Watu wakiamua system zote zinafeli. Waliweza kuvunja ukuta wa Berlin, Waliweza kumuondoa Nicolae Causescu, Waliweza kuing'oa serikali ya kipolish, Waliweza kumng'oa Charles De Gaulle, Waliweza kung'oa Napoleon,Waliweza kuung'oa utawala wa kikaburu, Wameng'oa kibaraka Mobutu, wamemg'oa Hosni Mubarak. Na ile ya Mtwara .....ilikuwa ni pasha pasha tu. Unachotakiwa kujua kwamba Watanzania wakigairi itakuwa ni kilio kwako wewe na wenzio mnaoamini Tanzania ni mali yenu. Mmezaliwa ikiwa ya kwenu. Nyerere aliwaambia tahadharini na kimya. Hakumwambia Muyaka bin Hajj (Soma Uongozi wetu na hatima ya Tanzania)aliwaambia watu kama nyinyi msiojua kusoma nyakati. Itafikia wakati risasi na mabomu yatakufa ganzi wanajeshi sio mashine, ni binadamu ingawa wanaowatuma wanaamini wao ni mashine inafanya kadiri unapoiendesha. Na wewe kama ni ajenti wa UWT jua kwamba watu wamechoka na hakuna anayejishughulisha na kulamba mfumo ama watu wenye dhamana ya kusimamia mfumo ulio mahututi miguu. Wanaangalia mambo ya msingi. Elimu, uwajibikaji, uongozi bora, demokrasia, utawala bora na jamii ya watu yenye usawa na umoja wakiheshimiana.
Kwa kukuhakikishia tu. Wazanzibari wanaweza kulianzisha wakati wowote waambie wenzako .