Kakindomaster,
Swali zuri isipokuwa kwanza turudi nyuma ktk mambo madogo sana. Ikiwa Tanzania ya leo hasa huko vijijini hata redio hawana uwezo wa kuinunua na wachache waliyonayo huiweka kijiweni (Ujamaa) kusikiliza mpira ama vichekesho, leo hii tukianza kufikiria mtandao kwa wananchi wote sidhani kama tumesha fikia huko.
Jua kali mjomba jua kali, hata feni la ndani (kama lipo) huwashwa kwa mgao ndi maana tunasisitiza zaidi maisha bora kwa wananchi wetu kuwawezesha hata kupata mlo mmoja wa uhakika kwa siku.
Labda kizazi kijacho nasikia siku hizi darasa la Kiingereza linalipa yaani tution yake ghali kuliko hesabu na sayansi!..
Mwendo mdundo, Kibongo bongo tutafika!
Mkandara,
Lengo la ICT ni kusaidia kuondoa hiyo digital divide. Lengo sio tena kwa kila mtu kuwa na radio yake, bali kuwa na vituo vingi vya mawasiliano wilayani ambako watu wanaweza kukutanika pamoja kama kuna jambo muhimu na kusikiliza au kuelemishana na zaidi kutumia ICT kuendeleza shughuli zao za kilimo na biashara.
Tatizo kwa TZ ni ubabaishaji ulioko kule wizarani, jamaa wengi
wana mawazo ya leo na kesho, they are not thinking big.
Pesa nyingi za ICT zimetumika isivyo kwa miradi njiwa badala ya kukaa na stakeholders kuangalia tufanyeje ili kutumia huu mwanya kwa ajili kuendeleza nchi yetu. ICT inaweza kuwa kama barabara, itakakofika maendeleo yatafuata, lakini kinachotakiwa ni mikakati ya maana yenye lengo la nchi na uzalendo na sio hii ya sasa ya kuwaridhisha wafadhili.
Mobile phones companies wamefanikiwa kile ambacho hakuna aliyetegemea, challenge ya ICT ni kubwa zaidi maana ina gharama zaidi, inahitaji serikali kusaidiana na wafanyabiashara kuhakikisha inafanikiwa kupitia PPP(Public private Partnership).