Nawapongeza wananchi na muungano wa Upinzani nchini Burkinafaso kwa Maandamano makubwa yalimuondoa mamlakani Dikteta Blaise Compaore.
Zaidi nalipongeza Jeshi la Wananchi wa Bukina Faso kwa kusimama na Wananchi.
Eti walitaka wabadili katiba bungeni kw wingi wao kisha washeherekee kwa ngoma na kukata viuno kama wale wa CCM walivyofanya kule Dodoma baada ya kupindua maoni ya wananchi
Jeshi la Burkina Faso Ni Jeshi la Wananchi kweli kweli.Hili ndio jeshi jasiri linalojitambua.
I wonder the kind of stuff our African Leaders are made of.
This is the same man who came into power almost three decades ago but still wants to cling onto it to the grave,Chai! !.
Africa must have a fundamental issue.
When few leaders turn the public offices as their birthrights,and when the poverty level of their governed majority become unbearable ,Revolution is inevitable.
Tanzanian government and the ruling party should take note.
Get prepared.
Mwenzako akinyolewa zako tia maji. Hii ndio dawa ya Marais wasaliti kwa wananchi wao na kudhani kuwa urafiki wao na Marekani au Ufaransa utawasaidia pale wananchi wanapoamua.
Wananchi wa Burkina Faso walimua kupambana barabarani na Dikteta aliyekaa madarakani kwa zaidi ya miaka 27 sasa na anabadili katiba ya nchi ili agombee tena Urais kwa kupeleka mswada Bungeni kwa matarajio kuwa wingi wao Bungeni ungetosha kupitisha lolote.Alitaka agombee kwa awamu ya Tano.Wananchi walizingira Dodoma yao na kuchoma moto jengo la Bunge na maandamano makubwa huku baadhi ya askari wakiwafyatulia Risasi.
Rais Blaise Compaore ambaye yupo katika list yangu ya wasaliti wakubwa wa Africa amevuna alichopanda.
Mwaka 1987 alimpindua rafiki yake wa Tangu Utotoni Thomas Sankara na kumuua kikatili. Thomas Sankara ambaye ninamuhusudu kama mwanamapinduzi halisi wa Africa,Adui wa Ubeberu na muumini mwenye msimamo mkali wa Mrengo wa Kushoto alianza kwa kasi kuijenga Burkina Faso akawa tishio kwa mataifa ya Magharibi kabla hajapinduliwa na kuuawa na huyu Kibaraka wa Magharibi. Malipo ni hapa hapa Duniani . Burkina Faso wameamua.
Blaise Compaore aliyekua mtu wa Kujipendekeza Ufaransa na Marekani na kujifanya kuwa msuluhishi wa migogoro kwenye Ukanda wa ECOWAS leo Marekani na Ufaransa wanatangaza kusimama na wananchi wa Burkina Faso.
Burkina Faso ni ya 4 kwa uzalishaji wa Dhahabu Baada ya Afrika Kusini,Ghana na Tanzania lakini takribani nusu ya Raia wake wanaishi chini ya Dola moja kwa siku huku chama tawala na viongozi wakijilimbikizia mali na kushirikiana na makampuni na serikali za nje kusaini mikataba ya siri na kusifiwa mara kadhaa na Marekani na Ufaransa kama taifa la kuigwa kidemokrasia na utawala bora.Tanzania haina tofauti
Ndio ninasema Utawala wetu hauna tofauti na utawala wa Burkina Faso na pia aina ya viongozi wetu hawana tofauti.
Natazamia hali iliyoanza kujitokeza ya kugombania madaraka kati ya Mkuu wa Majeshi Jenerali Traore na Luteni Kanali Isaac Zida itapatiwa ufumbuzi wa haraka kupitia timu ya dharura iliyoundwa na kamisheni ya Umoja wa Afrika, ECOWAS na UN .Serikali ya mpito irejeshe utawala wa kikatiba na kuondoa hali ya hatari(Emergency State) iliyotangazwa tangu juzi.
Tangu vuguvugu la mapinduzi ya uarabuni lilipoanza kumetokea mapinduzi na majaribio 6 ya kupindua Serikali za Afrika.
Narudia tena,Mwenzako akinyolewa basi zako tia maji.
Vijana wa Tanzania tuna mengi ya kujifunza kutoka Burkina Faso.
Tena nalipongeza Jeshi la Burkina Faso kusimama na wananchi.
Mwisho natoa wito kwa serikali ya Tanzania kupitia waziri wa Mambo ya Nje Bernard Membe itoe Msimamo wake kuhusu kutambua Mapinduzi ya Serikali ya Burkina Faso,isimame na kaka na dada zetu wa Burkinabe na pia ifanye jitihada za kuokoa watanzania ambao kwa namna moja au nyingine wako stranded kwenye machafuko Nchini Burkina Faso.
Pumzika kwa Amani Mwana wa Africa Thomas Sankara(Che Guevara wetu tuliyenyang'wanywa na Wasaliti wa Afrika), Mungu Ibariki Afrika ! We Shall Rise Again !
Aluta Continua,Victory Ascerta....
Ben Saanane