tanzania wanao tu wale wanaoweza kufuatilia vyombo vya nje tu au kusafiri. Juu ya deni la Kenya kuwa 70% ya GDP hiyo siyo neon ndungu. Deni la Japan ni 120% GDP na Marekani?
La muhimu ni vibrancy ya uchumi wako kuweza kurudisha. Mo anaweza kukopeshwa bilioni mbili za dola hivi sasa akitaka! Jee, utasema ana madeni Zaidi kuliko wewe uliekopa sh. laki tano?
Kwanza hao wanaokopesha wasingemkopesha hivyo kama hawajui wataweza kurudisha. Deni ni hatari Zaidi kwa Tanzania hivi sasa kuliko Kenya!
 
Tanzania na Kenya zilipata uhuru mapema miaka ya 1960s. Leo zinakaribia miaka 60 tangu zipate uhuru.

Nchi hizi mbili ni kama makaka wawili waliozaliwa tumbo moja ila kila mmoja kachukuwa njia tafauti katika kutafuta maisha. Na kwa mtazamo wa haraka Tanzania imefeli vibaya sana katika miaka yote 60 wakati Kenya angarau anapigia hatuwa kwenda mbele japo kuwa kwa mwendo wa ponda.

Tanzania imeshindwa hata kuinuka bado inapiga usigizi wa mtoto mchanga. sasa swali la kujiuliza Tanzania tumekosea wapi na kenya wamepatia wapi? Swali hili nitalijibu simple sana kenya pamoja na makosa mengi lakini kwenye upande wa elimu walipatia kwa kiwango kikubwa.

Mkenya wa darasa la saba anaweza kumzidi marifa mtanzania wa form six. Tanzania elimu yetu ni zero tangu enzi za Nyerere. Yaani elimu yetu sio ya kuelimisha bali ni ya kufaulu mitihani. Ndio maana tuna watu wenye PHD lakini matendo yao na fikira zao ni kama mtu ambaye hajaenda shule kabisa.

Kwa mfano ukiangalia PHD holders wa Tanzania wengi wanafanya kazi za kuteuliwa na watawala kama wa kuu wa mikowa au mawaziri. na ukiangalia performances zao ni ziro. Kwanini? Kwasababu wao kitu mhimu kwao ni cheo sio matokeo. Kwasababu tangu wakiwa mashuleni walifundishwa kufaulu mtihani mwisho wa muhula ndio mhim kuliko kuelewa.

Ungekuwa huna tembea hata nchi za watu,ya kwako ungeona unzuri.
Mimi nilikaa south africa lakini maisha ya kule japo kuwa ndo uchumi mkubwa lakini yamegawanyika kuwatajiri,kuwa wakati na kuwamaskini hata wabongo hana rahaa.

Kilichobaki kujua tunaweza kufika wapi ili kesho tusije kufanana na kile ambacho kipo kenya
Uzuri ardhi tunayo mpaka kitukuu kitapata
Bado fursa tanzania zipo sio mpaka mgeni aje azion
Ukilala nje bongo yani hata dini itakushangaa wakati nyumba za kulala kujitegemea zipo hata ya tope ni yako lakini unaishi vzuri.sio wale wenye mabanda ya kuku

Kulalamika sana wakati ujui jirani yako yupi vpi
 
Hii ina nusu ukweli nusu…. Watanzania wengi wanasafiri nje bila ya kuwa na tools za Maisha ya huko. Wao ni 'twenzetu Sauzi tu' mtu hata lugha ya kuombea kazi hana. Na kazi gani basi? Watanzania wengi nje hawana kazi za maana kwa sababu moja tu 'elimu'. Tena la ajabu, hata wakifika huko na wanajua fika wanahitajia kusoma…..wachache wanasoma! Huwezi kulinganisha Maisha ya Wazimbabwe, Wakenya, Waganda, Wamauritius, Wazambia……....na Watanzania nje. Jibu liko wazi, lakini Watanzania wengi wamezoea kulaumu na kulalamika!
 
Back
Top Bottom