Tanzania to go Wireless

Tatizo huyo atakayeingia...si tunaona STAMICO walikuwa wanaikalia hazina, sasa "wachimbaji" wameingia Mabuzwagi kila kona.
 
tatizo la umeme wa Tanzania ni la kukosa maono tu na uongozi. Leo hii sisi tungeweza kusupply hata asilimia 90 ya wananchi wetu kwa umeme, uwe wa maji, upepo, au jua! Tatizo bado tunafuata traditional models za kusubiri bwawa, then kusambaza nyaya, then watu wapate umeme.

Viongozi wetu hawana maoni kweli...ndio maana mtandao naupa nafasi kubwa sana ya kuleta maendeleo. Mfano aliyekuwa Mwl Mkuu wa Shauritanga Sec kwa miaka ya nyuma (jina kwapani) leo hii anatumia umeme wa asili kutokana na kinyesi cha ng'ombe wake pale Rombo. Sasa hebu fikiria ujuzi huo ungekuwa unapatikana kwenye mtandao na kijana wa kidato cha nne (aliyekuja mjini kumtembelea ndugu yake akapata nafasi ya kusoma kwenye mtandao) kisha akaupeleka kijijini kwake si tayari ameshakomboka huyo. Tena sio peke yake maana wengine nao wataiga, kwa namna moja au nyingine ujuzi huo na faida zake unasambaa kwa jamii nzima.
 
msiwe na wasi wasi vijana WIMAX ni new technology & very fast na haina complications nyingi kuitandaza ni minara tuu kama cell phone hakuna waya hapo wajomba wa kuchimbiwa mahandaki,mnaotaka kujifunza zaidi just google it utaelewa ninachoongea...wimax ni fungakazi inaweza kufungwa mji mzima wa Dar kwa siku moja tuu wote mkao mtandaoni.
 


....Zaidi, nakubaliana na wewe kuwa wananchi wengi zaidi wakimudu basi faida halisi ndio inaonekana mapema zaidi. Isipokuwa tu kwa sasa walet technologia hizo gharama zitajirekebisha huko mbele ya safari. Binafsi nina pricipal moja kuwa ni bora huduma iwepo nishindwe kulipia kuliko niweze kulipia halafu huduma isiwepo kabisa.

Iwapo watatimiza ahadi zao huu ni muendelezo mzuri kabisa wa hao ambao wameshatangulia kama Vodacom na Zantel kwa technologia tofauti kidogo...wakati huo huo Kenya very soon wanaanza project yao ya Fiber Optic kutoka Emirates hadi Mombasa. Pengine miaka 5 ijayo TTCL au wengine wakichangamka tutakuwa tunabofya bofya hizi keyboards na kubadili website pages kwa spidi ya ajabu.

Mhe. YeboYebo

Naafiki mawazo yako kabisaaa ...hasa hiyo sehemu ya kubofya hizi keyboards na kubadili website pages kwa spidi ya ajabu . Na mimi naongezea kuwa hata mpira wa Simba na Yanga (siyo Yanga na Simba - maaanake kuna tofauti kuubwa sana) tutaweza kuaangalia online ... hapo patakuwa patamu mzee mwenzangu!!!

Inshallah siku itafika ... I have a dream!!

ZalendoHalisa
 
Sana sana lililobaki ni kujua kusoma na kuandika basi - umeme watachoma gesi kama madimbwi yamekauka. Mchuchuma nayo inabidi izalishe haraka. Jua ni masaa 12, na sio chini ya siku 200 kwa mwaka.

In short, hakuna lisilowezekana katika miaka mitano ijayo kuwa na mtandao wa kuaminika kabisa nchi nzima.

Haya ndio yatakayokuwa mavuno ya Kikwete ya kujivunia haraka haraka kama anataka.
 
..acheni umbeya hapo juu,JK has nothing to do na hii kitu,watu wanaweka hard work,utaalam,pesa zao kwenye line kufanya Biashara na sio serikali ambayo ukiangalia sana ni kikwazo hapo kutokana na sera mbovu za mawasiliano...sasa hapo mavuno ya kikwete yametoka wapi? mnanikumbusha documentary moja niliiona National Geographic ya North Korea,watu vipofu wametibiwa na madaktari wa kutoka US basi walivyopona wakaanza kupiga magoti wanalia eti wanamshukuru The Great Leader...what a bunch of bafoon!
 
Mzee Mwanakijiji,

Baada ya kusoma ujumbe huu nimejaribu sana kuuliza watu kuhusu kampuni hii ambayo kusema kweli pamoja na kuwa nimeishi katika mji huu kwa miaka 15 sijawahi kuisikia wala kusikia kampuni inayo provide hizi services ndani ya Mji huu ama Canada isipokuwa ni watengenezaji/Waagizaji wa vifaa vya kurushia mawasiliano (Broadband wireless infrastructure products) kama vile GE ktk maswala ya electrinics lakini tatizo moja tu nilokuwa nalo ni kwamba kampuni nyingi nilizouliza vifaa vyao gani hutumia, wamenitajia majina tofauti kabisa na hata Motorola imo ndani na sio hawa jamaa.
Isipokuwa wamesema hata hivyo tukiachana na kampuni hiyo ni chaguo lako mwenyewe unataka vifaa gani kama vile unataka Music system ya Sony over Panasonic lakini sio jukumu la Sony kuprovide hadi urushaji wa radio nchini.
Hii Mjomba ni Monopoly, haiwezekani hawa jamaa wakawa ndio watengenezaji kisha leo wawe provider kwa wananchi kwa kutumia vifaa vyao wenyewe.
Labda kama sikuelewa vizuri hiyo habari iliyotangulia lakini mjomba hapa pananuka kiharufu fulani nisichokipendelea. Hata hivyo nitafanya uchunguzi zaidi wa hii kampuni pamoja na kwamba yaonyesha kuwa ni jina kubwa.
Maajabu ni kwamba sijawahi kuisikia which is not a big deal - hayo makao yako makuu hapo Markham ni usawa wa toka mjini Dar hadi Ubungo toka hapa napoishi lakini ndio kwanza naisikia kampuni hii ktk Ulimwengu huu wa service provider tena nchi kama hii ambapo matangazo huwa ndio kitoweo cha biashara zao, bila matangazo chakula hakishuki!
Nimepitia pia site yao nimevutiwa na mengi lakini hata hivyo kwa services zake, hakuna huduma kama hiyo kwa wananchi wakazi wa mji huu.
Sasa sielewi kama wao ni Provider kwa njia gani maanake wapohapa provider wengi wengi na wanajulikana.
Nitazidi Kuchimba zaidi kuhusu hawa jamaa.

Koba,
Haya maneno kweli lakini? hiyo habari ya Wamarekani kuwatibu wananchi wa North Korea maanake nachojua mimi marekani wamefunga kila kitu kuhusiana na N. Korea, ni marufuku kwa Mmarekani kwenda Korea ya kaskazini kufanya kazi ama kufanya biashara.
Kifupi kuna video clips chache sana zinazohusiana na N. Korea, hairuhusiwi kabisa kuchukua picha ama video nchini humo hasa na mtu wa nje acha uchuwa Mmarekani ndio kabisaaaa!
 
mkndara niko sure 100% na ninachosema na alikuwa yule mama LISA LING nafikiri unamjua ndio alitengeneza hiyo documentary lakini hao madaktari hawakutumwa na serikali ni wale wa kujitolea kama Drs without borders,na kuhusu hao provider usiwe na wasiwasi maana hiyo ni pesa ya macapitalist sio ya JK kama ya Richmond usifikiri wanaweza kuibiwa kijinga wanajua wanachofanya hao
 
msiwe na wasi wasi vijana WIMAX ni new technology & very fast na haina complications nyingi kuitandaza ni minara tuu kama cell phone hakuna waya hapo wajomba wa kuchimbiwa mahandaki,mnaotaka kujifunza zaidi just google it utaelewa ninachoongea...wimax ni fungakazi inaweza kufungwa mji mzima wa Dar kwa siku moja tuu wote mkao mtandaoni.

..koba,

..tunaijua,ila haiko rahisi kama unavyo-imply!huwezi ifunga kwa siku moja! utai-test lini? kumbuka kuwa inahitaji live testing ili ujue nini cha kurekebisha na kukiweka sawa!

..wasiwasi hapa ni kama kweli hao jamaa watafanya kweli!

..btw,mi naisubiri kwa hamu!
 
Mkandara,
Nam-back Koba hapa, hiyo habari ni kweli hata mie niliona kwenye Geographic channel. Ilikuwa ni issue ya humanitarin mission ambayo si suala la serikali(wajinga wamechora mstari hata kama kuna sanctions,pia ilikuwa about xposing the NOK juu ya ukandamizaji wa serkari yao kwa kupitia hiyo documentary)........kama una taka kuona hiyo documentary unaweza kuinunua toka kwa hao jamaaz thru website yao au piga toll free, si pesa mingi ni tens of $$.
Kuhusu hiyo kampuni ya Wimax hata mie nipo spektical maana hata Barrick ni kampuni ya Canada pia, na huku south of the boarder kuna stories(siyo kwenye nutshell) meaning USA kwamba makampuni ya Canada si maanifu, wanalalamika kwamba wapo sandwiched btn Canada na Mexico juu ya corpoarate irresiponsibility...........anywayz, as even wao wapo responsible!!.
Well, sie kwasababu ndio tunaanza basi chochote tuchukue mambo mengine mbele ya safari, inshallah.
 
Koba,
Ok, nimekuelewa ikiwa kitu hicho ni kama Sicko ambayo leo hii serikali ya Marekani wamefikia hatua ya kutaka kuwafungulia mashtaka wote waliokwenda tibiwa Cuba pamoja na huyo Michael Moore mwenyewe. Unajua yote haya yanategemea na lengo la documentary yenyewe pamoja na kwamba ndio Ukweli wenyewe. Yale yale ya Darwin's nightmare yalikuwa kweli lakini maisha yale sio picha halisi ya Tanzania nzima.
Najua North Korea wako nyuma sana lakini sio kiasi hicho ama jinsi wamerakani wanavyotaka dunia iamini.
Hata ukitazama ranking za huduma za afya duniani utakuta wao Marekani wako chini nafasi ya 36 wakizidiwa na nchi ndogo sana lakini waulize wao watakwambia they have the Best. Pia nchi kama Botswana na sifa zote za maendeleo ziko chini sana bora hata Bongo. Na wengi kati yetu tunaamini Botswana wako mbele!
http://www.photius.com/rankings/healthranks.html

Kwa kuhitimisha hili la wireless nadhani kitu muhimu hapa ni huduma yenyewe ikiwa hawa jamaa kweli wanaweza funga mitambo ya wireless Tanzania nzima kisha wakaendesha biashara wao wenyewe nadhani hii ni risk ya kutosha kwa kampuni hiyo maanake sio rahisi mtengenzaji kuwa msambazaji na mara nyingi sana bei za mtengenezaji anapoingiza mali zake dukani huwa ni ghali vibaya sana kutokana na kwamba mtaji wake unategemea mauzo ya rejareja. Ndio maana hata ukitaka Music system toka duka la Sony huwa ni ghali zaidi ya duka la mtaani kwa system hiyo hiyo.
Sababu kubwa inayoleta tofauti hizi ni kwamba Agent huwa amekwisha weka mtaji kama dhamana ambayo fedha hupokelewa hata kabla ya mauzo. kama unavyonunua tiketi ya ndege, Ukienda British Airways siku zote utalipa ghali kuliko agent wao sasa fikiria kuwa Airbus ndio wanafungua/wanamiliki Air Tanzania, kweli hiyo Air Tanzania itakuwa na Boieng ama ndege nyinginezo?
Sijui mjomba kuhusu hili hata kama ni wawekeshaji na jina kubwa Canada lakini kuna mengi yamenipa kiharufu.

YournameisMINE,
Mjomba kuhusu kampuni za Canada usitake kuwasikia hao South of the Border kwani hawasemi ukweli hata kidogo. Mengi ya Makapmuni makubwa Canada ni mali za Wamarekani, hata hiyo Barricks wanatumia jina la nchi Canada (kweli wnalipa taxes) kwa sababu Wajinga wengi huko duniani wanafikiri Canada ni nchi ya Malaika na Ma -saints kumbe uchumi wa nchi hii unajengwa na hao hao Wayahudi waliowekesha Marekani, UK, Canada na kwingine kote. Wanachofanya ni kubadilisha jina inapobidi lakini mzushi na mcheza stunt ni yule yule..wala sintashangaa kama hawa jamaa walioingia TZ ni Wamarekani ila wameweka Mkataba na kampuni hii kwa kutumia jina lao ili wasifanye makosa yaliyofanywa wakati wa Richmond. Kumbuka kitu cha kwanza wananchi walichofanya ni kupeleleza hii kampuni ya Richmond imewahi kusambaza Umeme wapi?.. kisha maswali yakajengwa na wao kwa ujinga wao wakaweka madai ma kujenga website ya haraka haraka kuonyesha kuwa wana Ubia na Boieng. Website yao ilijengwa within a week na ilitisha sana mambo wanayoyafanya..Mjomba kusambaza wireless nchi nzima ni investment kubwa sana na mtego mzuri sana kwa monopoly.
Mimi nachoona hapa ni kutorudia makosa walokwisha yafanya hivyo wamejiweka sawa this time. Hata hivyo weekend hii nitatembelea hiyo address yao nione madudu yao kuzoa moja mbili ya kampuni hii, kwani hadi sasatunavyozungumza hakuna kampuni yenye jina hili inayotoa huduma za wireless hapa pamoja na kwamba site yao imeonesha mambo makubwa!
Stay tuned!
 
Mkandara,
Tupo pamoja ndugu yangu,ile post yangu ilikuwa "loaded" na hayo yako na mengine zaidi........bado sisi tunafanyiwa visa na wakuu wa dunia hii, lakini kwa mwendo wa kinyonga mambo yatakuwa poa. Inshallah.
 
Hila jamani kuhusu hili, mimi kuna sehemu moja niliongelea suala la tanzania kuwa na mawasiliano hasahasa ya Mitandao ya Internet.

Suala nililo ulizwa lilinikatisha tamaa kabisa. Nalo ni hivi watanzania wataweza kusomaje Websites? Maana karibia zote zina lugha za kigeni(kiingereza) na watanzania asilimia kubwa Vijijini na bahadhi ya miji hii hawaijui.

Swali lilikuwa kuna initiative gani ya kuwawezesha kuelewa kilichoandikwa?

Kwa kweli huyu jamaa kwa sababu hakuwa Mtanzania, nilijitahidi kumweleza lakini akaonekana anaelewa Tanzania na Watanzania kuliko ninavyoelewa.

Sasa jamani mwenye data, kwanza ni kweli watu wa Vijijini hawawezi kusoma Mitandao?

Na kama hawawezi je kuna initiative gani za kuhakikisha wanaweza. Kumekuwa na pesa nyingi sana za kuhusiana na ICT kutoka kwa donars Je kuna lolote ambalo limeisha fanyika kuhakikisha watanzania wanawezeshwa kupata mawasiiliano bila kuathiriwa na Lugha yetu?

Nafikiri tunatakiwa kufikia wakati tukakubali kama Investment ya kutuwezesha watanzania kuelewa kiingereza ni kubwa basi tuwekeze katika kiswahili basi. Tuhakikishe tunatengeneza platform za kuweza kutafsiri kiingereza/kifaransa na Lugha nyingine kwenda kiswahili hili tusifaidi watu fulani tu.
 
Good news for consumers, because this bring more choices and definitely cheaper price. Good move.
 
in ICT;

This is called last mile solutions, meaning a link to the end user; Tanzania has never have this problem so far; there are several solutions and several last mile service providers so we have plent alternatives;

Our Main challenge has been the Backbone, while Kenya have connected allmost all towns with high speed media [Fibre Optic] and now connecting the country to the rest of world through fibre to the indian ocean, in Tanzania we are still relying on multiple microwaves links, which are limited with capacity, and this has been installed by each service providers, hence redundance of resources, eg. Voda, Tigo,Celtel,TTCL each have microwave backbone to Arusha, Dodoma etc... this is nonsense,,,

Why; Regulartory alikuwa amelala, sijui kwamba ameamka kitandani hata sasa!!!

Second,

Today, These organisations have un-used fibre optic capacity build by our taxes, TAZARA [DAR-TUNDUMA], TRC[DAR-TABORA], SONGAS[DAR-LINDI], TANESCO[DAR-KIHANSI], [DAR-TANFGA], [DAR-ARUSHA] etc,,, and almost everywhere where the national grid is installed, but till today we have not connected these high way pathways in terms data,,, and we are just waiting for them to be obsolete.

We have big problem guys!!!
 
Kakindomaster,
Swali zuri isipokuwa kwanza turudi nyuma ktk mambo madogo sana. Ikiwa Tanzania ya leo hasa huko vijijini hata redio hawana uwezo wa kuinunua na wachache waliyonayo huiweka kijiweni (Ujamaa) kusikiliza mpira ama vichekesho, leo hii tukianza kufikiria mtandao kwa wananchi wote sidhani kama tumesha fikia huko.
Jua kali mjomba jua kali, hata feni la ndani (kama lipo) huwashwa kwa mgao ndi maana tunasisitiza zaidi maisha bora kwa wananchi wetu kuwawezesha hata kupata mlo mmoja wa uhakika kwa siku.
Labda kizazi kijacho nasikia siku hizi darasa la Kiingereza linalipa yaani tution yake ghali kuliko hesabu na sayansi!..
Mwendo mdundo, Kibongo bongo tutafika!
 
Good news kwa hao wenye access ya hizo wireless computers.Lakini huko Kibondo,Nkasi,Gezaulole,Sekenke,Malinyi,etc what they want to hear ni maji,umeme wa kuaminika,barabara nzuri,madawa hospitalini,nk/ "maisha bora kwa kila Mtanzania" in terms of unafuu wa maisha.

Kaka tumeitika kwa hoja yako but hii technology isingeliwasubiri wananchi wa Malinyi,Senkenke na kule kwetu,acha tuende kwa stahili hiyo ndiyo kurithishana teknolojia ndg yangu.
 
in ICT;

This is called last mile solutions, meaning a link to the end user; Tanzania has never have this problem so far; there are several solutions and several last mile service providers so we have plent alternatives;

Our Main challenge has been the Backbone, while Kenya have connected allmost all towns with high speed media [Fibre Optic] and now connecting the country to the rest of world through fibre to the indian ocean, in Tanzania we are still relying on multiple microwaves links, which are limited with capacity, and this has been installed by each service providers, hence redundance of resources, eg. Voda, Tigo,Celtel,TTCL each have microwave backbone to Arusha, Dodoma etc... this is nonsense,,,

Why; Regulartory alikuwa amelala, sijui kwamba ameamka kitandani hata sasa!!!

Second,

Today, These organisations have un-used fibre optic capacity build by our taxes, TAZARA [DAR-TUNDUMA], TRC[DAR-TABORA], SONGAS[DAR-LINDI], TANESCO[DAR-KIHANSI], [DAR-TANFGA], [DAR-ARUSHA] etc,,, and almost everywhere where the national grid is installed, but till today we have not connected these high way pathways in terms data,,, and we are just waiting for them to be obsolete.

We have big problem guys!!!

Kilitime,
Hiyo technology wanayosema watafunga TZ sio last mile solution. Wimax inaweza kutumika kwenye last mile solution, kwa maana kwamba tayari una mtandao wako na unatumia wireless kufikisha huduma kwa urahisi sehemu ile ambayo vinginevyo mtandao wako
ungelikuwa ngumu au expensive (the last mile). Kitu ambacho sio kwa hawa jamaa.

Koba, amesimplify kweli argument yake kiasi kwamba kama ingelikuwa kweli basi ISP (Internet Service Providers) wote wapya huku West wangekimbilia hiyo technology kwasababu ingelikuwa cheaper kwao.

Ulichoandika kuhusu backbone ndicho hasa tatizo la TZ. Bila kuwa na backbone network ya kueleweka hayo mambo mengine yote ni fire fighting exercise and will not help us in the long run.

Hii Wimax kama inavyopendekezwa haiwezi kusaidia kuwafikia Watanzania walio wengi huko wilayani na pia itakuwa expensive kwa sababu ni technology mpya na bado iko kwenye utekelezaji.

Kinachotakiwa ni kutengeneza backbone ya nchi nzima, kikubwa kuwapa TTCL uwezo wa kutengeneza hiyo backbone, kuna sehemu nyingi tayari. ISP wapya baadaye watashirikiana na TTCL kununua
capacity ili kuweza kufikisha huduma zao huko wilayani.

Hiyo technology inayopendekezwa ni ya vigogo ambao watakuwa na uwezo wa kumuda gharama. Tena nilivyoelewa ni fixed solution, sio mobile, yaani huwezi kuitumia ukiwa uko kwenye gari kati ya Dar na Moro. Sasa faida yake si itakuwa ndogo kuliko hata hiyo solution ya TTCL? Wimax mobile solution tayari iko kwenye market lakini bado ni mpya na aghali na sio hiyo wanayotaka kufunga Dar na mwanza.

Kuhusu mapesa yote ya ICT yamefanya nini, kwasehemu kubwa hayajafanya kazi inayotakiwa. Miundo mbinu kumejaa ukiritimba na pia kuna watu wengi ambao hawaijui hiyo technology ndio wako pale wakiongozwa na waziri wao Chenge ambaye naye ni mbumbumbu kwenye ICT.

Wengine ni wadau kwenye hili lakini inasikitisha jinsi mawasiliano kwa TZ yalivyo hafifu na aghali. Technology ipo sasa nashangaa kwanini tuna sua sua na kukimbia technologies ambazo huenda kwa mazingira ya TZ zikawa ngumu kuziendeleza kwa muda mrefu.
 
Back
Top Bottom