Tanzania itaendelea kukuza na kuimarisha zaidi ushirikiano na Kenya

Ojuolegbha

JF-Expert Member
Sep 6, 2020
741
479
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Hussein Ali Mwinyi amesema Serikali ya Tanzania itaendelea kushirikiana bega kwa bega na Kenya katika kukuza na kuimarisha zaidi uhusiano na ushirikiano wa kindugu na kihistoria kwa manufaa ya nchi zote mbili.

Rais Dk. Mwinyi amesema hayo wakati akihutubia katika sherehe za Maadhimisho ya Miaka 60 ya Uhuru wa Kenya (Jamhuri Day) akimwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan uwanja wa Uhuru Gardens Nairobi, Kenya Tarehe: 12 Desemba, 2023.

Aidha, Rais Dk. Mwinyi ameeleza kuwa uhusiano uliopo wa Kenya na Tanzania una manufaa makubwa kiuchumi hususan katika nyanja ya uwekezaji na biashara ambao unakadiriwa kufikia takribani Trilioni 1.8 za Tanzania mwaka 2022.

Maadhimisho hayo yameongozwa na Rais wa Kenya Mhe. Dk. William Ruto ambayo yaliyohudhuriwa na Viongozi mbalimbali akiwemo Rais wa Ethiopia, Makamu wa Rais wa Burundi, Naibu Waziri Mkuu wa Uganda.

Baadae, Rais Dk. Mwinyi ameshiriki katika dhifa ya chakula cha mchana iliyoandaliwa na mwenyeji wake Rais Dkt. Ruto katika viwanja vya Ikulu, Nairobi.

IMG-20231213-WA0003.jpg
IMG-20231213-WA0005.jpg
IMG-20231213-WA0006.jpg
IMG-20231213-WA0015.jpg
IMG-20231213-WA0016.jpg
IMG-20231213-WA0014.jpg
IMG-20231213-WA0007.jpg
IMG-20231213-WA0008.jpg
IMG-20231213-WA0011.jpg
IMG-20231213-WA0010.jpg
IMG-20231213-WA0004.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom