Tanzania tulikosea wapi na Kenya walipatia wapi?

Tanzania tulikosea wapi na Kenya walipatia wapi?

Kuna sababu nyingi zilizoleta tofauti kubwa katika nyanza nyingi kati ya Tanzania na Kenya iliyopata Uhuru miaka miwili baada ya sisi. Sababu kubwa kabisa ni elimu iliyoharibiwa toka Awamu ya Kwanza muda mfupi tu baada ya Uhuru katika juhudi ya kuleta elimu nzuri ya Kitanganyika tofauti na ile ya Kikoloni. Elimu hiyo mpya ilikuwa na makosa mengi yaliyoadhiri ubora lakini kosa kubwa kabisa ilikuwa kuondoa kabisa Darasa la Nane ambalo lilikuwa la mwisho Shule za Msingi. Hii ikawa sawa na kubomoa msingi wa nyumba ukaendelea kujenga nyumba ukitegemea itakuwa imara ya kudumu. Kenya nao waliiga mtindo huo lakini waligundua kosa hilo mapema na kurekabisha miaka michache tu baadaye na kurudisha Darasa la Nane hadi leo badala yake waliondoa kabisa Form Six. Wakenya wakaja na mfumo wa 8-4-4 ikiwa na maana ya miaka 8 Msingi, miaka 4 Sekondari na miaka 4 Chuo Kikuu digrii ya kwanza. Hii ina maana Form Five ilihamishiwa Chuo Kikuu kumuandaa mwanafunzi kuingia Chuoni. Huu ndo mfumo uliokuwapo Chuo Kikuu cha Makerere kabla ya Uhuru wa nchi zote tatu za Afrika Mashariki. Zambia wao walifutilia mbali Form Five na Six wakabaki na Form Four tu na wanafunzi wao wanapokelewa vyuo vyote duniani wa kwetu wa Form Six wakikataliwa. Bahati mbaya sana toka Awamu ya Kwanza kila Waziri anayeteuliwa kuongoza Wizara ya Elimu alikuja na mbinu zake za kuboresha elimu lakini amekuwa akimaliza kwa kuharibu zaidi. Matokeo yake sasa hivi kila kiongozi Serikalini, Bungeni na Mahakamani ana PhD ambayo haijulikani ni ya Chuo gani wala fani gani ikileta hisia tofautitofauti juu ya elimu ya viongozi wetu.
Mkuu,

Umeeleza uzuri kwa hiyo ni muda muafaka sasa wenye dhamana na mamlaka ya unongozi wa nchi wawasikilize wadau namna bora ya kuboresha utoaji elimu yenye tija kwa vija ili malalamiko ya kukosa ajira yapungue kwa kuwezeshwa kuwa na maarifa yanayomwongoza mtu kupambana na changamoto za kimaisha.

Mfano, vyuo vya ufundi vya enzi hizo kama Dar Tech, Arusha, Moshi Tech nk walikuwa na ujuzu wa hali ya juu sana kuliko sasa pampja na kwamba vyuo hivyo vimepandishwa hadhi kutoa mafunzo ya shahada!!!

Mwarobaini ni kutoa mafunzo bunifu na milikishi kwenye ubungo ambayo mhitimu wa ngazi yoyote aweze kuanzisha shughuli za kiuchumi kwa kuzingatia mahitaji ya soko la ndani na nje yaliyoboreshwa kwa teknolojia ya kisasa. Serikali itoe mikopo yenye riba ya asilimia 6% kwa shughuli za ufundi, biashara, kilimo, mazao ya maliasili kwa mjibu wa sheria. Matumizi ya lugha fasaha ya Kiswahili, Kiingereza, Kichina, Kifaransa nk. Kujenga uelewa mpana na kujiamini kutokana na ufahamu wa kinadhaniria unapohamishiwa kitafsiri kwa vitendo kwa matokeo chanya. Kuajiri walimu waliofaulu vizuri sekondari na chuo badala ya hao wa madaraja ya tatu na nne-haifai. Wahadhiri wa chuo kikuu ni sharti utaratibu wa zamani urejeshwe kwa ni lazima awe amepata daraja bora la kwanza badala ya sasa hadi daraja la pili wanachukuliwa. Serikali itoe elimu bila malipo ya ada na michango yenye usumbufu kwa wazazi kuanzia kidato cha kwanza hadi cha sita. Wanafunzi wote wanaofaulu na kuchaguliwa kujiunga vyuo vikuu katika fani yoyote waoewe mkopo kwa mrejesho wa riba ndogo baada ya kufuzu, kuajiriwa au kujiari kwa kipato cha kueleweka nk.
 
Sasa hapo umefanya la maana, kuuliza:
1- Wanatuzidi 'quality' elimu. Hii ni elimu bora, si bora elimu
2- Wanatuzidi ukubwa wa uchumi
3- Wanatuzidi uhuru na haki za raia
4- Wanatuzidi pato la mtu binafsi
5- Wanatuzidi kwa uenevu wa mtandao wa internet (Yaani watu wengi wana broadband internet nyumbani). Watanzania wengi internet wanaiona kwenye simu tu (hii ina maana kubwa kwa wanaojua maana!)
6- Wanatuzidi kwa 'quality of life' (kama wajua)
7- Katika Nyanja nyingine nyingi pia: stock market, exchange rate, mipango miji, barabara (ya 7 Afrika, Tanzania hata haimo katika 10 bora!) Kuna Library nyingi zaidi mjini Mombasa tu kuliko hata Tanzania nzima;
Lakini pengine twawazidi kwa baa nyingi, bendi nyingi za muziki naa….ndiyo, pengine Tanzania mtu aweza kukaa tu bila kufanya kazi na akapata hela na kula (kama alivyosema mmoja!).
Hii siyo kuiweka chini nchi yangu Tanzania, ila nasema tunayobidi tuige. Na kwa kweli, baadhi ya maendeleo ya Kenya ni kwa sababu za Kihistoria. Pia, Tanzania tuna mustkbali mzuri Zaidi (kama…) kuliko Kenya. Kikubwa Zaidi ninachokichukia ni watu kudanganywa-danganywa. Ukweli hapa Tanzania wanao tu wale wanaoweza kufuatilia vyombo vya nje tu au kusafiri. Juu ya deni la Kenya kuwa 70% ya GDP hiyo siyo neon ndungu. Deni la Japan ni 120% GDP na Marekani?
La muhimu ni vibrancy ya uchumi wako kuweza kurudisha. Mo anaweza kukopeshwa bilioni mbili za dola hivi sasa akitaka! Jee, utasema ana madeni Zaidi kuliko wewe uliekopa sh. laki tano?
Kwanza hao wanaokopesha wasingemkopesha hivyo kama hawajui wataweza kurudisha. Deni ni hatari Zaidi kwa Tanzania hivi sasa kuliko Kenya!

1,wanatuzidi quality ya elimu benchmark ikiwa wapi mkuu???maana ndio hawa wanaangusha madaraja na maghorofa kwao kila mara.

2,ukubwa wa uchumi sina neno nakubali-swali langu la msingi uchumi ni kitu gani kama mwananchi anakufa njaa!!!uchumi mkubwa unakuwa umetoa mchango gani kuzuia hilo???

3,uhuru wa haki za raia-kwenye kufanya jambo gani ndipo sample imechukuliwa??maamndamano au nini??katafute ukanda huu ni nchi gani iko kwenye hali mbaya riport police brutality,kisha uniambie ni uhuru upi unazungumzia.

4,pato la mtu binafsi ndio hapo ilipo per capita,sihitaji kukuelekeza tena ni kitu gani.

5,broadband hivi ni vitu vya ziada,muhimu ni internet coverage eneo inapopatikana hizo ni mikakati za kibiashara za watu.so kama kenya wana coverage kubwa zaidi ya mtandao sawa,ndio maana walisema wako na user 48ml over 49mln kenya pop.

6,quality ya life sijui ni ipi unazungumzia,maana $1mln wearth individuali tumewaacha mbali sana.

7,hapa kwenye barabara,sina shaka wametuacha ila ni kidogo sana,na ndio nikasema ni kiongoni mwa sekta ambazo soo statistics zitabadirika.

kudanganywa ambako wengi wanadanganywa ndio huko tunakokataa kusema kenya imeiacha mbaali sana tz!!!huu ni upuuzi ambao hauisaidii kenya.

yote kwa yote kenya sio japan,ukitaka kujua hayo angalia rate ya urejeshaji mikopo ndio utaelewa.
 
Duh! Wajua miye sijadili kwa ku win points. Hivyo sijadili na mtu anayesema jua ni mwezi. Kwa kukusaidia, jaribu kwenda Kenya, popote pale hata mji wa mpakani halafu ufanye comparison. Ukifanikiwa kwenda ndani Zaidi, huko utakutana na maelfu, kama siyo mamilioni, ya Watanzania wakifanya kazi ndogo ndogo, wengi za nyumbani. Sijui hiyo itakueleza nini, au pia utasema kuna maelfu ya Wakenya wakifanya kazi za ndani Tanzania!
 
Wakati sisi Tanzania kwenye miaka ya 70 na 80 tunasaidia nchi za kusini ya Afrika kujitawala,wakenya walikunja mikono na kuendelea kuwakumbatia mabeberu, matokeo yake karibu nusu ya ardhi nzuri ya Kenya ni mali ya watu wachache sana. Hivyo Tanzania hakuna tulipokosea na wala hao unaowasifia hawatuzidi chochote.
 
Wakenya wanajitambua sana, likija suala la kupigania haki zao wako tayari kupoteza hata uhai wao ili wapate wanachotaka, ila kwetu sisi ni tofauti, tunataka tukae nyumbani tuletewe mabadiliko na wengine, hapo ndipo tunapofeli.

Katiba ndio msingi wa maendeleo, wakenya waliipigania Katiba yao ya sasa mpaka wengine kupoteza uhai wao, atleast leo wanafurahia matunda ya demokrasia.

Ukisema sababu ya elimu nayo naitilia shaka, mbona elimu yetu inaonekana ni bora zaidi ya Uganda lakini waganda nawaona wakipigania haki zao kwa vitendo, sio wanaume tu hata wanawake wote wanaingia barabarani kumtaka mtu wao aachiwe na polisi, sisi hatuwezi, watanzania tumezubaa sana.
Wangekuwa wanajua kupigania haki zao wangehakikisha kila mkenya ana ardhi badala yake ardhi imehodhiwa na kundi dogo la watawala na rafiki zao. Hatudanganyiki.
 
Tanzania na Kenya zilipata uhuru mapema miaka ya 1960s. Leo zinakaribia miaka 60 tangu zipate uhuru.

Nchi hizi mbili ni kama makaka wawili waliozaliwa tumbo moja ila kila mmoja kachukuwa njia tafauti katika kutafuta maisha. Na kwa mtazamo wa haraka Tanzania imefeli vibaya sana katika miaka yote 60 wakati Kenya angarau anapigia hatuwa kwenda mbele japo kuwa kwa mwendo wa ponda.

Tanzania imeshindwa hata kuinuka bado inapiga usigizi wa mtoto mchanga. sasa swali la kujiuliza Tanzania tumekosea wapi na kenya wamepatia wapi? Swali hili nitalijibu simple sana kenya pamoja na makosa mengi lakini kwenye upande wa elimu walipatia kwa kiwango kikubwa.

Mkenya wa darasa la saba anaweza kumzidi marifa Mtanzania wa form six. Tanzania elimu yetu ni zero tangu enzi za Nyerere. Yaani elimu yetu sio ya kuelimisha bali ni ya kufaulu mitihani. Ndio maana tuna watu wenye PHD lakini matendo yao na fikira zao ni kama mtu ambaye hajaenda shule kabisa.

Kwa mfano ukiangalia PHD holders wa Tanzania wengi wanafanya kazi za kuteuliwa na watawala kama wa kuu wa mikowa au mawaziri. na ukiangalia performances zao ni ziro. Kwanini? Kwasababu wao kitu mhimu kwao ni cheo sio matokeo. Kwasababu tangu wakiwa mashuleni walifundishwa kufaulu mtihani mwisho wa muhula ndio mhim kuliko kuelewa.

Please give us the research report on what you have written. Do not take things from abstract, put your empirical evidence to substantiate it.
 
Duh! Wajua miye sijadili kwa ku win points. Hivyo sijadili na mtu anayesema jua ni mwezi. Kwa kukusaidia, jaribu kwenda Kenya, popote pale hata mji wa mpakani halafu ufanye comparison. Ukifanikiwa kwenda ndani Zaidi, huko utakutana na maelfu, kama siyo mamilioni, ya Watanzania wakifanya kazi ndogo ndogo, wengi za nyumbani. Sijui hiyo itakueleza nini, au pia utasema kuna maelfu ya Wakenya wakifanya kazi za ndani Tanzania!

angalia nini hiki umeandika mkuu???

kazi za ndani aje kufanya mkenya tz kwa kibari gani??
 
Bunge la Kenya lingekuwa na meno kila mkenya angekuwa ardhi. Inawezakana hata hiyo Kenya hujafika unaropoka tu.
Kenya katiba yao inawasaidia sn mahakama zipo huru na bunge lipo huru na wakati huku ni mashina ya CCM
 
Tatizo hajui Kenya ilikuwa British East Africa na Tanganyika ilikuwa Protectorate baada ya mjerumani kushindwa kwenye vita ya pili vya dunia. Wazungu waliwekeza sana Kenya kabla ya uhuru kwa sababu ilikuwa ni nchi yao iliyokuwa Afrika Mashariki na hawakutegemea kwamba watakuja kuondoka wakati Tanganyika iliwekwa chini ya waingereza ili ikisha kuwa na uwezo ijitawale. Mtoa post hata historia tu ya primary hajui.
Ulivyo anza mada yako inaonyesha kwamba huijui Tanzania (Tanganyika) kabla ya uhuru na huijui Kenya kabla ya uhuru! Pia hujui Tanganyika na Kenya zilivyopata uhuru. Ukiyajua hayo, hutalinganisha Tanzania na Kenya mpaka unakufa!
 
angalia nini hiki umeandika mkuu???

kazi za ndani aje kufanya mkenya tz kwa kibari gani??
Ni kibali, si kibari. Ki-Bari ni lugha inayzungumzwa Sudan ya Kusini. Watu wengi siku hizi wanakosea Kiswahili na kutoa maana tofauti, wakiwemo viongozi! 'Elimu'!
Kwa hilo unalosema, inakuonesha wazi kuwa Kenya ni nchi iliyo open, inayojiamini, siyo kama sisi woga woga na 'upolisi' hadi kazi za ndani pia lazima kibali!
Naendelea na uzi huu nikiamini tu kuwa angalau una kiasi kizuri cha elimu, la sivyo si rahisi kufahamu nasema nini.
 
Shida ni Kiingereza, sidhani kama kuna kingine
Tatizo Siyo kingereza tu ingawa lugha ikiwa tatizo ina maana uelewa wa kile unachofundishwa utakuwa midogo pia.Malawi na Zambia kingereza Chao kiko vizuri kuliko Kenya. Ila ukiwalinganisha na Wakenya bado kuna tofauti.
 
Tatizo hajui Kenya ilikuwa British East Africa na Tanganyika ilikuwa Protectorate baada ya mjerumani kushindwa kwenye vita ya pili vya dunia. Wazungu waliwekeza sana Kenya kabla ya uhuru kwa sababu ilikuwa ni nchi yao iliyokuwa Afrika Mashariki na hawakutegemea kwamba watakuja kuondoka wakati Tanganyika iliwekwa chini ya waingereza ili ikisha kuwa na uwezo ijitawale. Mtoa post hata historia tu ya primary hajui.
Mkuu, Wazungu walijua kuna Siku wataondoka tofauti na CCM wana fikiri watatatawala milele. Tofauti ni kwamba hawakutegemea kama wangeondoka mapema vile. Second World War was a game changer.
 
Unajua Moi alikaa madarakani muda gani? Unajua Wakenya wangapi wanauliwa hadharani na kamera zinashuhudia? Acha ujuaji kijana, Kenya sio nchi ni genge kati kati ya nchi. BBC leo wametoa uchunguzi wao wa namna watoto wanauzwa Nairobi kwa shilingi laki 7. Tuwe na shukurani.
Shukrani 50 yrs for nothing bro. kwanza tuache story tuanzie hapa . ulishawahi fika kenya au kuishi kenya hata kama ni siku 2
 
Maendeleo yeyote ya mtu mmoja mmoja au kundi yanategemea akili na akili , inajengwa na msingi mzuri wa elimu ...

harambee Kenya
 
Ni kibali, si kibari. Ki-Bari ni lugha inayzungumzwa Sudan ya Kusini. Watu wengi siku hizi wanakosea Kiswahili na kutoa maana tofauti, wakiwemo viongozi! 'Elimu'!
Kwa hilo unalosema, inakuonesha wazi kuwa Kenya ni nchi iliyo open, inayojiamini, siyo kama sisi woga woga na 'upolisi' hadi kazi za ndani pia lazima kibali!
Naendelea na uzi huu nikiamini tu kuwa angalau una kiasi kizuri cha elimu, la sivyo si rahisi kufahamu nasema nini.

vyema mwalimu,ila unajipa kazi nyingi utachoka mapema.

kenya ni nchi isiyo na maisha ndugu yangu,ndio sababu mnatamani kuingia na nachi zingine hasa tanzania muishi huko ni vile haiwezekani.

ingekuwa elimu nzuri nayo inafundisha matamshi na maandishi ya maneno hoja yako ingekuwa na mashiko,bahati mbaya utumbo wote unaishia elimu ya msingi.hivyo doctor na anayejua kusoma wote wanaweza kuwa na tatizo moja kwenye lugha.

labda doctor wa kiswahili.
 
Maendeleo yeyote ya mtu mmoja mmoja au kundi yanategemea akili na akili , inajengwa na msingi mzuri wa elimu ...

harambee Kenya

akili,elimu.

ni vitu visivyo na uhusiano kabisa.
ndio sababu watu wanahoji mtu wa kwanza kupata degree alipewa na nani???
 
Tanzania na Kenya zilipata uhuru mapema miaka ya 1960s. Leo zinakaribia miaka 60 tangu zipate uhuru.

Nchi hizi mbili ni kama makaka wawili waliozaliwa tumbo moja ila kila mmoja kachukuwa njia tafauti katika kutafuta maisha. Na kwa mtazamo wa haraka Tanzania imefeli vibaya sana katika miaka yote 60 wakati Kenya angarau anapigia hatuwa kwenda mbele japo kuwa kwa mwendo wa ponda.

Tanzania imeshindwa hata kuinuka bado inapiga usigizi wa mtoto mchanga. sasa swali la kujiuliza Tanzania tumekosea wapi na kenya wamepatia wapi? Swali hili nitalijibu simple sana kenya pamoja na makosa mengi lakini kwenye upande wa elimu walipatia kwa kiwango kikubwa.

Mkenya wa darasa la saba anaweza kumzidi marifa Mtanzania wa form six. Tanzania elimu yetu ni zero tangu enzi za Nyerere. Yaani elimu yetu sio ya kuelimisha bali ni ya kufaulu mitihani. Ndio maana tuna watu wenye PHD lakini matendo yao na fikira zao ni kama mtu ambaye hajaenda shule kabisa.

Kwa mfano ukiangalia PHD holders wa Tanzania wengi wanafanya kazi za kuteuliwa na watawala kama wa kuu wa mikowa au mawaziri. na ukiangalia performances zao ni ziro. Kwanini? Kwasababu wao kitu mhimu kwao ni cheo sio matokeo. Kwasababu tangu wakiwa mashuleni walifundishwa kufaulu mtihani mwisho wa muhula ndio mhim kuliko kuelewa.

Slums zile za kibera zimetokana na nini? Na sifa unazotoa?

Haujafika kenya bado, jitahidi basi usiwe na mahaba usiyoyajua

Zero yako uliipatia shule gani?😂😂
 
Tanzania na Kenya zilipata uhuru mapema miaka ya 1960s. Leo zinakaribia miaka 60 tangu zipate uhuru.

Nchi hizi mbili ni kama makaka wawili waliozaliwa tumbo moja ila kila mmoja kachukuwa njia tafauti katika kutafuta maisha. Na kwa mtazamo wa haraka Tanzania imefeli vibaya sana katika miaka yote 60 wakati Kenya angarau anapigia hatuwa kwenda mbele japo kuwa kwa mwendo wa ponda.

Tanzania imeshindwa hata kuinuka bado inapiga usigizi wa mtoto mchanga. sasa swali la kujiuliza Tanzania tumekosea wapi na kenya wamepatia wapi? Swali hili nitalijibu simple sana kenya pamoja na makosa mengi lakini kwenye upande wa elimu walipatia kwa kiwango kikubwa.

Mkenya wa darasa la saba anaweza kumzidi marifa Mtanzania wa form six. Tanzania elimu yetu ni zero tangu enzi za Nyerere. Yaani elimu yetu sio ya kuelimisha bali ni ya kufaulu mitihani. Ndio maana tuna watu wenye PHD lakini matendo yao na fikira zao ni kama mtu ambaye hajaenda shule kabisa.

Kwa mfano ukiangalia PHD holders wa Tanzania wengi wanafanya kazi za kuteuliwa na watawala kama wa kuu wa mikowa au mawaziri. na ukiangalia performances zao ni ziro. Kwanini? Kwasababu wao kitu mhimu kwao ni cheo sio matokeo. Kwasababu tangu wakiwa mashuleni walifundishwa kufaulu mtihani mwisho wa muhula ndio mhim kuliko kuelewa.
Daah hiyo para ya mwisho umemaliza kila kitu mkuu...
 
Back
Top Bottom