Tanzania: The Electronic And Postal Communications (Online Content) Regulations, 2017

Tanzania: The Electronic And Postal Communications (Online Content) Regulations, 2017

Jamani mnaojua mambo ya mitandao hivi wataweza kudhibiti hata mtandao wa facebook?
 
Mtawala anapofikia muda wa kuangamia Mnyezi Mungu humsahaulisha kuwa kuna kufa. Kumbuka kisa cha Nabii Ibrahim na Namrooz ambaye ni baba wa madikteta. Nabii Ibrahim wakati anamlingania amuogope Mungu, akimwambia Mungu pekee ndiye mwenye kuleta uhai na yeye pekee ndiye mwenye kufisha, Namrooz akawaleta watu wawili. Mmoja akasema auwawe na mwengine akampa nafasi aendelee kuishi. Hilo linaonekana ndio mwenendo wa Madikteta wote. Sina haja ya kuelezea yaliyomkuta Maalim Seif na Profesa Lipumba. Lakini kitu kimoja kilimshinda Namrood pale Nabii Ibrahim alipomwambia Mungu wangu na Mungu wa kila kitu analitoa jua mashariki sasa Namrooz wewe litoe magharibi. Namrooz ashindwa. Sasa dikteta yoyote anajiona Ana uwezo zaidi ya Mungu. Anaweza kutumia maneno ya ulaghai kujifanya anamuogopa Mungu, lakini Mungu humsahaulisha. Utakuta matamko yake ni kinyume cha Amri 10 za Mungu. Je, ukituma watu wakatoe roho ya mtu, anafanya hivyo kwa kusema tuko vitani ni lazima mtu huyu akalale...
 
Tutafika, ila kama wapenda kutukana watu kama yule dada wa Instagram lazima sheria ikunyooshe na uadabike kabisa..
 
Tutafika, ila kama wapenda kutukana watu kama yule dada wa Instagram lazima sheria ikunyooshe na uadabike kabisa..
Hao walioshindwa kutumia uhuru vizuri ndio wanaponza na wenzao...sidhani kama kuna nchi Africa ina vijana wenye matusi kama Tz...natembelea blogs za Nigeria...watu wana staha...si wabongo aisee...
 
Kuna cku itatungwa ya kulala,alafu watamalizia muda wa kuinama kusujudu Mkuu wa kaya ,ole wao watakao kaidi
 
Tutafika Mkuu.Wanaoweka hizo sheria wa nadhani watakuwepi madarakani Maisha.Sheria hizo hizo zitakuja kuwabana wao wenyewe.Muda ni dawa.

Mtoto akililia wembe mpe
Hahahaha. Sheria ni msumeno
 
Washamba wanavyonyosha nchi wanataka hadi mawe yaongee ... La sivyo udikiteta uchwara hauwezi kukomaa na kuwa udikiteta kamili
 
Sasa hivi unajua kabisa mtu akitoa matamko yasiyo ya kusifia viongozi watawala tayari uhuru wake unakuwa mashakani!
Nadhani walio salama ni wale wanaojadili USA vs North Korea, huu ndio ungekuwa uchochezi mkubwa maana unahatarisha amani ya dunia na unahusu nguvu za kijeshi. Napata shaka nguvu ya hoja inapozimwa kwa mabavu!
 
Utafikiri hii ni nchi ya wakaldayo yenye sheria lukuki zaidi ya 30000 na bado decree
 
cf4906afd77210576299ff687e435067.jpg

Wadau, tuchangamkie hii fursa tukaende na kutoa maoni yetu.

Kama kuna jambo tunaona litaathiri matumizi yetu ya mtandao, twende na kuwaeleza wazi.
 
Kibatala yupo,

Hivi mwanza na mbeya huwa kuna mawakili?

Maana mawakili wenye nguvu,uthubutu ni Dar na Arusha

Hizi kanuni za kupiga chini mahakamani kwanza kwa kuzizuia zisifanye kazi,pili kufungua kesi ya kikatiba

Mambo mengi tunayoyajua yalianza kama habari za kufikirika,

Kuzuiwa kwa bombadia na wanaotudai ni mfano mzuri,serikali kukopa dola milioni 500 kwa riba ya dola milioni 400,ilianza kama tetesi,kutekwa kwa Roma,Ney wa Mitego

Hizi loophole wanataka kuziziba

Na kwamba habari ifutwe ndani ya masaa 12,Roma ilichukua zaidi ya siku mbili kwa bashite kusema atamleta!!!!! Sasa ukiifuta hiyo habari inakuwaje?
Kwann umeuliza khs mwanza na mbeya
 
hivi wakuu haiwezekani kuhamisha mitambo nje ya nchi??mbona Mange hakamatwi and she is far worse than JF
 
Back
Top Bottom