Tanzania tulikosea wapi na Kenya walipatia wapi?

Ikulumaliyawananch

JF-Expert Member
Mar 14, 2018
339
533
Tanzania na Kenya zilipata uhuru mapema miaka ya 1960s. Leo zinakaribia miaka 60 tangu zipate uhuru.

Nchi hizi mbili ni kama makaka wawili waliozaliwa tumbo moja ila kila mmoja kachukuwa njia tafauti katika kutafuta maisha. Na kwa mtazamo wa haraka Tanzania imefeli vibaya sana katika miaka yote 60 wakati Kenya angarau anapigia hatuwa kwenda mbele japo kuwa kwa mwendo wa ponda.

Tanzania imeshindwa hata kuinuka bado inapiga usigizi wa mtoto mchanga. sasa swali la kujiuliza Tanzania tumekosea wapi na kenya wamepatia wapi? Swali hili nitalijibu simple sana kenya pamoja na makosa mengi lakini kwenye upande wa elimu walipatia kwa kiwango kikubwa.

Mkenya wa darasa la saba anaweza kumzidi marifa Mtanzania wa form six. Tanzania elimu yetu ni zero tangu enzi za Nyerere. Yaani elimu yetu sio ya kuelimisha bali ni ya kufaulu mitihani. Ndio maana tuna watu wenye PHD lakini matendo yao na fikira zao ni kama mtu ambaye hajaenda shule kabisa.

Kwa mfano ukiangalia PHD holders wa Tanzania wengi wanafanya kazi za kuteuliwa na watawala kama wa kuu wa mikowa au mawaziri. na ukiangalia performances zao ni ziro. Kwanini? Kwasababu wao kitu mhimu kwao ni cheo sio matokeo. Kwasababu tangu wakiwa mashuleni walifundishwa kufaulu mtihani mwisho wa muhula ndio mhim kuliko kuelewa.
 
Tanzania tuna wapenda madaraka CCM na sio wapenda maendeleo ni kuangalia matumbo yao tu

Wako tayari kuua kwa yeyote anayetaka kuhatarisha kula yao na sio maendeleo ya watanzania.

CCM watakapoondoka madarakani kwa njia yeyote ndipo Tanzania tutapata mafanikio makubwa kuwahi kutokea.

Tuondoe nidhamu ya woga CCM haitufai pamoja na washirika wake wote.
 
Inabidi pia ueleze watu Kenya anapatia kwenye nini.

Kenya inaongoza kwa tatizo la ajira ukanda huu
Kenya inaongoza kwa rushwa mbaya ukanda huu
Kenya ina raia wenye maisha duni zaidi ukanda huu
Kenya gharama za maisha ziko juu zaidi, mbali ya kwamba wana uchumi mkubwa wakiwa wachache zaidi yetu
Kenya ina siasa chafu, sisi zina kasoro moja ndogo tu
Ukabila na ukosefu wa umoja wa kitaifa ni tatizo sugu Kenya

Kwa kukutaarifu tu, wana mabaya mengi zaidi kuliko mazuri machache waliyotuzidi, ambayo hata hivyo yanakwenda yakibadirishwa kuwazidi siku si nyingi.

Msiishi kwa stori za mitandaoni, tembeeni.
 
Tanzania hatujakosea popote, kesi yetu ni sawa na China vs South Korea. Maendeleo ya china ni ya juhudi za Wachina bila msaada wa ushirikiano na nchi nyingine ila wa Korea ni vibaraka wa mmarekani.

Kenya ni changudoa wa Marekani, Marekani ikianguka hakutakua na nchi ya kenya. Wanategemea stability ya Marekani. Sisi tunavyokwenda hakuna cha kututeteresha.

Ukiona mafuta Kenya ni bei ndogo jua kuna mkono wa USA, hata hivyo kwa kuangalia kenya wangapi wanaweza kuafford kutumia hayo mafuta ya bei ndogo? Sisi tumejenga stable state.
 
Tanzania tuna wapenda madaraka CCM na sio wapenda maendeleo ni kuangalia matumbo yao tu..
Unajua Moi alikaa madarakani muda gani? Unajua Wakenya wangapi wanauliwa hadharani na kamera zinashuhudia? Acha ujuaji kijana, Kenya sio nchi ni genge kati kati ya nchi. BBC leo wametoa uchunguzi wao wa namna watoto wanauzwa Nairobi kwa shilingi laki 7. Tuwe na shukurani.
 
Wakenya wanajitambua sana, likija suala la kupigania haki zao wako tayari kupoteza hata uhai wao ili wapate wanachotaka, ila kwetu sisi ni tofauti, tunataka tukae nyumbani tuletewe mabadiliko na wengine, hapo ndipo tunapofeli.

Katiba ndio msingi wa maendeleo, wakenya waliipigania Katiba yao ya sasa mpaka wengine kupoteza uhai wao, atleast leo wanafurahia matunda ya demokrasia.

Ukisema sababu ya elimu nayo naitilia shaka, mbona elimu yetu inaonekana ni bora zaidi ya Uganda lakini waganda nawaona wakipigania haki zao kwa vitendo, sio wanaume tu hata wanawake wote wanaingia barabarani kumtaka mtu wao aachiwe na polisi, sisi hatuwezi, watanzania tumezubaa sana.
 
Unajua Moi alikaa madarakani muda gani? Unajua wakenya wangapi wanauliwa hadharani na kamera zinashuhudia? Acha ujuaji kijana, Kenya sio nchi ni genge kati kati ya nchi. BBC leo wametoa uchunguzi wao wa namna watoto wanauzwa Nairobi kwa shilingi laki 7. Tuwe na shukurani.
Tunakuwa na shukrani gani kwa nchi ambayo imejaaa kila kitu but watu ni maskini utafikiri wameingia leo duniani? Kwanza ni ujinga na upumbavu kujilinganisha na Kenya ambapo tunawazidisha mara mia kwenye resources. Sisi watanzania viongozi wetu hawana akili, wanafikiri kwa kutumia matumbo.
 
Tunakuwa na shukrani gani kwa nchi ambayo imejaaa kila kitu but watu ni maskini utafikiri wameingia leo duniani? Kwanza ni ujinga na upumbavu kujilinganisha na Kenya ambapo tunawazidisha mara mia kwenye resources ,Sisi watanzania viongozi wetu hawana akili, wanafikiri kwa kutumia matumbo.
Sisi tunategemea mawazo ya mtu mmoja tu.
 
Mbona mimi niliwazidi hao Wakenya unaowasifia kwa kiingereza, kujieleza, na hata kupata alama nyingi nilipokuwa nasoma nao ESAMI - Arusha. Acha uongo.
 
Wakenya wanajitambua sana, likija suala la kupigania haki zao wako tayari kupoteza hata uhai wao ili wapate wanachotaka, ila kwetu sisi ni tofauti, tunataka tukae nyumbani tuletewe mabadiliko na wengine, hapo ndipo tunapofeli.

Katiba ndio msingi wa maendeleo, wakenya waliipigania Katiba yao ya sasa mpaka wengine kupoteza uhai wao, atleast leo wanafurahia matunda ya demokrasia.

Nadhani hata Uganda siku sio nyingi watatuacha tubaki na ujinga wetu, nawaona wakipigania haki zao kwa vitendo, sio wanaume tu hata wanawake wote wanaingia barabarani kumtaka mtu wao aachiwe na polisi, sisi hatuwezi.
Hivi wewe unaijua kenya au unasikia mambo ya mtandaoni
 
Wakenya wanajitambua sana, likija suala la kupigania haki zao wako tayari kupoteza hata uhai wao ili wapate wanachotaka, ila kwetu sisi ni tofauti, tunataka tukae nyumbani tuletewe mabadiliko na wengine, hapo ndipo tunapofeli.
Uongo Wakenya wengi hawana ardhi
 
  • Thanks
Reactions: B51
Tanzania hatutaki kupitianjia
Tanzania hatutaki kupitianjia ya Kenya waliopitia yaani kuifikia demokrasia kwa njia vurugu hapana tunataka kuifikia demokrasia kwa njia salama je njia salama hiyo ndio njia gani?
 
True kuna RC mmoja eti amesoma lkn matamko yake ayalingani na mtu aliyewahi pita shule. Ipo tofauti Kati ya kusoma na kuwa civilized educated.
 
Back
Top Bottom